*****SORY MADAM*****(29)
AGE.........................................................
....................18+
WRITER......................................................
..............EDDAZARIA G.MSULWA
WAALIKE NA WEZAKO KULIKE HII PAGE.ASANTE
ILIPOISHIA
Kwa nguvu zungu zote nikarusha teke lililo mpiga
kwenye miguu yake kwa nyuma na kumfanya
aanguke kama mzigo wa kuni na akaangukia pua
kitendo kiliho shuhudiwa na watu wengi ikiwemo
askari walio anza kukimbia wakija kwenye eneo
tulilopo huku bunduki zao zikiwa mikononi
mwao huku wakinimrisha nisifanye kitu cha iana
yoyote na John akabaki akiwa haamini kitu alicho
kiona
ENDELEA
Nikamnyanyua mwanasheria wa serikali na
kumuamrisha kuelekea lilipo gari lake na askari
walio kuwa wakinifwata wakajikuta wakisimama
huku wakionekana kunishangaa.Ila mmoja wao
akanifwata akiwa na bunduki yake na
kumbukumbu zikanikumbusha kuwa ni askari wa
getini ambaye mara ya mwisho alinisaidia katika
kotoroka mikononi mwa baba
"Eddy vipi tena?"
"Safi"
Nilizungumza huku nikumuongoza mwanasheria
hadi kwenye gari lake nikamuomba funguo yake
kilazima na akaitoa kabla sijaingia kwenye gari
nikastukia nikiguswa bega na nikageuka
nikakutana na sura ya askari wa getini
"Kaka Eddy huyo mkuu ana nini?"
"Si unamkumbuka yule binti niliye kuwa naye
siku ile tulivyo kuwa tunatoroka home?"
"Ndio si amehukumiwa kifuno cha maisha
tayari?"
"Ndio ila kwa kosa la kuonewa sasa ndio huyu
---- ninamuomba anipeleke alipo anakazi ya
kunizingua hapa"
"Ahaa mimi ninapajua tunaweza kwenda pamoja"
Tukaingia ndani ya gari na kumkabidhi askari
wetu wa getini funguo ya gari na safari
ikaanza.Kitu ambacho ninakishukuru kutoka kwa
askari wetu wa getini ni kuwa mtu muelewa japo
ni askari wa jeshi la polisi ila mama alipendekaza
kuwa askari wa kuilinda nyumba yetu kutokana
na upole na hekima aliyo nayo ni tofauti na
maaskari wengine ambao wana dharau kiasi
kwamba mtu unashindwa kuwadhamini katika
maisha
"Kaka Eddy unajua hata mimi niliamini kuwa
umefariki dunia?"
"Sijakufa ndugu yangu ila wee acha tuu"
"Basi unajua habari za kifo chako zilinistua kiasi
kwamba nikawa nipo njia panda kwa maana yule
binti kwa muonekano anaonekana anakupenda
kiasi kwamba hasikii la mtu juu yako sasa
sikuelewa nilipo ambiwa kuwa amesababisha kifo
chako"
"Najua zote ni mbinu za mzee ila zitafikia
mwisho"
"JAMANI NINAOMBA MUNISIKILIZE"
Mwanasheria wa serikali alizungumza na
kutufanya sote tukae kimya na kumsikila kitu
anacho taka kutuambia
"Jamani ukweli ni kwamba Sheila hajanyongwa
japo mahakama ilitoa hukumu ya namna hiyo"
Sote tukajikuta tukiguna kila mmoja kwa mtindo
anao ujua yeye mwenyewe kiasi kwamba
tukabaki tukimsikilizia kitua atakacho
kizungumza
"Ukweli ni kwamba Mr Godwin alitokea
kumpenda yule binti na akahitaji tuweze
kumhukumu hivyo ila yeye amepanga safari ya
kwenda naye kuishi visiwa vya Komoro na hapa
ninavyo zungumza amenitumia meseji akidai
yupo uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya
kuelekea visiwa vya Comoro"
Nikajihisi nguvu za mwili zikiniiishia kiasi
kwamba nikabaki nikiwa kimya nisijue nini cha
kufanya na hasira kali dhidi ya baba yangu
ikanipanda na kujikuta nikinyang'ata meno yangu
kiasi kwamba sauti ya msuguano wake ikasikika
kwa kila mtu.
"Muheshimiwa amekuambia kuwa anaondoka na
ndege ya saa ngapi?"
"Ngoja niwaonyeshe meseji aliyo nitumia"
Mwanasheria akatoa meseji aliyo tumiwa na
baba na kuanza kumuonyesha John ambaye
nikamshuhudia akishusha pumzi nyingi kiasi
kwamba akionekana kuchoka na kile alicho
kisoma na kabla hajamuonyesha askari wetu wa
getini nikampokonya simu na kuisoma meseji
iliyopo kwenye simu yake
{MR KILONGO MIMI NIPO NIPO UWANJA WA
NDEGE NINAELEKEA VISIWA VYA COMORO KULA
RAHA NA HUYU MTOTO,JANA NIMEMUONJA NI
MTAMU SANA.ILE PESA NIMEKUINGIZIA KWENYE
AKAUNTI YAKO ASANTE KWA KAZI NZURI ULIYO
IFANYA NA HAKIKISHA UNAMALIZIA JUHUDI ZA
KUZIBINAFSISHA MALI ZA MKE WANGU
NITAKUPA ROBO YA UTAJIRI WANGU}
Nikabaki nikiwa ninatetemeka kwa hasira kiasi
kwamba nikajihisi michuruziko ikinitoka puani
kwangu na matone baadhi yakadondoka kwenye
mapaja juu ya nguo za wauguzi nilizo zivaa na
kugundua kuwa ni damu ndio zimenitoka puani
na sikujua zimesababishwa na nini kwani ndio
mara yangu ya kwanza kutokwa na damu za
puani.John akanipa kiatambaa chake na kujifuta
damu zinazo nitoka na askari akasimamisha gari
pembeni ya barabara na wakaniomba nishuke
nipigwe na upepo wa wa halisi kulilo IC iliyo
tawala ndani ya gari
Nikashuka na kuinama chini na damu zikanitoka
kidogo na chakumshukuru Mungu zikakata japo
kichwa nikaanza kukihisi kikiwa kimetaliwa na
maumivu makali
"Unajisikiaje?"
