Hotuba ya kufunga mwaka.....31 Dec 2010

Hotuba ya kufunga mwaka.....31 Dec 2010

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Kwa wajukuu zangu wapenzi, wadogo zangu, kaka zangu, dada zangu na wadau wote wa JF,

Babu anawatikia heri ya mwaka mpya wa 2011.

Kwa upande wa babu mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa sana ingawa wengi wetu itawachukua miaka mingi kuyaona. Hata nikipumzika kabla ya kuiona 2011, bado nitaenda na amani walau kidogo, kwani nitakuwa nimewaacha wajukuu zangu na ndugu zangu wote Wadanganyika wakiwa tayari wametokwa na nyamulunda waliyokula kwa miaka 49 sasa.

Babu hana zawadi ya kuwapa isipokuwa anawashukuru nyoote kwa michango yenu iliyotufikisha hapa tulipo.

Naomba kuwashirikisha haya maneno ya busara ya ndugu yetu PakaJimmy,

Nia ya msingi ya JF si pahala pa kujifichaficha kama kichuguu cha NGUCHIRO!..Ni mahala pa kusocialize, kubadilishana mawazo, kutoa hoja za kisomi na kitaaluma za kusaidia maendeleo ya nchi na kutoa majawabu ya matatizo mbali mbali ya kijamii.

Ni imani yangu thabiti kabisa kwamba baada ya kile kichotokea 31 Oct 2010, Tanzania hatakaa iwe ile tuliyoizoea. Hata mafisadi wote wanalijua hili.

Nawatakia kila la heri. Mwaka mpya wa 2011 uwe na amani kwenu, mpate furaha na raha ya kutosha.

Babu DC.
 
Taratibu utaelewa tu maneno ya mkuu DC n i mazito sana hayo

swirry upo? Heri ya mwaka mpya ushatoka usalule. Babu 2nashukuru kwa ho2ba yako nzuri hope utavuka mwaka bado hekima zako 2nazihitaji
 
Dark City, poa tu kwa hutuba nzuri na mimi nikipata NAULI basi tukutane huko huko 2011 basi, au vipi???
 
Nashukuru sana babu DC kwa maneno yako ya hekima na mungu akujaalie umri mara mbili ya ulio nao sasa.
 
swirry upo? Heri ya mwaka mpya ushatoka usalule. Babu 2nashukuru kwa ho2ba yako nzuri hope utavuka mwaka bado hekima zako 2nazihitaji

heri na kwako pia sweetie, nimeshatoka kule bana....sasa nipo mitaa ya kati! vipi umesalimika?
 
sijaelewa

Heri ya mwaka mpya Ezen,

Hujaelewa nini ndugu yangu?

Hata hivyo nimeshasema kuwa kuna watu itawachukua muda kung'amua kuwa Tanzania (au soma Tanganyika) ya kabla ya tarehe 31 10 2010 siyo ile ile iliyozaliwa baada ya hapo. May be wewe ni mmoja wao.

Ila kama huamini, basi unaweza kuona mwenyewe jinsi msanii mkuu wa nchi hii alivyoamua kujaribu kuyakimbia mafuriko kwa kudandia treni kwa mbele. Natumai ulimwona jana usiku kwenye luninga!

Labda niseme tu kwamba 31/10/2010 Wadanganyika walitamka pasipo kumng'unya maneno kuwa si mabwege tena. Naamini tutaona mengi kabla ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru!

Babu DC
 
Back
Top Bottom