Hotuba ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mbele ya wazee wa Dar Es Salaam, Diamond Jubilee hall 5 Novemba, 1985

Hotuba ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mbele ya wazee wa Dar Es Salaam, Diamond Jubilee hall 5 Novemba, 1985

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HOTUBA YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE MBELE YA WAZEE WA DAR ES SALAAM DIAMOND JUBILEE HALL TAREHE 5 NOVEMBA, 1985

Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam.

Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo.

Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru.

Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru.

Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:

‘’Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo.

Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho.

Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo.

Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.’’

1570285534191.png
 
Nimewahi kusoma mahali ukisema Nyerere kwenye hotuba hii alisema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani wakati wanampokea Nyerere kwenye chama, ni kweli alisema hivyo?!
 
Nimewahi kusoma mahali ukisema Nyerere kwenye hotuba hii alisema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani wakati wanampokea Nyerere kwenye chama, ni kweli alisema hivyo?!
Gagnija,
Msikilize Mwalimu anavyomweleza Abdul Sykes hapi chini:
 
Back
Top Bottom