"Kichwa kidogo kina gonga"
"Noja tukakutafutie dawa"
"Hapana twendeni air port"
"Utaweza kweli Eddy?"
"John usijali kwa hilo nitaweza tu"
Tukaingia ndani ya gari na safari ikaanza upya na
kwawakati huu tukaelekea uwanja wa ndege na
hatukuwa na uhakika sana kama tunaweza
kuwaona baba na Sheila au laa.Tukafika uwanja
wa ndege na sote tukashuka kwenye gari na
mimi nikawa wa kwanza kuelekea sehemu ya
abiria na nikajitahidi kuyapa wepesi macho
yangu katika kuwatazama watu wengi waliopo
kwenye eneo hili ili niweze kuwaona baba na
Sheila ila juhudi zangu zikagonga mwamba kwani
sikuweza kuwaona.Kwa kupitia kioo kikubwa
kinacho onyesha sehemu ndege zilipo simama na
kuwashuhudia baba akiwa amemshika Sheila
kiuno wakimalizi ngazi ya mwisho kuingia ndani
ya ndege na kunifanya niaze kumuita Sheila huku
mkono wangu mmoja ukipiga kioo ila
hawakuweza kunisikia na kuwafanya askari
waliopo uwanja wa ndege kunishika na kunizui
kitendo kilicho nifanya machozi kunimwagika
kiasi kwamba nikaanza kupata maumivu ya kiua
John na askari wa nyumbani kwetu wakanichukua
na nikaishuhudia ndege waliyo panda Sheila na
baba ikiacha ardhi na kupaa angani na kunifanya
nishiwe nguvu na kujikuta nikianguaka chini.John
na weza watu wengine wakaninyanyua na sikujua
ni wapi wananipeleka na kujikuta nikiwa kwenye
kitanda cha matairi na kuingizwa ndani ya gari ya
wagonjwa na kupelekwa hospitali.Madaktari
wakaanza kunifanyia uchunguzi na wakanichoma
sindano ambayo sikujua inakazi gani mwili
mwangu
Ndani ya madaa matano madaktari wanipa
ruhusa ya kutoka huku wakiwa wamenifungushia
na baadhi ya vidonge vya kunywa pale nitakapo
tokwa na damu kwani waliniambia chanzo cha
damu kunitoka puani ni kutokana na kuwaza
sana kiasi kwamba mishipa yangu inayopandisha
damu kichwani husindwa kufanya kazi
vizuri.Askari wetu wa getini akanipeleka
nyumbani kwake ambapo anaiishi peke yake
kwenye chumba kimoja alicho pangisha maeneo
ya mbagala rangi tatu.Na tukafika kweye nyumba
iliyo jaa wasichana wengi ambao kitendo cha sisi
kupita mbela yao wakaanza kunong'onezana na
kucheka kwa kicheko kikubwa
"Eddy wazoee ndivyo walivyo hawa wanawake
humu ndani?"
Askari wetu wa gatini alizungumza na sikumjibu
kitu cha aina yoyote na sote tukaingia ndani ya
chumba chake alicho kihaza viti vingi vya
dhamani
"Eddy jisikie huru ndugu yangu"
"Asante"
"Hapa ninaishi peke yangu ila ni mara chache
mke wangu anakuja kutokana yupo masomoni
Arusha"
"Ni mwanafunzi wa sekondari au chuo?"
"Ni mwanafunzi wa sekondari yupo shule moja
hivi ya bodi na miezi minne ya nyuma
wamechoma shule yao ila wazazi wake
wamempeleka shule ya wasichana Iringa"
"Ahaaa anaitwa nani?"
"Salome Alex Edward"
Moyo ukanipasuka na kujikuta nikimtaza askari
wetu wa getini kwani Salome anaye mzungumzia
ni yule miongoni mwa wapenzi wangu japo mimi
na yeye tumeachana kwa katika mazingira ya
kutatanisha na mbaya zaidi ametembea na mkuu
wa shule na ameambukizwa virusi vya ukimwi.
"Yule dogo ninampenda sana hadi imefiki hatua
mimi ninamlipia ada ya Advance"
"Yupo kidato cha ngapi?"
"Kidato cha tano japo sasa hivi anadani kuwa
nimuache asome ndio tutaendelea na mapenzi
imenilazimu nimsomeshe kwani familia yake ni
duni sana"
"Mmmm pole sana ndugu yangu"
"Kwa nini unanipa pole"
"Jukumu la kumsomesha mtu ni kubwa sana na
ikitegema ndio hivyo wazazi wake hawajiwezi
kiuchumi"
"Ndio ndugu yangu si unajua mwanaume
unatakiwa kujikaza na tumeubwa kupambana na
ile pesa uliyonipatia kidogo ilinisaidia kumlipia
ada na matibabu hospitalini"
"Alikuwa anaumwa na ugonjwa gwani?"
