Lizy ukirudi mbili usiku uko nyeng'e bin nyeng'e unataka uoge, ule na ukalale au uangalie vipindi vyako kwenye TV labda mpaka saa tano ya usiku. Njemba, ikikugusa...inaambiwa not tonight sweetie, I am very tired. Hii inakuwa order of the day Monday to Friday, kama ndio unafanya biashara/kazi na weekend mambo ndiyo yanakuwa mazito zaidi. Njemba inatafuta nyumba ndogo na kwenda kupumzika huko. Nakumbuka mwanaJF mmoja aliwahi kulalama kuhusu maisha kama haya, na akasema anachat sana na wanawake mbali mbali kwenye mtandao maana mamsap hana muda naye ama kachoka au anaangalia 'vipindi vyake' alivyorekodi. Mnaendelea hivi kwa muda, halafu mnakuja kugundua kwamba pamoja na kuwa mnaishi nyumba moja lakini mnaishi separate lives kila mtu kivyake vyake, na mara nyingi mkija kugundua it is too late!!.
Hmmmm! Maisha ya ndoa tangu zamani yalikuwa magumu, lakini sasa hivi ugumu umeongezwa zaidi na vitu kama TV, internet n.k.