Chambusiso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 2,592
- 4,640
Siku nyingi sana najaribu kutafuta hotuba za mwalimu zile zilizokuwa zinatolewa kwenye ujumbe wa leo RTD enzi zake kwenye media yoyote Audio CD, cassetes, DVD etc. Ninapenda sana kusikiliza hizi record na kupata ujumbe lakini zinazopatikana ni chache na ni vipande vidogo vidogo. Najua wappo wengi wanaopenda zipatikane kwa njia yoyote kwa wananchi na watu tunaomuona kama mkombozi wa Tanzania tupate ule ujumbe na falsafa zake. Siku zote falsafa za kiongozi zinapatikana vizuri zaidi unaporudia kuzisikia na kuzisoma kazi zake mbalimbali.
Najua katika Tanzania ya leo ya mafisadi hakuna mwenye ujasiri wa kusikiliza ndani ya serikali na ni mwiba mkali kwa viongozi waliopo kusikiliza, nategemea wao ndio source kubwa ya kufanya zifichwe
Iwe ni familia yake, TBC, Serikali, Tasisi ya Mwalimu yoyote anayehusika hebu toeni kazi za mwalimu tutazinunua!! Waache ubinafsi wa kizificha tunataka elimu iliyopo tuichote na kuitumia. Watanzania tusipoangalia historia ya huyu mtu muhimu kwa nchi yetu ndio inazikwa hivyo jamani, kwa maslahi ya ubinafsi. Watawala hawataki kabisa kuona watu wanasikiliza ujumbe huu.
Ingewezekana kuelekea uchaguzi mkuu zipatikane in public kwa wingi najua watu watapata hekima iliyopo. Hebu kumbuka aliposema CCM si mama yangu! Watu wakipata ujumbe kama huu atakapokuja Makamba kusema CCM ni ya Nyerere, watu watakuwa na kitu cha kukumbuka mwenyewe alisemaje. Hebu kanzi katusaidie vyovyote
Nawakilisha