"Waliniambia kuwa ni mstuko wa moyo"
"Ahaa ndugu yangu hongera sana"
"Asante ndugu yangu"
John akanionyesha nguo za kuvaa nikitoka kuoga
kutokana ni uswahilini ikanilazimu kutoka na
kindoo cha kuogea huku nikiwa nimeshika kopo
lenye sabuni na John akanionyesha bomba la
maji na nikakuta kuna kindoo kimekigwa
ikanilazimu kusubiri kwa muda na kuna wamama
wawili wapo pembeni wanapika vyakula vyao kwa
ajili ya jioni wakaanza kunong'onezana taratibu
"Eheeee OSAMA BIN LADEN ameingia mbagala
jamani....mabomo yasije yakalipuka tena"
"Shosti sema wewe Obama nikisema mimi Bush
nitaambiwa ninakiherehere"
"Mmmm na hayo mandevu sasa unaweza kusema
kama kama paka aliye mwagikiwa na mchuzi wa
moto"
Moja kwa moja nikajua wananisema mimi
kotokana na jinsi nilivyo na ndavu nyingi ambazo
zimenifanya kuonekana na sura ya
kutisha.Nikabaki nikiwa nimewatazama kwa jicho
la hasira mpaka wakajistukia.Nikaona nikiendelea
kusimama katika bomba watanikera zaidi na
nilicho kifanya ni kuyamimina maji yaliyopo
kwenye kindoo nilicho kikuta na kuyaweka
kwenye ndoo yangu na kabla sijaondoka mama
mmoja akasimama na kunifwata kwa haraka
huku akubwatuka
"Wee wee usijifanye muhuni rudisha hayo maji
sehemu ulipo yatoa"
"Kwani si nimekikinga kindoo chako si kitajaa?"
"Koma mwanaume mzima ovyoo unazani pale
nimekalisha makalio yangu bure...Nimekaa ili
kindoo changu kijae maji"
"Samahani kama nimeuudhi"
Nikayamimina maji niliyo yatoa kwenye kindoo
cha huyu mama ambeye sikujua ni kwanini
amenichukia pasipo kuwa na sababu maalumu
kwani ni siku yangu ya kwanza kufika atika
nyumba hii ila wanaonekana kunichukia sana"
Nikakikinga kindoo changu hadi kikajaa na
kwenda nacho kweye bafu alilo nionyesha askari
wetu ambaye hadi sasa hivi nilisahau jina lake
kani nilisha zoea kumuita afande.Nikaoga na
kumaliza na kurudi ndani kwangu na kumkuta
askari wetu akivaa nguo nyingine za kazini
"Unaondoka?"
"Ndio kaka hapa nimepigiwa simu ninahitajika
lindo si unajua nilitoaka pasipo kuaga
inanilazimu kwenda kufidi muda niliokuwa sipo
kazini"
"Ahaa sawa ndangu yandu ila mbona hawa mama
humu ndani wamekuwa watu wa maneno ya
chini chini?"
"Hao wamama huwa wanapenda kumpima
mtu....hata mimi kipindi nilipokuwa ninakuja
walikuwa wanavimaneno vya chini chini hadi
kuna siku kuna mama nilimzaba makofi ndio
wote wakaniheshimu"
"Wana waume?"
"Ndio wana waume zao ila waume zao nao ni
wanaume suruali"
"Wanaume suruali kivipi?"
"Wanawategemea wake zoa wao kila ikifika
asubuhi hukaa maskani hadi mida ya kula ndio
utawaona wakirudi mmoja mmoja"
"Mmmm ndio maana wake zao wanakuwa na
dharau?"
"Ndio hivyo ndugu yangu"
"Kaka hivi unaitwa nani?"
"Eddy ina maana siku zote hulijui jina langu?"
"Silijui ndugu yangu?"
"Mimi ninaitwa Afande Josephat"
Josephat akanipa elfu kumi kwa ajili ya kununua
chakula cha usiku kisha yeye akaondoka na mimi
nikavaa nguo zake alizo nipa nizivaa kisha
nikaenda kununua chipsi kwenye kibanda kisicho
mbali na sehemu ya nyumba yuliyopo na
nikarudi na kabla sijaingia mlangoni nikakutana
na msichana ambaye sikuwahi kumuona akiwa
anagonga mlango wa chumba cha Josephat
"Mambo vipi kaka?"
"Salama vipi?"
"Safi tuu Jose nimemkuta?"
"Hapana amekwenda kazini"
"Hawezi kurudi leo?"
"Sijajua"
"AHaa mimi ni mgani wake ameniambia kuwa
nije je nimsubiei huku kwake?"
"Mmmm amekuambia saa ngapi?"
"Ahha..si....sijana"
Dada alizungumza huku akiwa anajing'ata
ngat'ata kiasi kwamba sikuwa ninamuelewa ni
kitu gani kilicho mleta na akapita dada mmoja
na akaropoka neno lililo muudhi dada niliye
simama naye
"Wewe Asha ngedere usione chaka mavi
yanakubana utakuja kufa nyoo mwanamke kila
ukimuona mwanaume kidubwasha chako kina
kuwasha"
"Koma na wewe sura mbaya kama kwapa la bibi
kizee"
"Weewee tena utaifananisha sura yangu na hilo
sura lako kama ku** ya changudoa aliye kosa
mteja"
Maneno yao makali yakawafanya wapangaji
waliomo kwenye yumba vyao kutoka wakiwa
wanashangaa majaibizanio yao,Sikutaka
kuwaingilia nisije na mimi nikavurugwa bure
nilicho kifanya ni kuingia ndani na kufungua
mlango na nikasikia masufuria yaliyo pangwa
kwenye kordo yakianguaka huku watu wangine
wakishangilia na nikagundua wanapimana lishe
na nilicho kifanya nikufungulia redio yenye spika
kubwa hadi mwisho na sikuzisikia sauti zao
wakigombana
Baada ya muda ugomvi wao ukaisha kisha na
nikapunguza sauti ya redioa na kuanza kula
nilicho kinunua huku nikiwa siamini kama ipo
siku nitaishi maisha kama haya ninayo yaishi na
mipango ya kwenda ikulu ikaanza kujipanga
taratibu kichwani kwangu na lengo zima ni
kwenda kujua ni jinsi gani wataweza kunisaidi juu
ya kumpata mama.Kwa msongamano wa mawazo
mengi nikajikuta nikipitiwa na usingizi kwenye
sofa moja lililopo kwenye chumba hicho kilicho
jaa vitu vingi na mbaya zaidi kina dirisha moja
tuu
Nikastushwa na mlango unao gongwa huku
nikiisikia sauti ya Josephat ikiita nje ya
mlango.Nikanyanyuka na kwenda kumfungulia
mlango na akaingia huku akionekana kuwa na
haraka sana
"Kaka nimepata safari ya kikazi naelekeaa
Kagera"
"Kuna nini tena?"
