Hotuba ya Rais Magufuli yawa "Lulu" duniani kote, Wachina na Wahindi wataka itafsiriwe kwa lugha za mataifa yao

Lengo la wao kutaka itafsiriwe kwenye lugha yao ni kwasababu wameikubali hio hotuba?

Na kama wameikubali kuwa ni nzuri inamaana wameielewa.

Huenda kuna kitu wanataka kusikiliza tu ambacho mimi na wewe hatujui n nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichoona mimi kwamba ile hotuba imekuwa kichekesho maana vyombo vingi vimeikejeli....Hata wataalamu wabobezi wamesema kabisa kifaa ambacho kimekuwa calibated kupima covid19 kwa sample ya binadamu hakiwezi kutoa jibu sahihi kwa viumbe au non-living things vingine lazima litatoa jibu lisiloeleweka na ndio maana ukaona oil ina corona19.
 
The end always justifies the means. Ukishaona mwandishi ni nani inatosha kabisa kukufanya uitupe post kwenye dustbin kwani ni takataka tu.
 
Amekuwa kituko duniani kote kweli ni aibu huku ughaibuni tunadharauliwa.

Umejuaje kama tunadharauliwa?! Na mbona unajali?! Na umejuaje kama Rais hayuko sahihi?! Huenda anawachallenge mabeberu ndo maana yanampaka matope na kumfanya aonekane kituo. Yanatumia wananchi wa nchi yake kumu attack Rais. Lait ungejua jinsi mabeberu yanavyotenda kazi na nia yao hata usingejali yanafikiria nini ila ungetumia akili yako kufikiria kila anachokitenda mkuu. Usitumie media au akili ya mwingine kujudge.
 
Nyie ndio wafia-magu. Poleni sana kwa kazi ngumu. Madagascar ndio wametangaza jana kwamba ile dawa ya corona wanaanza kuifanyia utafiti wa kitaalam manake ilikuwa inatumika kienyeji tu kama vile mwarobaini hako kwetu. Lakini kiongozi tuliyenaye tayari alishasema atatuma ndege kuchukua dawa! Unawanyweshaje watoto wako dawa isiyothibitishwa? Unawepanda kweli?

Ishu nyingine ya aibu kubwa ni kupeleka sample za maembe, mbuzi na mapapai kupima corona. Wanaojua sayansi ya maabara ni kwamba vipimo hivi ni very specific. Huwezi kupeleka sample ya oil chafu ya magari eti kucheki ubora wa vipimo, au hata sample ya mafenesi. Wangepaswa kuchukua sample ya binadamu kwani vipimo hivi havipimi kila sample kuna specificity. Tunachekwa sana duniani.
 

Mi nipo neutral. I don't judge. Sijui nani yupo sahihi kati ya Magu na wapinzani wake.
 
Kwa kisukuma huwa tunaita " sarcasm "
 
Mi nipo neutral. I don't judge. Sijui nani yupo sahihi kati ya Magu na wapinzani wake.
Ufunuo 3:15-16
"Nayajua matendo yako yakuwa hu baridi wala hu moto ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvungu, wala hu baridi wala moto nitakutapika utoke katika kinywa changu."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupata vichekesho kama hvyo tunabonyeza ngapi mkuu..?
 
Unataka wafe mara ngapi?
 
Kwani Magufuli alisema mapapai yake yamepimwa kwa vifaa alivyopewa msaada au alivyonunua kwa pesa za walipa Kodi wa Tanzania
 
Ufunuo 3:15-16
"Nayajua matendo yako yakuwa hu baridi wala hu moto ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvungu, wala hu baridi wala moto nitakutapika utoke katika kinywa changu."

Sent using Jamii Forums mobile app

I'm not sorry- siamini katika biblia- sio muongozo katika imani yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…