housegirl ni Mke mwenzio!!!!!!!!


kuwa na HG ni sawa je unataka afanye kila kitu huku wewe wanyoosha miguu kuangalia TV na kusoma magazeti hata huyo hg anatakiwa kupata maelekezo kwako we mama na wakati mwingine kufanya. Ninachopingana nacho ni kwa wale baadhi ya wanawake kupenda kufanyiwa kila kitu
 
Last edited by a moderator:
Blaki Womani
Tunapaswa pia kukubaliana kuhusu shughuli anazopaswa kufanya mwanaume!

Sasa hivi kuna cutural shock, kiasi kwamba kwenye baadhi ya mambo mnakimbilia kwenye asili, kwa mengine mnaukubali ukisasa.

Angalia mfano wa typical life ya working mother n wife ambaye hana HG na hiyo miday care anayosema NN haipo. Jibu utapata mwenyewe!

Tuchagua, au tuwe 100% house wives au kama tunafanya kazi na hatutaki helper then tugawane majukumu ya nyumbani! Ili huyo mwanaume asi'muhurumie' HG kwa kumuongezea majukumu ya kutimiza tamaa zake za ngono!
 
Last edited by a moderator:

Kwahiyo na ofisini/kiwandani/salon/dukani huyo HG anakuja kunifanyia kazi?
Nikiweka 3 ili wapate muda wa kupumzika nitakuwa nimekosea?
 
Mwanaume ambae haijui thamani ya mke wake na ambae hajui kutofautisha kati ya mke na housegirl hafai kuwa kiongozi wa famili na pengine hatakiwi awe na familia!
 

Alaaniwe anayeikurubia zinaa
 
Unabii kampa nani, dini ninayoamini hiyo kitu haipo kabisa. Kuzini dhambi period!
 
Mimi huyu Nabii Tito huyu namchukuliaga anafit kwenye ile..wengi watakuja kwa jina langu, jihadharini
 

:thinking::A S confused:
 
Sioni ubaya wa mtu kuwa na housegirl na wala si kitu cha kuona aibu kufanya as long as unamlipa inavyostaili na kutomyanyasa. Nyie wenyewe mnajua ajira serikali imeshindwa kuzitengeneza; kuna ubaya gani kwa mtanzania kuajili msichana wa kazi? Mimi nawajua ma house ambao wamewajengea wazazi wao nyumba. Na kuna swala la specialization; kama muda wako unaweza kuutumia kufanya kinachokuingizia zaidi why not leave hosework to somewone else who can do it efficiently.

Ndio maana hata wanaharakati wa haki za binadamu hawapingi kuwa na watumishi wa majumbani (wakijua ni msaada kwa hao mabinti) wanapinga terms zao za employment.

Kwa hiyo wewe uliyeajiri h/girl be proud kuwa ume create ajira (kama unamlipa vizuri msichana wako)
 
haya sasa makubwa ndugu ndo mwisho wa dunia huu ni nabii wa uongo wale wlioandikwa ktk bible kitabu cha mwisho kabisa ufunuo wa yohana
 
dah huyo nabii ni noma kwa kweli.bt sometimes wanawake 2najiendekeza,kuna mpangaji mwenzangu ana watoto wa2 mmja yupo boarding mwingine std4 na huwa anashinda shule till kumi na mbili jion.huyu mama ful tym yupo nyumbani mara chache sana huenda kutazama miradi yake bt cha ajabu haus gal wake ndo anaepanga hadi bajeti,anafua nguo za mumewe jaman had vibukta,anaingia kufanya usafi chumbani kwa bosi wake yan inshort haus gal ndo kila k2.kwa mantiki hiyo baba mwenye nyumba akitoka na hauc gal kwa kweli hatakua na kosa kabisa coz hata radha ya mapishi ya mkewew haijui loo
 
Kwa hiyo kwako wewe hiyo ina justify mtu kutembea na house girl wake? Na wale vijana ambao ni bachelors na wana ma house girl wanaosafisha vyumbani kwao nao wana haki kutembea nao? Kweli ni sifa mwanaume kutokuwa na utashi na kuwa weak kwa kila anayeingia kwenye anga zako?

 
wakati mwingine wanaume tunasema maneno mabaya yanayoumiza sana wanawake!hili si jambo jema!fikiria mtu akuambie houseboy,mlinzi wako,au dereva wako ni mme mwenzio kwa mkeo utajisikiaje?lets respect women
 
ahmada umelewa, ahmada umelewaaaaaaaa, punguza kashfa kaka, afu hasira znapunguza maisha, magonjwa ya moyo humo humo, mie nlikutana na huyu bwana niaknunua kitab chake huo mshangao nlioupata ndio ulinifanya niamue kushea na wanajamvi. siafikiani na huyu nabii tito. usiact kama jina lako bana kha, umenkera ww
 
Ukila kuku wa haus gal wako huli wa haus gal wako bali unakula kuku wako mwenyewe
 

kwanza ni mlevi, huwa ananipiga, harudi home mpaka kesho yake, ukimuuliza hakujibu eti ni cold war! navumilia kwa sababu ya wanangu tu, ningeshasepa long tym. hivi majuzi tu kwa siye waislamu alisikia mtu kaja kwa wazazi wangu kutaka kuniposa upya tena si mke wa pili, mke haswa wa ndoa, alitoaje macho sasa alipopata hizi taarifa?? ni kaka zangu walimwambia yule mwarabu kuwa kie nishaposwa kitambooooooooooo! ila jamani nimesema hivi makusudi na huwa anaingia humu ataona tu! JARIBUNI KUWAHESHIMU WAKE ZENU!
 
Hata mimi sijawahi elewa kazi ya housegirl, niseme tu ukweli
Labda hapo baadae nitakapo kua na kazi, familia na mengine
I think ni suala la organization na role distribution ndani tuu.

mbona unajicontradict sasa.

umeanza na kusema HUJAWAHI ELEWA kazi ya housegirl, na wakati huo huo unafikiria kuwa na house girl utapo pata familia.
Any way, sio lazima u post hata usipokuwa na cha kupost, unaweza piga kimya sometimes, lol.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…