"Ni maswala ya kikazi tu na ninaweza kukaa hata
wiki hapo nimekuja na wezangu wananisubiria
hapo nje"
"Ahaaa kwani ni saa ngapi saa hizi?"
"Nane usiku"
Afande Josephat alizungumza huku akidumbukiza
nguo zake kwenye begi na la mgongoni kwa
haraka akachukua vitu vyake muhimu kisha
akatoa elfu hamsini na kunipatia kisha
akaiiandika namba yeke ya simu pembeni na
kuniambia endepo nitapata tatizo lolite nitafute
simu kwa ajili ya kumpigi.Akatoka na mimi
nikarudi kitandani na kujibwaga na kutokana na
uchovu mwingi usingizi ukanipitia tena wa safari
hii ulizidi usingizi wa mwazo
Kwa mbali nikahisi mlango ukifunguliwa
nikayafumbua macho yangu na kugundua
mwanga wa juu ukiwa umetawala ndani ya
chumba changu ikiashiria kumesha
pambazuka.Nikayapeleka macho yangu mlangoni
kumtazma mtu anaye usukuma sukuma mlango
na akaingia kwa haraka
"SAPRAIZZZZ BABY JOS........"
Macho yangu yakakutana na Salome ambaye
alishindwa kuimalizia sentensi yake na sote
tukabaki tukitazamana kwa mshangao huku yeye
akionekana kunishangaa zaidi
ITAENDELEA
*****SORY MADAM*****(30)
Age........................... ...........................18+
Writer........................ .......................Eddazar ia
G.Msulwa
WAALIKE NA RAFIKI ZAKO KATIKA KUILIKE HII
PAGE,ASANTE
ILIPOISHIA
"SAPRAIZZZZ BABY JOS........"
Macho yangu yakakutana na Salome ambaye
alishindwa kuimalizia sentensi yake na sote
tukabaki tukitazamana kwa mshangao huku yeye
akionekana kunishangaa zaidi
ENDELEA
Nikajinyanyua tararibu kitandani na kukaa kitako
huku Salome naye akiliingiza begi lake la nguo
na kuliweka pembeni na taratibu akakaa kwenye
sofa lililopo ndani ya na kuanza kuminya minya
vidole vyake vya mkononi huku sura yake akiwa
ameilekezea chini akionekana kujawa na aibu
kubwa ikanilazimu kuanza kumsalimia
"Mambo"
"Powa vipi?"
"Salama za huko utokapo?"
"Mmmm....?"
"Za huko utokapo vipi?"
"Nzuri tu"
"Karibu mbona unaona aibu?"
"Eheee walaa Jose yupo wapi?"
"Ahh amesafiri kikazi"
"Mungu wangu sijui itakuwaje?"
"Iakuwaje nini?"
"Mmmm hamna mwaya"
Nikanyanyuka kitandani huku nikiwa ninawenge
la usingizi kidogo na nikaanza kuvinyoosha
viungo vyangu huku nikipiga miyayo na kama
kawaida ya wanaume wengi walio kamilika
kimaumbile pale wanapo amka ni lazima koki zao
husimama kuashiria ni siku mpya hii na ndivyo
ilivyo kwangu jambo lililo mpelekea Salome
kuyagandisha macho yake kwenye koki yangu
pasipo kuyapepesa hata kidogo.Nikawasha redio
na kuifungulia sauti ya kawaida kisha nikarudi
kukaa tena kitandani na Salome akatoa simu
yake aina ya Samsung Galax na kuanza kuiminya
minya kisha akaiweka sikioni
"Jose jamani upo wapi?"
"Sasa utarudi lini wakati mimi nipo kwako
nilikuja kukufanyia supriz naona supriz yenyewe
imeharibika"
"Nimpe simu nani?"
"Haya........Eddy ongea na Jose simu ipo hewani"
"Mmmm vipi kaka Jose"
"Safi.....sasa huyo bibie ndio hivyo kaja bila
taarifa"
"Ndio"
"Basi ninakuomba ukatafute hata sehemu ya
kujishikiza kwa hizi siku ambazo nitakuwa sipo
na yeye aishi ndani humo hadi nitakapo rejea"
"Ahaaa powa kaka"
"Hakikisha unafanya hivyo bwana....Huyo ni
Malkia wangu muache ajitanue ndani kwangu"
"Sawa mzee......Chukua simu yako"
"Eeehe baby"
"Ahaa ataondoka eheee"
"Haya kazi njema"
"I love too mwaaaaa"
Salome akakata simu na kuachia tabasamu pana
ila kwa upande wangu nikajikuta roho yangu
ikiwa inauma kupita maelezo kwani kitendo cha
kuambiwa kuondoka kikabaki kikiniumiza na
sikuwa na jinsi ya kufanya.Nikanyanyuka
kiustaarababu na kuzitoa ndala chini ya uvungu
nilizo kwenda kuogea jana usiku na kuzivaa vizuri
na kusimama kwenye kioo kikubwa na kujitazama
jinsi sura yangu ilivyo jaa ndevu zisizo na
mpangilio na kunifanya nionekane kama mzee
wa miaka 70 na zaidi kumbe ni kijana mdogo tu
wa miaka ishirini naa.
"Nawatakia maisha mema wewe na mchumba
wako"
"Eddy unakwenda wapi?"
