Hotuba ya Mobhare Matinyi katika Hafla ya Kitaifa ya MISA Tanzania ya Tafakuri ya Uchechemuzi wa Uhuru wa Kujieleza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Hotuba ya Mkurugenzi Wa Idara Ya Habari Na Msemaji Mkuu Wa Serikali Ya Jamuhuri Ya Muungano Tanzania, Mobhare Matinyi, Kwenye Hafla Ya Pili Kitaifa Ya Tafakuri Ya Uchechemuzi Wa Uhuru Wa Kujieleza Iliyoandaliwa na Misa- Tanzania, kwenye Hoteli Kilimanjaro Hyatt, Dar es Salaam, Tarehe 31 Mei, 2024

Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema uzima na kutuwezesha kushiriki tukio hili muhimu na kubwa katika historia ya nchi yetu la tathmini ya uchechemuzi wa uhuru wa kujieleza chini ya MISA Tanzania.

Pongezi kwa MISA-Tanzania kwa kuandaa tukio la leo. Siku hii ni maalum na ya kihistoria kwa kuwakutanisha wadau wa sekta husika ili kutathmini namna

wanavyoweza kuendesha shughuli za kichechemuzi hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na baadaye uchaguzi mkuu mwakani; hivyo kusaidia kuongeza hamasa kwa wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki kikamilifu katika chaguzi hizi kwa kuzingatia sheria za Tanzania. Nawapongeza washiirki wote kwa kuwa sehemu muhimu ya historia hii.

Ninatambua pia uwepo kwa wakongwe wa MISA Tanzania na tasnia kwa ujumla, na wageni wetu maalum kutoka balozi za Marekani na Uingereza; na naomba nizungumze kwa lugha ya Kiingereza ili kuwafikia ujumbe.


Your Excellency, the Ambassador of the United States to Tanzania, Dr. Michael Battle and the Representative of the British High Commission and representatives of international organizations, here present.

Let me first and foremost express our gratitude as the Government of the United republic of Tanzania, for your sincere dedication and support to our efforts in ensuring our country attains its goals in promoting the freedom of expression and the press freedom in our growing democracy.

The current administration under Her Excellency President Samia Suluhu Hassan, has demonstrated its political will to support this freedom, which is enshrined in our constitution, and as you know the moment she assumed power she ordered the government to restore the registration of four papers that had been closed down by the government. Why did she do so? She wanted her government to support media freedom in the country through actions, guide the sector and not muzzle it.

The President also ordered the amendment of the Media Service Act, which happened last year as well as the regulations of the Electronic and Postal Communication Act, in order to support media freedom in the country.

The President also directed the Minister responsible for the sector to establish a special committee to look into the economic challenges facing the media sector in Tanzania, a global challenge caused by the development of technology, so that the government may address those challenge to enable the media sector to function comfortably and succeed.

It is no wonder that Tanzania is now the highest ranked country in the east and central African region according to report issued by the Reporters Without Borders, just this April – the World Press Freedom Index.
AfroBarometer has also ranked Tanzania first among 39 surveyed countries in Africa in terms of freedom of expression.


We therefore, once again, express our appreciation and welcome your support in making sure that our progress in that endeavour and remain respectful of the media freedom while emphasizing ethical and responsible practice.

Thank you very much.



Naomba sasa niwape salamu kutoka kwa viongozi wetu wakuu wa nchi yetu:

Mhe. Rais wa JMT – Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yuko ziarani nchini Korea Kusini ambapo inatarajiwa kwamba, mbali na masuala mengine ya maslahi ya nchi hizi mbili, atajadiliana na wenyeji wake kuhusiana na ushirikiano katika sekta ya habari baina ya nchi zetu mbili hizi. Huu ni ushahidi mwingine kwamba Mhe. Rais anajali maendeleo ya sekta ya habari nchini.

Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, naye anatuma salamu za heri akiwatakia majadiliano mema kuhusu mustakabali wa nchi katika eneo la uhuru wa kujieleza na kupashana habari.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, juzi tarehe 21 Mei tulikuwa naye pale UDSM kwenye tukio la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ambapo aliwashukuru kwa juhudi zao za kuhabarisha wananchi kwa manufaa ya maendeleo ya nchi yetu na akaitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoa mafunzo kwa wanahabari hawa ili wafanye kazi zao vizuri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu. Mhe. Waziri Mkuu anawasalimu sana.

Mhe. Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, ambaye tarehe 29 Aprili tulikuwa naye Dodoma kwenye tukio la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), na ambaye pia kama si kubanwa na ratiba zingine za kitaifa, huko Ifaraka hivi leo, basi angekuwa nasi hapa leo. Mhe. NWM anawasalimu sana na anaipongeza MISA-Tan kwa kufikisha miaka 30.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Moses Nape Nnauye, ambaye hivi leo yupo na Mhe. Rais nchini Korea Kusini, naye pia anawatakia heri wadau wote katika kuhakikisha kwamba sekta ya habari nchini inakua na kufikia malengo ya taifa letu ya kuwa na weledi, uhuru na uwajibikaji katika suala zima la habari kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.

