Hotuba ya mwisho aliyoindika Muammar Gaddafi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
QADDAFI.jpg
KANALI QADDAFI.jpg

HOTUBA YA MWISHO ALIYOIANDIKA QADAFFI

QADAFFI ANAANZA HIVI:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema..
..

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
 
Nimeisoma nikafurahi mno. Hili liwe fundisho kwa wanaotamani kumuiga kuwa Miafrika ndivyo tulivyo (In Nyani ngabu's voice). Hata uwape wali kwa panzi. Hawana jema kwao. Full Stop.
Nnani kakuambia kuwa tunahitaji hayo makitu chini ya ukandamizi?
 
Kosa lake kubwa ni kujiona yeye ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa libya pekee

Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakulijua au alilijua akalipuuzia

Ni bora angeachia madaraka akamwachia mwingine, ungekuta mpaka Leo anadunda tu.
 
Naanza kuamini kuwa lengo la NATO halikuwa kumuondoa gadaf na kuweka mfumo nzuri wa democrasia, naamini walibya wanajuta bali lebgo lilikua kutafuta na kutafuna raslimali za Libya. Hakuna afya bure, elimu bure wala raia kupewa pesa ya kujikimu kwa wale wasiokuwa na kazi. Walitaka uhuru zaidi kumbe wamepata vita zaidi, umwagaji wa damu usioisha, nchi imekuwa chaka na chochoro za kupitia wakimbizi kwenda ng'ambo. Ni fujo tupu. Kila mtu anataka uongozi. Na kwa hali hii kitafika kiama hii nchi haitulii. Tutegemee iwe somalia ya kaskazni. Kwangu, ni bora ya gadafi kuliko madhila ya sasa.
 
Kosa lake kubwa ni kujiona yeye ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa libya pekee

Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakulijua au alilijua akalipuuzia

Ni bora angeachia madaraka akamwachia mwingine, ungekuta mpaka Leo anadunda tu.
Hebu tumia akili kidogo. Hivi hata ingekuwa ni wewe unapata vitu vyoye hivyp kutoka kwa kiongozi aliyepo madarakani ungetamani aondoke?
 
Kosa lake kubwa ni kujiona yeye ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa libya pekee

Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakulijua au alilijua akalipuuzia

Ni bora angeachia madaraka akamwachia mwingine, ungekuta mpaka Leo anadunda tu.
Sasa hayupo hao walibya wanapata nini? Mbona hawaweki kiongozi mwingine wakaendelea na maisha
 
Kosa lake kubwa ni kujiona yeye ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa libya pekee

Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakulijua au alilijua akalipuuzia

Ni bora angeachia madaraka akamwachia mwingine, ungekuta mpaka Leo anadunda tu.
madikteta wengi wanaoleta maendeleo huwa wanalazimika kubaki madarakani kwa sababu mbili
1.wakitazama jinsi walivo hustle toka ujana hadi uzeeni kuleta maendeleo wanaona kabisa hakuna mrithi wa kuendeleza mazuri yao

2.wakitazama mambo mabaya waliyoyafanya katika juhudi za kuleta maendeleo na amani kwa watu wao wanaogopa maadui waliojitengenezea watawamaliza
 
Dah!!inasikitisha sana aisee..
Na wale wahanga wa ndege (zaidi ya 250) ktk anga la Lockerbie mbona huwaonei huruma. Roho zisizo kuwa na hatia ziliteketezwa kupitia mkono wa huyu Gaddafi.
Unajua alichowafanyia wanafunzi wa University mnamo 1976? Na Wakurdi je?
Gaddafi squad special kwa kunyonga watu ulishawahi kuisikia?
Kwanini usiwasikitikie Watz wenzako waliokufa 1978/79 kupitia kwa huyu Gaddafi pale alipomsaidia Nduli Iddi Amini kuipinga Tz?
 
View attachment 1123851View attachment 1123850

HOTUBA YA MWISHO ALIYOIANDIKA QADAFFI

QADAFFI ANAANZA HIVI:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema..
..

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
This does not change the reality that he was a good dictator; but, what good is money and security when no one is free?
Gaddafi alikuwa juu ya sheria; hakuna yeyote ktk Libya aliyethubutu kutenda lolote bila kibali kutoka kwa Jiwe Gaddafi. Walibya waliishi kama mashetani.
 
Sasa wanaishi kama nani?
 
Back
Top Bottom