Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Rais Kikwete ameanza kuhutubia Taifa katika utaratibu wa mwisho wa mwezi. Ameanza kuzungumzia suala la rushwa katika uchaguzi kama alivyozungumzia kule kwenye Mkutano wa TAKUKURU Mwanza.. more to come..
mimi nadhani JK haishi katika muda tunaoishi maana miezi mingine ina mwisho mingine haina!
Hakuna sababu ya kumsikiliza kiongozi aliyeshindwa kuongoza. JK anawalea mafisadi, wahujumu wa uchumi na kila uchwao anakuja na hizi ngonjera zake.
Siku yake itafika wengi wamejaribu lakini historia duniani kote wameshindwa. Aliapa kulinda katiba ya Jamhuri na hivi sasa anachofanya ni kuwalinda wahujumu - Dowans, shirika la reli, BWM, BOT, Shirika la Reli, Shirika la simu kila upande left, right, top and bottom. Hizi ni ngonjera za udanganyifu wa kutaka kupata kura lakini ni fisi aliyevaa ngozi ya kondoo.
Mie nishamchoka huyu baba yani sio kama matarajio ya wengi walidhani atakuwa mkombozi wetu kumbe, tumeruka nanihii ka kukanyaga nanihii🙁
Inamaana hakuna mtu aliyepelekwa mahakamani kwa sababu ya EPA ? BOT ? hakuna watu waliojiuzuru kwa ajili ya Richmond/Dowans ?
Katika mambo yote hujawahi kuona mafanikio ya serikali ya sasa ? Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi sana kiuchumi afrika ya mashariki ukiacha rwanda