Mhe. Naibu Waziri wetu, Mhandisi Maryprisca Mahundi, yeye yuko bungeni akijibu maswali lakini pia anatuma salamu kwenu.

Naomba sasa niipongeze MISA Tanzania kwa kufikisha umri wa miaka 30 na zaidi pia kwa kuwa moja ya taasisi za habari kongwe nchini ambazo zimetoa mchango mkubwa kwenye ustawi wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa.

Ndugu Washiriki,​

Naomba nitumie fursa pia kuwapongeza wanahabari wakongwe nchini ambao wameipa heshima nchi yetu katika siku za karibuni.

Kwanza, ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ndg. Ernest Sungura, ambaye tarehe 16 Mei, 2024, jijini Cape Town, Afrika Kusini, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA).

Itakumbukwa pia mwezi Oktoba tukiwa Arusha kwenye HQ ya EAC tulizindua Baraza la Vyombo vya Habari Afrika Mashariki (EAPC), ambapo Mtanzania, Katibu Mtendaji wa zamani wa MCT, Kajubi Mukajanga, ndiye aliyechaguliwa kuliongoza katika kipindi hiki.

Lakini pia tarehe 18 Mei, 2024, jijini Accra, Ghana, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Ndg. Deodatuts Balile, alichaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Mashariki mwa Afrika (EAES), kwa mwaka 2024/25.

Ukiondoa wenzetu hawa ambao sasa watakuwa vinara kimataifa, juzi tarehe 29 Mei, huko Copenhagen, Denmark, mwanamama mwandishi mkongwe nchini, Beatrice Bandawe, Mhariri Mtendaji wa gazeti la NIPASHE, naye pia alikabidhiwa Tuzo ya Mwanamke Kiongozi katika Chombo cha Habari iliyotolewa na Umoja wa Wachapishaji wa Magazeti Duniani (WAN-IFRA). Hii ni mara ya kwanza kwa tuzo hii kuja Tanzania.

Haya ni mafanikio ambayo sisi Watanzania hatuwezi kuyachukulia kwa urahisi tu – kwani yanadhihirisha maendeleo katika sekta yetu ya habari na kuthibitisha kwamba juhudi za serikali ya Mhe. Rais zinazaa matunda kwa namna mbalimbali, achilia mbali uhuru wa kukutana kama hivi na kujadiliana kwa uhuru.

Kwa hakika Serikali inatambua kazi muhimu inayofanywa na tasnia ya habari nchini katika kuhabarisha umma, na hivyo inaheshimu na kutambua kazi nzuri ya taasisi mbalimbali za sekta hii kama MISA TANZANIA na ndio sababu ya msingi ya mimi kuja kujumuika nanyi leo.

Aidha, nawapongeza wanahabari wote nchi kwa kuendelea kuhabarisha umma hasa kwa kueleza sera na kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania.

Sekta hii inakua kwa kasi kubwa; hivyo umakini na uhakiki wa taarifa ni muhimu ili kulinda maadili ya sekta na jamii ya Watanzania kwa ujumla. Uchechemuzi wa uhuru wa kujieleza lazima uzingatie maadili, miongozo na desturi za Mtanzania kwa kulinda utu na utaifa.

Makamu Mwenyekiti wa MISA TANZANIA​

Kwa kutambua sekta ya habari ni sekta inayokuwa kwa kasi nchini - Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza kuchukuliwa hatua mbalimbali ikiwamo kufunguliwa kwa magazeti yaliyofungwa kwa muda mrefu, kupitia sera ya habari na utangazaji ya mwaka 2003 ili iendane na wakati na mabadiliko ya teknolojia nchini.

Pia Mheshimiwa Rais Samia alituagiza kufanya marekebisho ya Sheria ya Habari ya mwaka 2016, ambayo tumewashirikisha wadau mkiwamo MISA Tanzania katika mchakato wote wa kupitia vifungu vyote na kukubaliana kwenye maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho,.

Aidha, mwaka huu Tanzania imekuwa kinara kinara wa kuheshimu uhuru wa habari Afrika Mashariki na haya yote ni matunda ya masikilizano na majadiliano kati ya serikali yetu sikivu na raia wake.

Tanzania imeshika nafasi ya 97 kutoka nafasi ya 143 mwaka (2022/2023) kidunia na nafasi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa mafanikio ya kulinda uhuru wa vyombo vya habari. Taarifa hii ni kwa mujibu wa "World Freedom Report" ya mwaka 2023/2024 iliyotolewa na taasisi ya Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF). Nchi yetu imepiga hatua 46 mbele ndani ya mwaka mmoja.