"Sijajua ila ngoja niondoke"
"Eddy..."
"Salome wewe tayari umesha mpenda mtu
mwengine kuwa na mimi hilo litakuwa ni
ngumu"
"Powa nenda"
Salome akajibu kwa dharau na kunifanya
nimtazame kwa muda huku machozi yakianza
kunilenga lenga na kuyakumbuka mambo mema
niliyo mfanyia Salome kuanzia siku ninampa pesa
ya matumizi kipindi tupo shule na alipo poteza
pasa yake hadi siku ninamkuta na mkuu wa shule
wakitoka kwenye mlango wa chumba cha Hotel
kisha taratibu nikashika kitasa cha mlango
"Salome naamini unaijua afya yako ila ni bora
ukamueleza ukweli Jose kuliko kumuua pasipo
yeye kujua"
"Nashukuru kwa ushauri wako ila ukweli ni
kwamba sijaadhirika kama unavyo dhania"
"Sawa kama ni hivyo"
"Powa nenda usije ukanivunjia ndoa yangu na
mume wangu mtarajiwa....Ila umeachwa nini na
mpenzi wako mbona umechakaa hivyo kipindi
kile nilivyokuwa nikikuomba msamaha ukawa
unanidharau haya pole mwaya"
Maneno ya Salome yakaniumiza kiasi kwamba
nikajikuta nikitokwa na machozi kisha
nikafungua mlango na kutoka nje na mtu wa
kwanza kukutana naye ni yule mama wa jana
aliye ninyang'anya maji yake na baada ya
kuniona akaanza kucheka kwa kicheko cha kejeli
"Heeeheee Osama na wewe pia unalia makubwa
haya"
Nikasimama na kumtazama kwa macho makali
na akaendelea kujichekesha kitendo kilicho anza
kunipandisha hasira na nikapiga hatua za haraka
hadi alipo simama na sura yangu nikaisogeza
karibu na sura yake huku ndevu zangu zikiwa
zinamgusa kwenye mashavu yake na akakaaa
kimya kiasi kwamba akaanza kutetemeka
"NITAKUUA"
Nilizungumza kwa hasira huku nikijitahidi kuizuia
hasira yangu ambayo siku zote ni mbaya na
taratibu nikageuka na kuondoka zangu.Na
nikafika kwenye moja ya maskani na kuwasalimia
watu wote nilio wakuta na mimi nikatafuta
sehemu nikakaa huku nikiwasikiliza mabishano
yao ya mpira dhidi ya timu za afrika zinavyo
fanya vibaya kwenye kombe la dunia la mwaka
huu na jinsi mabishano yao yanavyo endelea
nikajikuta hasira yangu ikipungua
"Alafu wewe jamaa ni mwera(polisi) nini?"
"Kwa nini?"
"Kwa maana umekuja hapa umesalimia na
kuvamia vamia kijiwe cha watu usije ukawa
unatuchunguza?"
"Hapana jamani mimi mtu wa kawaida sana"
"Sio kawaida usije ukasababisha pira(gari la
polisi) likaja hapa ni kutunyanyua"
Jamaa mmoja aliye jazia kifua akanisogelea huku
akiwa na kipisi cha bangi mkononi huku kikiwa
kinawaka kisha akavuta fumba kubwa la moshi
na kuinama na kunipulizia usoni jambo lililo
nikasirisha sana na kujikuta nikinyanyuka na
kumtandika kichwa cha pua na akayumba
nyumba na kuwafanya wezake wapatao wanne
kunivamia na kuniangusha chini na kuanza
kunishambulia kwa mangumi na kujikuta
nikimdaka mmoja sikio lake na kumng'ata kwa
nguvu zangu na kumfanya atoe ukelele mkubwa
huku akisema anakufa na nikamuachia
kumng'ata na akanyanyuka huku damu zikiwa
zinamwagika kwenye masikio yake na gafla
vumbi jingi la gari lililo funga breki za gafla
likasimama na watu walio nishambulia wote
wakakimbia na kuniacha nikiugulia kwa
maumivu.
Nikastukia askari wawili wakiwa wakininyanyua
huku wakinipiga na virungu vya miguu na
wakanisukumia kwenye gari lao walilo kuja
nalo.Kwa wenge la maumivu sikujua ni wapi
wananipeleka.Gari likasimama kwenye mtaa
mwengine na kuwakuta askari wengine wapatao
wanne wakiwa na bunduki mikononi
wakiwaamrisha watu wapatao nane waliokuwa
wamelala chini huku mikono yao wameiweka
kichwani na wanavyo onekana ni wavuta
bangi.Watu hao wakaamrishwa kuingi ndani ya
gari hili la polisi na watu wengi tumezoea kuyaita
‘Defendar' na sote tukajikuta tukiwa tumetosha
na askari wote wakapanda na likaondoa kwa
kasi.Ndani ya dakika kadhaa tukawa tumesimama
kwenye moja ya geti ambalo kwa haraka
nikafahamu kuwa ni gereza la Keko.
Gari ya polisi ikaingia ndani na sote
tukaamrishwa kushuka na kupanga mastari
mmoja huku tukiwa tumechuchumamaa na
tukaanza kuhesabu namba huku na mimi nikiwa
namba tano kati ya watu tisa tuliopo kwenye
eneo hili na tukasimama huku mikono tukiwa
tumewekeana kwenye mabega na kunyoosha
mstari mmoja na tukaaza kutembea huku
tukiongozwa na askari wa magereza hadi kwenye
chumba kimoja cha mahabusu na sote tukaingia
ndani na mlango wake ukafungwa.Nikatafuta
sehemu yangu na kukaa huku nikijutia kitu
kilicho nifanya nikae kwenye ile maskani ni nini.
