Pius B. Ngeze
New Member
- May 30, 2011
- 2
- 3
Private Office
P.O. Box 1222, Bukoba, Tanzania
E-mail: ngezep@yahoo.co.uk
Mob: Mob.0784 690277 & 0768 023019
HOTUBA YA KUKUBALI TUNZO (THE SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE AWARD FOR DISTINGUISHED CONTRIBUTION IN ADVANCEMENT OF AGRICULTURE IN TANZANIA FOR THE YEAR 2011/2012)
Shukrani kwa Chuo Kikuu (SUA)
Makala yangu ya kwanza kuchapishwa
Miaka 42 ya uandishi wa vitabu 54 vya kilimo
Baadhi ya vikwazo kwa mapinduzi ya kijani nchini
Mhe. Mkuu wa Chuo,
Hapa nchini, kilimo kitaendelea kuwa tasnia muhimu sana kwa miaka mingi ijayo kama chanzo kikuu cha chakula, mapato na ajira kwa Watanzania zaidi ya milioni 45 waishio mijini na vijijini. Wakati uchumi wa taifa ukiongezeka kwa asilimia 6.5 7.0 kwa mwaka, ongezeko la uzalishaji wa kilimo uko chini sana. Hali iko hivyo licha ya nia njema ya serikali zote tangu tupate Uhuru. Walio wengi tunakumbuka matamshi na kaulimbiu kadhaa za kisiasa, kama vile Siasa ni Kilimo, Kilimo cha Kufa na Kupona na programu kabambe kadhaa kama vile ASDP, MKUKUTA, MKURUBITA, SAGGOT n.k., lakini, zote hazijaleta mapinduzi ya kijani haraka yaliyokusudiwa. Kwa sasa tuna Kilimo Kwanza, yenye lengo lilelile la kuleta mapinduzi ya kijani nchini. Kilimo Kwanza imetambua vikwazo kadhaa vya kilimo nchini na kubainisha nguzo 10 ambazo zikitekelezwa barabara tutashuhudia mapinduzi ya kijani nchini. Pamoja na nia nzuri ya serikali ya kuona uzalishaji wa kilimo nchini ukiongezeka mara kumi na zaidi na jitihada za SUA kuzalisha wahitimu wengi kila mwaka katika fani ya kilimo, naona vikwazo vingine vitano kwa ukuaji wa kilimo chetu. Kikwazo cha kwanza, ni uharibifu wa mazingira na mbadiliko ya tabianchi, mapacha yanayotegemeana. Watu wengi hapa nchini bado hawalioni kuwa tishio kubwa la kutuletea njaa, umaskini, janga na hata vifo. Tembelea mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara, kama mfano, ushuhudie athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi kwenye kilimo. Barafu kwenye mlima Kilimanjaro inatoweka haraka na wakulima wadogo wa mikoa hiyo wanashuhudia athari mbaya sana kwenye kilimo chao ambazo hawajawahi kuziona maishani mwao. Mito ambayo huko nyuma haikuwahi kukauka, sasa inakauka. Katika baadhi ya wilaya za mikoa hiyo, kama vile Monduli, mvua hukosekana hata kwa miaka miwili mfululizo na maziwa, kama vile Ziwa Manyara, yanaendelea kukauka. Hali iko hivyo hivyo katika mikoa mingine mingi nchini, na hata iliyosalia inanyemelewa. Natoa mwito kwa serikali, taasisi na asasi mbalimbali kuongeza kasi katika kuwaelimisha wananchi juu ya suala hili na kuchukua hatua za kupunguza athari na kukabiliana na hali hiyo.Kikwazo cha pili, ni wahitimu wa kozi za kilimo nchini kutokuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu vyenye elimu ya kilimo bora. Maofisa hawa ni wahitimu wa Vyuo Vikuu, SUA ikiwamo, na Vyuo vya kilimo nchini. Kutosoma vitabu ni kansa kwa Watanzania walio wengi sana. Hatimaye taifa