Vilevile, kwa mujibu wa taarifa nyingine iliyotolewa Aprili 2024 na taasisi ya Afrobarometer inayopima namna watu wanavyojisikia kuwa huru kuhisiana na taarifa, Tanzania inashika nafasi ya kwanza miongoni mwa nchi 39 za bara la Afrika. Mafanikio haya katika taarifa hizi mbili ni hatua muhimu ya kujivunia na inapaswa kupongezwa na kila mdau wa habari hapa nchini.

Ni hakika kwamba, na kwa mafanikio haya, serikali yetu ina nia thabiti na inatekeleza kwa vitendo matakwa ya jamii yake ikiwemo kuongeza uhuru wa watu kutoa na kupata taarifa hali ambayo imeongeza uwajibikaji na kukuza uhuru wa kujieleza.

Mwenyekiti wa MISA TANZANIA​

Ninatambua kuwa MISA Tanzania, imekuwa na safari ndefu yenye mengi ya kujifunza, lakini mchango wake mkubwa kwenye ustawi wa tasnia na nchi yetu kwa ujumla hauwezi kuacha kukumbukwa.

Leo mnapoongoza gurudumu la tathmini ya uchechemuzi juu ya uhuru wa kujieleza, ni rai yangu mzingatie misingi ile ile iliyosababisha mabadiliko chanya katika uhuru wa habari na kuelimisha na siyo wanahabari tu bali wananchi kwa ujumla ikiwemo taasisi za maendeleo juu ya uhuru wa kujieleza wenye kujenga na kuheshimu mipaka ya kikatiba.

Pia mchango wa MISA Tanzania kwenye kuwapatia mafunzo ya ndani na nje ya nchi waandishi wa habari, hali ili waongeze uwezo wa kutekeleza majukumu yao na kuwa na uzoefu wa nchi nyingine ni muhimu sana na ninaupongeza..

Aidha, serikali imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa wanahabari na wadau wa maendeleo nchini na ndio maana kumekuwa na ongezeko la taasisi za kijamii, wadau wa maendeleo nchini pia vyombo vya habari na wanahabari ambao wanachangia pato la taifa kupitia ajira mbalimbali.

Mwenyekiti wa MISA Tanzania​

Sekta ya habari imeendelea kukua kwa idadi ya vyombo vya habari na vimeongezeka, vyote, televisheni, redio, magazeti na vyombo vya mitandaoni ambapo sasa vilivyoandikshwa ni zaidi ya 700. Haya ni maendeleo ya uhuru wa habari. Hizi zote ni jitihada za Rais Samia kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi kwenye mazingira mazuri, ndio maana kwenye kikao kazi cha Mawaziri alielekeza maofisa habari kutangaza taarifa za serikali ili umma wa Watanzania ufahamu mambo makubwa yanayofanywa ikiwamo miradi ya kimkakati.

Aidha, serikali inatambua hali ngumu ya waandishi mmoja mmoja na vyombo vya habari nchini, ndiyo maana imeunda kamati ya kuangalia hali ya uchumi wa vyombo vya habari ambayo inaendelea na kazi, tunatarajia itakuja na taarifa ya kina ambayo itasaidia kuboresha tasnia ya habari nchini.

Washiriki.
Serikali inawahikishia ushirikiano na mazingira mazuri ya kazi, na tunawakumbusha kutekeleza majukumu yenu ya kutumikia na kuhabarisha umma kwa kuzingatia maadili, weledi na sheria za nchi huku mkitanguliza uzalendo mbele kwa kueleza mazuri ya nchi siku zote hasa miradi ya kimkakati ambayo italeta mabadiliko makubwa kwenye nchini mwetu.

Baada ya kusema hayo natamka kufungua rasmi mkutano huu na kuwatakia majadiliano mema kwa mustakabli wa nchi yetu.
 
Hafla ya Pili Kitaifa ya Tafakuri ya Uchechemuzi wa Uhuru wa Kujielezea iliyoandaliwa na MISA - Tanzania

Ushirikiano wa Serikali
Serikali inawahikishia ushirikiano na mazingira mazuri ya kazi, na tunawakumbusha kutekeleza majukumu yenu ya kutumikia na kuhabarisha umma kwa kuzingatia maadili, weledi na sheria za nchi huku mkitanguliza uzalendo mbele kwa kueleza mazuri ya nchi siku zote hasa miradi ya kimkakati ambayo italeta mabadiliko makubwa nchini mwetu.

Ukuaji wa Sekta ya Habari
Sekta ya habari imeendelea kukua kwa idadi ya vyombo vya habari na vimeongezeka, vyote, televisheni, redio, magazeti na vyombo vya mitandaoni ambapo sasa vilivyoandikshwa ni zaidi ya 700. Haya ni maendeleo ya uhuru wa habari. Hizi zote ni jitihada za Rais Samia kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi kwenye mazingira mazuri.