"Hata nikiwaambia kuwa mama yangu ni waziri
haina tija"
Nilijisemea mwenyewe kimoyo moyo na sikuwa
na uwezo huo kwa jinsi ninavyo wajua askari
wangeniambia mambo ya dharau ambayo
yangenikera zaidi na kunisababishia matatizo
mengi zaidi.Hadi jioni inaingia sikujua ni kitu
gani kinacho endelea juu ya chakula.Usiku
mzima sikuweza kulala kutokana na baridi kali
kwenye sakafu isitoshe tumbo langu tangu jana
usiku halikuuingiza chakula cha aina
yoyote.Mawazo ya jinsi nitampata mama yangu
yakaanza kunitawala kichwani kwangu kwani kwa
maelezo ya John aliniambia kuwa mama yangu
yupo South Africa akiwa anaumwa na amelazwa.
Hadi inatimu asububuhi sikuweza kupata usingizi
na kengele kubwa likagongwa na milango
ikafunguliwa na wezangu wakatoka kwa haraka
na mimi ikanibidi nitoke kwa haraka na
kuwafwata kwa nyuma na tukafika kwenye
sehemu na kuwakuta wafungwa wengine walio
valia sare wakinganyanyiana mabakuli yaliyo
tengenezwa na alumuminiam na nimachafu ndani
ya maji yaliopo kwenye karo na anayepata
chombo chake anakimbilia kwenye sehemu
unapotolewa uji.Nikabaki nikiwa nimesimama na
kutokujua ni nini nifanye kwani nikahisi endapo
nitakunywa uji wao ninaweza nikatapika kwani
una harufu mbaya sana.
Watu wakakanywa uji kisha sisi tulio tolewa
kwenye chumba tukaamrishwa kurudi kwenye
chumba tulicho toka.
"Oya wewe ni mtoto wa mama nini?"
Jamaa mmoja alizingumza na nikabaki nikiwa
nimemtazama pasipo kukjibu kitu cha aina
yoyote huku akininyooshea kidole
"Oya wewe chok* si nanikuuliza wewe ni mtoto
wa mama?"
"Kwani wewe umezaliwa na mbwa?"
"Ahaaa dharau sasa hizo"
"Sio dharau unavyoniambia kuwa mimi ni mtoto
wa mama ina maanisha wewe umazaliwa na
mbwa tena mbwa koko"
"Oya dogo inakuwaje anakuita mbwa koko alafu
na wewe unakubali kirahisia rahisi"
"Na wewe yasiyo kuhusu isiyaingilie ua na wewe
unataka kuitwa mbwa koko?"
Jamaa aliye ingilia mada akanifwatwa huku kifua
chake akiwa amekitunisha na mimi nikasimama
kwa haraka na akanisukuma kidogo na kurudi
nyuma na kwanguvu zangu zote nikamrukia kwa
kutumia bega langu na likatua kwenye tombo
lake na kumsukuma hadi ukutani na kuanza
kumshindilia mangumi na kuwafanya watu
wengine kushangilia kwa nguvu.Jamaa naye
hakuwa nyuma katika kuyajibu mashambulizi
yangu na kusema ukweli ngumi zake ni nzito
kiasi kwamba nikaanza kuona nyota nyota na
kwa bahati mbaya akanisukuma na kichwa
changu kikagonga kwenye nondo ya mlango na
kujikuta nikianguka kama mzigo na kupotaza
fahamu
***
Nikastuka na kujikuta nipo kwenye kitanda cha
hospitalini huku mkono mmoja nikiwa
nimefungwa pingu na pembeni yangu
amesimama askari wa magereza.Nikajishika
kichwani kwangu na kukuta nikiwa nimefungwa
na bandeji kubwa
"Unajisikiaje?"
Askari aliniuliza na kunifanya nikae kimya nikiwa
nikimtazama kwa macho ya unyonge.Askari
akafungua mlango na kumuita nesi kisha na yeye
akarudi kukaa kwenye sehemu aliyokuwa umekaa
hapo awali.Nesi akaingia huku akiwa amebeba
kisinia chenye vifaa vingi na kukiweka pembani
kwenye meza iliyopo karibu na kitanda nilicho
lala na kuanza kunitazama kwenye jeraha lililopo
kichwani kwangu
"Amesha kula?"
"Bado hajakula"
"Ina bidi tuweze kumpatia chakula ili aweze
kunywa dawa"
"Hapa ni wapi kwenye kibanda ambacho
ninaweza kumnunulia chakula?"
"Ukitoka kwenye geti hapo utaweza kuona
kibanda cha wauza chipsi na unaweza
kumnunulia chakula"
"Sawa"
"Akimaliza kula ninaomba uniite"
"Sawa"
Nesi akatoka na kukiacha kisinia chake na askari
akanyanyuka na kutoka nje na nikapata wazo la
haraka nikaanza kutafuta kifaa kidogo
kinachoweza kuingia kwenye shimo la funguo la
pingu na kuchukua kijikifaa kidogo kilichopo
kwenye sinia na sikujua kina kazi gani na kuanza
kuifungua pingu niliyo fungwa kwa utulivu wa
hali ya juu na chakumshukuru Mungu ikafunguka
kisha nikashuka kitandani japo mwili
umetawaliwa na maumivu makali ila nikajikaza
na kuufwata mlango wa kutokea kwenye chumba
nilichopo na kuwaona watu wakiwa wanaendelea
na mishe zao.Nikatoka ila kitu kilicho
nichanganya sikujua askari ni wapi alipo
elekea,nikaanza kutembea kwa umakini huku
nikifwata sehemu yenye mlango wa kutokea na
kwabahati nikamuona kwa mbali askari wa
magereza akija kwa mwendo wa haraka huku
mkononi mwake akiwa ameshika kifuko
cheusi.Nikajibanza kwenye ukuta na akapita
pasipo kuniona na kwaharaka nikatoka huku
miguuni nikiwa sina hata kitu chohote,Nikafan
ikiwa kuondoka eneo la hospitali na safari hii
moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwetu
Japo kuna umbali kidogo ila nikajikaza kutembea
na nikafanikiwa kifika na kukuta geti likiwa
limefungwa,nikakumbuka kwenye sehemu ya
nyuma ya ukuta wetu kuna matofali yaliyo
pagnwa ya mtu mwenye kiwanja chake aye taka
kujenga.Nikazunguka na kuyakuta matofi kama
nilivyo tarajia
"Hivi mwenye haya matofali amefariki dunia au?"
