Hotel za kitalii katika mbuga zafungwa hadi mwezi June, wafanyakazi watakiwa kurudi makwao

Vitaboreshwaje wakati hata rambirambi tu wanaiba tena bila aibu
 
The Worlds' Greatest Economic Depression nears...

Tujiandae... Uliye na shamba umelima mahindi..maharage tunza. Chondechonde.
 
Sasa ni wazi waafrika tumejua ni hasara kubwa kiasi gani tunapata kwa kuwacheka wazungu kuwa wanakufa kama kuku na tutajua kuwa zile kauli "ugonjwa wao huo hautuhusu". Tunasahau kuwa aina ya maisha yao na ubunifu wao na pesa zao ndio vinatupa maisha na sisi huku africa.
Leo karibu vyanzo vyetu vyote vya mapato vinakwama. Wao wanapata fidia kubwa kutoka katika serikali zao imara ili kupunguza ugumu wa maisha. Sisi uwezo huo hatuna maana tu masikini wa kipato na serikali yetu haina akiba ya kututosha wote.

Ni MUNGU tu atatusitiri katika hali hii maana vinginevyo mwisho wa janga hili sisi ndio tutakuwa hoi kuliko wao.
 
Na dhani njia pekee ya kuondokana na umasikini sio serikali kuitolea lawama .
Ni mimi, ww na waafrika kwa pamoja kuacha uvivu kufanya kazi tena sana. Tofauti na hvyo tutamtafta sana mchawi kumbe sisi wenyewe ni wachawi.
Tushawaona wanasiasa kma Miungu itakayotuokoa na umasikini, inatuendesha na kutuchezesha akili tumekuwa watumwa wao.
Maisha yangu, kazi yangu, mafanikio yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…