Tanzania yapaa katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari
Tanzania imeshika nafasi ya 97 kutoka nafasi ya 143 mwaka 2022/2023) kidunia na nafasi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa mafanikio ya kulinda uhuru wa vyombo vya habari. Taarifa hii ni kwa mujibu wa "World Freedom Report" ya mwaka 2023/2024 iliyotolewa na taasisi ya Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF). Nchi yetu imepiga hatua 46 mbele ndani ya mwaka mmoja.

Haya ni mafanikio ambayo sisi Watanzania hatuwezi kuyachukulia kwa urahisi tu kwani yanadhihirisha maendeleo katika sekta yetu ya habari na kuthibitisha kwamba juhudi za Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zinazaa matunda kwa namna mbalimbali, achilia mbali uhuru wa kukutana kama hivi na kujadiliana kwa uhuru.

Wanahabari wa Tanzania katika anga za kimataifa
Ukiondoa wenzetu hawa ambao sasa watakuwa vinara kimataifa, juzi tarehe 29 Mei, huko Copenhagen, Denmark, mwanamama mwandishi mkongwe nchini, Beatrice Bandawe, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, naye pia alikabidhiwa Tuzo ya Mwanamke Kiongozi katika Chombo cha Habari iliyotolewa na Umoja wa Wachapishaji wa Magazeti Duniani (WAN-IFRA). Hii ni mara ya kwanza kwa tuzo hii kuja.

Pili, itakumbukwa mwezi Oktoba tukiwa Arusha kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tulizindua Baraza la Vyombo vya Habari Afrika Mashariki (EAPC), ambapo Mtanzania, Katibu Mtendaji wa zamani wa MCT, Kajubi Mukajanga, ndiye aliyechaguliwa kuliongoza katika kipindi hiki.

Naomba nitumie fursa pia kuwapongeza wanahabari wakongwe nchini ambao wameipa heshima nchi yetu katika siku za karibuni. Kwanza, ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ndg. Ernest Sungura, ambaye tarehe 16 Mei, 2024, jijini Cape Town, Afrika Kusini, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA).

Lakini pia tarehe 18 Mei, 2024, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Ndg. Deodatus Balile, alichaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Mashariki mwa Afrika (EAES), kwa mwaka 2024/25.

Salamu kwa wanahabari
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Moses Nape Nnauye, ambaye hivi leo yupo na Mhe. Rais nchini Korea Kusini, naye pia anawatakia heri wadau wote katika kuhakikisha kwamba sekta ya habari nchini inakua na kufikia malengo ya taifa letu ya kuwa na weledi, uhuru na uwajibikaji katika suala zima la habari kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.

Mhe. Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, ambaye tarehe 29 April tulikuwa naye Dodoma kwenye tukio la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), na ambaye pia kama si kubanwa na ratiba zingine za kitaifa, huko Ifaraka hivi leo, basi angekuwa nasi hapa leo.

Mhe. Naibu Waziri Mkuu anawasalimu na anaipongeza MISA Tanzania kwa kufikisha miaka 30. Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, naye anatuma salamu za heri akiwatakia majadiliano mema kuhusu mustakabali wa nchi katika eneo la uhuru wa kujieleza na kupashana habari.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, juzi tarehe 21 Mei tulikuwa naye pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye tukio la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ambapo aliwashukuru kwa juhudi zao za kuhabarisha wananchi kwa manufaa ya maendeleo ya nchi yetu na akaitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoa mafunzo kwa wanahabari hawa ili wafanye kazi zao vizuri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu. Mhe.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko ziarani nchini Korea Kusini ambapo inatarajiwa kwamba, mbali na masuala mengine ya maslahi ya nchi hizi mbili, atajadiliana na wenyeji wake kuhusiana na ushirikiano katika sekta ya habari baina ya nchi zetu mbili hizi. Huu ni ushahidi mwingine kwamba Mhe. Rais anajali maendeleo ya sekta ya habari nchini.

Pongezi kwa MISA Tanzania kwa kuandaa tukio la leo. Siku hii ni maalum na ya kihistoria kwa kuwakutanisha wadau wa sekta husika ili kutathmini namna wanavyoweza kuendesha shughuli za kichechemuzi hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na baadaye uchaguzi mkuu mwakani; hivyo kusaidia kuongeza hamasa kwa wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki kikamilifu katika chaguzi hizi kwa kuzingatia sheria za Tanzania. Nawapongeza washiirki wote kwa kuwa sehemu muhimu ya historia hii.
 
Watanzania watakula uhuru wa habari?

Ndiyo maana hamna hata flyover mpya iliyojengwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…