ambalo wananchi wake hawana utamaduni wa kusoma litakuwa taifa la wajinga na mwisho wake siyo mzuri. Mwito wangu kwa Vyuo Vikuu vyote (SUA ikiwamo), vyuo vya aina mbalimbali, shule za sekondari na shule za msingi, ni kuwa lazima mkazanie kuanzisha "somo la kupenda kujisomea ili wahitimu wenu wathamini kusoma, muwajengee mazoea na utamaduni wa kujisomea, maana elimu kubwa na inayokwenda na wakati hupatikana nje ya vipindi vya kuwa vyuoni na shuleni. Kuthibitisha rai hii, pamoja na kuzitumia orodha ya vitabu vya kilimo tulivyonavyo Halmashauri, kati Halmashauri za Miji/Manispaa/Majiji 156 ni 22 tu ambazo zimewahi kuagiza vitabu vya kilimo kwa ajili ya Vituo vya Elimu vya Kata, maofisa ugani, viongozi wao na wakulima. Je, hizo zilizobaki hazina maofisa wa kilimo ambao wanatambua umuhimu wa vitabu hivyo kama nyenzo ya kufanikisha Kilimo Kwanza katika maeneo yao? Aidha, tusisahau kuwa nchi hii ina watu wengi vijijini na mijini ambao wanajua kusoma na kuandika, na hivi sasa kila mwaka maelfu ya wahitimu wa shule za sekondari na shule za msingi hubaki vijijini na mijini bila ajira tofauti na kilimo au wasioendelea na elimu ya juu. Hawa wangekuwa na utamaduni wa kusoma vitabu vya kilimo na wakavipata, wangevutiwa kuanzisha kilimo, hivyo, kuchangia mapinduzi ya kijani nchini. Kikwazo cha nne, ni uwezo mdogo wa kifedha wa wakulima wetu, maofisa watendaji wa vijiji na kata, viongozi wao na hata maofisa ugani wa kununua vitabu vya kilimo. Hata kama wengependa kuvisoma, hawawezi kuvinunua! Natoa mwito kwa serikali, taasisi na asasi mbalimbali kubuni miradi itakayowawezesha kupata na kusambaza vitabu hivyo kwa wakulima, Vituo vya Elimu vya Kata na Maktaba za Vijiji/Kata kwa kupitia Halmashauri zao za Wilaya/Miji/Majiji. Kwa hakika, haina maana wala faida yoyote kuwapo nchini vitabu vya kilimo, lakini, walengwa haviwafikii ili wafaidike navyo. Kikwazo cha tano, ni serikali kutosaidia tasnia ya uchapishaji nchini. Miaka minne hadi sita iliyopita, hadi sasa, imeshuhudia kudorora kwa uchapishaji na biashara ya vitabu nchini. Hii ni kwa sababu soko kubwa la vitabu ni serikali. Isiponunua vitabu vya kupelekwa mashuleni, vyuoni, vijijini na taasisi nyingine, kama ilivyotokea katika kipindi hicho, matokeo yake ni wachapishaji kukwama na kujiondoa katika biashara hiyo. Inapokuwa hivyo na maduka mengi ya vitabu nchini hufungwa, na ndivyo imetokea. Hali hii ni tofauti na ilivyo katika nchi nyingine za Jumuia ya Afrika Mashariki, Jumuia ya SADC n.k. Hatari inayotukabiri Watanzania na taifa, ni kuwa tunaelekea kuwa soko la vitabu kutoka nchi jirani ambavyo viliandaliwa maalumu kwa ajili ya watu wao na si Watanzania! Natoa mwito kwa serikali kukabili haraka hali hii na kuokoa tasnia ya uchapishaji nchini. Tusipofanya hivyo, taifa litaangamia kielimu.
Huduma za Ugani katika kufanikisha Kilimo Kwanza
Mwito kwa wasomi nchini kuandika vitabu
Pius B.NgezeMTUNUKIWA TUNZO
Hotuba hii imetolewa tarehe 23 Novemba, 2012 SUA Morogoro, Tanzania