Nilijisemea huku nikianza kuyapanga matofali
karibu na ukuta wetu ambao ni mrefu kiasi kisha
na kitu kingine kilicho niogopesha ni nyaya za
umeme za ulinzi zilizo zungushiwa kwenye ukuta
wa nyumba yetu sehemu ya juu.Ikanichukua
kama dakika kumi na tano kutengeneza urefu wa
ngazi za kuingilia kwenye nyumba yetu na
nikafanikiwa kupanda ukutani huku kwa
hahadhari kubwa nikizikwepa nyaya za umeme
na nikafanikiwa kurukia kwa ndani na ukimya
mwigi umetawala ndani ya nyumba,nikafika
kwenye mlango wa mbele na kukuta umefungwa
na kawaida mlango ukiwa umefungwa huwa
funguo tunazificha kwenye vyungu vya udongo
vyenye mau.Nikanza kutafuta kwenye chungu
kimoja baada ya kingine wala sikuzikuta
"Huyu shetani ameondoka na hizi funguo nini?"
Nikaendelea kutafuta na kwabahati nzuri
nikaziona zikiwa nimefichwa kwenye kindoo
kidogo chenye maua ambayo mama siku zote
huwa huyapenda na kwamadai yake
ameyanunulia nchini Canada na aliyanunua kwa
gharama kubwa kubwa sana.Nikafungua ndani na
kukukuta vitu vikiwa vimeshanguliwa sana huku
kukiwa na chupa nyingi za pombe zikiwa
zimezagaa zagaa kwenye sakafu huku vijimito
vidogo vya masofa vikiwa vimetupwa
tupwa.Nikapanda ngazi hadi chumbani kwangu
na kuingia bafuni na kuoga kisha nikapanda
kitandani na kulala kutokana na uchovu mwingi
sana.
Nikaamka mida ya saa mbili usiku huku niikiwa
nimechoka nikaelekea jikoni na sikukuta kitu
chochote cha kula hata mafriji yote hayakuwa na
kitu chochote,Nikakumbuka kwenye nyumba ya
uwani kuna handaki ambalo mara nyingi nikiwa
nipo likizo nilikuwa nikamuona mama akiingia na
sikujua ni kitu gani anacho kifwata ndani ya
handaki hilo.Nikaingia kwenye nyumba ya nyuma
katika chumba ambacho kuna kitanda kimoja na
kiti kisha nikasogeza pembeni kitanda na
kulisogeza kapeti lilolopo ndani na kuukuta
mlango wa chuma ambao ni mlango wa
handaki.Nikaufungua na kukuta ngazi za kushuka
chini ambapo kunagiza la kutisha sana ikanibidi
nirudi tena juu kutafuta tochi.Nikafanikiwa
kuiona tochi yenye uwezo mkubwa wa wa
mwanga.Nikaingia tena ndani ya handaki huku
tochi ikiwa inawaka,nikaanza kuona picha nyingi
za kutisha zikiwa zimebandikwa kwenye kuta za
handaki hili huku kukiwa na vitu vichache sana
ikiwemo majoho matatu moja likiwa jeusi la pili
likiwa na rangi nyeupe na jengine ni la rangi
nyeusi.Sikujua ni ya kazi gani nikakifwata kitabu
kikubwa kilicho jaa vumbi nilicho kikuta na
kukifungua na kukuta maandishi ambayo sikujua
ni ya lugha gani iliyo andikwa ndani yake
Nikakiacha na kukiona kisanduku kidogo cha
wastani kikiwa kimefungwa na kuwekwa kwenye
kona ya handaki na nikakisogelea na
kukifungua,Sikuamini macho yangu baada ya
kukuta cheni na pete za dhahabu pamoja na
vipande vaya madini.Na nikaanza kuchangua
changua na kukuta pete moja ya madini ya
Tanzanite ikiwa imetengenezwa kwa ustadi
mkubwa huku kukiwa na vipande vingine vingi
vya madini yenye dhamani kubwa na hata
madini mengine sikuwahi kuyaona maishani
mwangu.Nikakibeba kisanduku huki nikiwa nina
furaa kubwa na nikaingia ndani ya chumba
changu na kuvimwaga vitu vyote kitandani na
furaha ikazidi kunitawala hata njaa sikuweza
kuihisi tena na kujikuta nikiaanza kuimba nyimbo
za aina mbali mbali huku nikicheza kiduku
kisicho na mpangilio maalumu.
Nikazikusanya na kuziweka kwenye kisanduku
chake kisha nikaviweka chini ya uvungu wangu
wa kitanda na kwenda sebleni na kuwasha Tv na
kuangalia angalia miziki hadi usingizi
ukanipitia.Cha kwanza baada ya kuamka asubuhi
nikaoga na kuvaa nguo nyingine zilizo nipendeza
na kuingia chumbani kwa mama na kuzikuta
baadhi ya funguo za magari zinapo wekwa
kwenye kabati na kuchukua moja kisha
nikichukua dini moja la kuliweka mfukoni na
kutoka nje na kuingia kwenye gari moja aina
Verosa ambayo mama aliinunu kipindi
zinatoka.Moja kwa moja nikaenda kwa sonara na
kukutana na muhindi mmoja na tukakubaliana
biashara na nikamuuzia kwa milioni kumi
ambazo zinanitosha sana kwenye matumi ya
kwenda nchini Afrika kusini kumuona
mama.Nikaingia saluni moja kiume na kunyolewa
vizuri kisha moja kwa moja nikaelekea benki ya
backrays kwenye akaunti yangu ambayo ni siku
ningi niliifilisi hadi ikabaki kilinda akaunti na
kukiweka kiasi cha milioni saba na kubaki na tatu
na nikaanza mipango ya kutengenezewa hati
yangu mpya ya kusafiri
Na ndini ya masaa machache nikawa
nimefanikiwa kutokana na kuhonga sana pesa
kwa watu wanao husika na utengenezaji wa hati
za kusafiria na hadi ninafanikiwa kuipata
nikajikuta nikiwa nimebakiwa na laki tano na
nusu nusu na nikakata tiketi ya ndege ya shirika
la South Africa Aur ways.Na nikaelekea kwenye
ofisi za wizara ya afya na kukutana na mmoja wa
masekretari wa mama ambaye nina fahamiana
naye vizuri na akaonekena kunishangaa.
"Eddy si nimesikia umefariki wewe?"
"Nani amekuambia?"
"Eddy kila mtu anajua kuwa wewe umeuawa kwa
kuchomwa sindano ya sumu kitendo kilicho mpa
mama yako mstuko na tumemkimbiza Afrika
kusini kwa matibabu zaidi"
"Tena hilo ndilo nililokuwa nimekuja kulijua
mama yangu amelazwa hospitali gani?"
"Amelazwa hospital moja inaitwa Louis Pasteur
ipo mji wa Pestoria"
"Ahaaa asante kwa hilo"
"Ila Eddy niambie ni kitu gani kilicho kupata
hadi ukafufuka kwa maana mimi mwenye kwa
macho yangu niliiona maiti yako ikiingizwa
mochwari ila cha kustaajabu leo hii ninakuona
hapa?"
"Ni historia ndefu ila Mungu akibariki nikipata
nafasi nitakuja kukusimulia ila nashukuru kwa
masaada wako"
"Usijali nakutakia safari njema"
Kutokana tiketi ya ndege niliyo kata inaondoka
saa Mbili usiku ikanilazimu kurudi nyumbani na
kubeba nguo kadhaa na kurudi uwanja wa ndege
kwa kutumia taksi ya kukodi.Nikatafuta sehemu
yenye mgahawa na kujipatia chakula cha kutosha
kwani kutokea asubuhi sikuweza kuingiza
chochote kutokana na mizunguko ya kuandaa
safari.Imebaki lisaa limoja kabla ya safari
nikaendelea kusubiri kwenye sehemu za abiria.
"Samahani kaka hii sehemu kuna mtu?"
"Hapana unaweza kukaa"
Dada mmoja aliye valia suruali ya kubana na
kuyafanya makalio yake makuwa kujichora vizuri
huku akiwa amejiremba na kuonekana mrembo
zaidi alianiambia na baada ya kumjibu akakaa
pembeni huku akiwa na pochi yake kubwa kiasi
na kujikuta nikimtazama kwa jicho la
kuiba.Nikaendelea kusoma gazeti hadi tulipo
tangaziwa abiria shirila la ndege la South Afrika
Air ways tujiandae kwa safari na tukapanga
foleni na kuanza kuingia sehemu maalumu ya
kukaguliwa kisha nikaingia kwenye ndege na
kutafuta sehemu ilipo siti yangu na kukaa baada
ya mida kidogo akingia dada aliye niuliza
kuhusiana na sehemu ya kukaa kisha na yeye
akakaa siti ya pembeni yangu na baada ya muda
safari ikaanza pasipo kusemeshana kitu cha iana
yoyote hadi katikati ya safari ndipo akaanza
kuniongelesha
"Samani kaka unaelekea wapi?"
"Afrika kusini"
"Ahaa mimi ninaitwa Emmy"
"Mimi ni Eddy"
"Ahaa nashukuru kukufahamu"
"Na mimi pia"
"Unakwenda South kufanya nini?"
"Ninakwenda kumcheki bi mkubwa ni mgojwa"
"Ahaa mimi kule ndio ninaishi ila mimi ni
Mtanzania
"Kwa hiyo wewe ni mwenyeji kule"
"Ndio....mama yako amelazwa hospitali gani?"
"Inaitwa Louis Pasteur"
"Ahaa ndipo ninapo fanyia kazi na nidaktari pale"
"Kweli?"
"Ndio ila nilikuwa nipo likizo ndio ninarudi hivi
nilikuja kuwaona wazazi mara moja"
"Eheee asante Mungu nimepata mwenyeji kwa
maana hapa nilikuwa ninajiuliza ni jinsi gani
ninaweza kumpata mama yangu"
Safari ikaendelea kwa masaa kadhaa huku nikiwa
nina amani moyoni mwangu kwani nimempata
mwenyeji wangu.Ndege ikatua kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Maputo.Emmy akaniomba
kwanza niende kwake ili kukipambazuka vizuri
tuweze kwenda hospitali kwani yeye amebakisha
siku tano za kurudi kazini.Tukafika nyumbani
kwake kwenye gorofa refu moja ambalo
alinieleza kuwa watu wangi wamepanga na yeye
sehemu yake ni gorofa ya saba kutoka chini.
"Eddy karibu ndani?"
"Asante"
Emmy akanikaribisha kwenye sehemu anayo ishi
ambayo yenye vitu vingi vya dhamani ya hali ya
juu.Taratibu Emmy akaanza kuvua nguo zake
moja baada ya nyingine na kunifanya nibaki
nikiwa nimemshangaa kwani sikujua ana maana
gani na imekuwaje amevua nguo mbele yangu na
kubakiwa na chupi wakati mimi na yeye hatuna
mahusiano ya namna yoyote
ITAENDELEA