How Are Kenyans Possible?(Languages)

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Hello Dear JF Users.
Kenyans are further developed in different sectors.

Let me concentrate in Education especially in Linguistic/Languages
Kenyans speak fluent English contrary to Us Tanzanians who have been struggling a lot to achieve and encounter the language in both criterias speaking and writing..
I have witnessed many authors from Kenya having a collection of books we use in our Tanzanian Syllabus not only books but Dictionaries and other important tools concerning the Language.

Sio Tu Kiingereza bali Wakenya wako vizuri kwenye Kiswahili pia watu wao wanaongea kiswahili kizuri na hata katika uandishi wapo vizuri pia
Nimeshuhudia vitabu vingi ya kiswahili vya Wakenya vikitumika hapa Tanzania.

Hata Kamusi Sanifu pia tumekuwa tukizipata kutoka Kenya..
Nawajua baadhi ya waandishi vitabu mashuhuri akiwemo Ngongi wa Thiongo kutoka Kenya.

 
Nikubali nikusahihishe tu kidogo mleta mada, umahari kwenye uandishi hauhusiani hata kidogo na lugha ya kiingereza au hata kiswahili. 'Case in point' ni uliyemtaja, Ngúgí wa Thiong'o, ambaye huwa anaandika kwa lugha yake asili ya Gíkúyú ila anafahamika kote duniani.
 
Ni vema ungevitaja hivo vitabu maarufu vya Kiswahili vilivyo andikwa na Wakenya na vinatumika TZ. Kumbuka ndugu zetu ni mabingwa wa kufoji! Wanaweza edit cover tu ili ionekane kitabu wameandika wao.
 
Nawe nikusahihishe kidogo...

Ngugi alianza kuandika kwa Kiingereza na umaarufu wake aliupata huko. Riwaya zake za kwanza kama The River Between na Petals of Blood zilikuwa katika Kiingereza. The Devil on the Cross (kazi yake bora kabisa) na tamthiliya ya Nikiolewa Nikipenda ndiyo aliziandika katika Kikikuyu na baadaye akazitafsiri katika Kiingereza. Baadaye pia hata kazi zake zilizoandikwa katika Kiingereza nadhani alizitafsiri katika Kikikuyu (na Kiswahili) pia.

Ngugi pia siyo mwandishi tu lakini pia umaarufu wake unatokana na harakati zake za kutetea lugha za Kiafrika kama mkakati mama katika ukombozi wa kifikra wa Mwafrika. Anaamini kuwa Mwafrika hawezi kujithamini na kujiletea maendeleo ya kweli wakati akiwa ametengwa na utamaduni wake na kupotezwa hata asiitambue nafasi yake kifalsafa na kiutu katika dunia hii. Ukombozi wa kweli wa Mwafrika na kujiamini kwake kutawezekana tu pale atakapoanza kutumia lugha zake za asili na kurudi katika utamaduni wake kama ilivyo duniani kote. Kitabu chake cha Decolonizing the Mind ni mashuhuri sana duniani kote kwa waungaji mkono wa mkondo wake huu wa mawazo.

Akiwa kama profesa na mkuu wa idara huko Chuo Kikuu cha California, Davis, Ngugi ni mmojawapo wa wasomi wa Kiafrika wanaopendwa na maoni yao kusakwa sana hasa katika masuala yote yanayohusu ukombozi wa kweli wa Mwafrika; na ametunukiwa nishani na shahada nyingi za udaktari wa heshima kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani. Wengi wanaamini kuwa ndiye mwanariwaya bora kabisa wa Kiafrika baada ya Chinua Achebe japo hii inawatenga waandishi wengine magwiji ambao waliamua kutumia lugha za Kiafrika na hivyo hawajulikani sana kimataifa mf. Shaaban Robert na Euphrase Kezilahabi katika fasihi ya Kiswahili.
 
Hoja yako kuu hasa ni ipi?

Kulingana na sera za lugha na falsafa ya nchi katika matumizi ya elimu ni kweli hali ya Kiingereza huko Kenya na Uganda ni bora kuliko huku kwetu.

Mengine yote ni kama vile umetia mubaalagha (chumvi) sana ili kuunga mkono hoja yako. Vitabu vya msingi vinavyotumika katika mashule yetu ni lazima vipite katika Taasisi ya Elimu na sioni jinsi vitabu vya waandishi wa Kenya vinavyoweza kutumika katika mitaala yetu isipokuwa vile vya Fasihi ya Kiafrika ambako vitabu vya waandishi wa bara zima la Afrika (mf. Chinua Achebe wa Nigeria, Sembene Ousmane wa Senegal?, Peter Abrahams wa Afrika Kusini, Ngugi wa Kenya, Okot p'Bitek wa Uganda, Mariam Ba wa Nigeria, Kwasi Prah wa Ghana...) na wengineo.

Kamusi bora kabisa ya Kiswahili - Kiingereza/Kiingereza-Kiswahili inayotambuliwa duniani kote ni ile iliyochapishwa na TUKI (kwa sasa TATAKI) katika Chuo Kikuu cha Dar ea salaam.

Vitabu vya masomo ya Sayansi kwa shule za sekondari hasa kidato cha tano na sita ndivyo pia vina mawanda ya waandishi wa kimataifa zaidi na havijaandikwa na Wakenya wala Waganda...
 
Naifahamu historia ya uandishi wa Ngúgí. Alipoamua kuandika kwa lugha ya kikuyu walisema kwamba option zake zilikuwa kati ya umaarufu wake na kuandika kwa lugha yake asili. Ila alifanikiwa na anaendelea kufanikiwa kunyakua zote kwa pamoja. Point yangu kuu ndio hiyo.
 
Kama Mkenya ambaye nimewahi kuishi Tanzania nahisi nina uwezo wa kuchangia nini nilikiona kama kiini cha matatizo yenu kwenye suala la lugha. Kwenu huko uhuru wa mtu kutumia lugha aitakayo haupo kabisa, mumelazimisha Kiswahili huku mkijua chenyewe hakijajishosheleza. Mtu akiongea lugha yake ya asili mnamuona mshamba, akizungumza kingereza mnamuona mtumwa.

Binadamu anapaswa aachwe atumie lugha yoyote aitakayo ili awe na uhuru kimawazo, kimtazamo na kifikira. Niliwashangaa sana kwamba mtu anasomea kwa Kiswahili kuanzia chekechea mpaka darasa la saba, halafu mnamshtukiza kwa Kingereza pale anapoingia sekondari, hapo mnakua hamjawatendea haki wanafunzi wenu maana umahiri wa lugha huwezekana kama utaanza kuisomea ukiwa mdogo na pia kuitumia mara kwa mara.

Mara nyingi nilikua tukikaa kikao na Watanzania, hususan kama humo ndani kuna wageni kama vile wazungu, wahindi n.k., unakuta Watanzania wanaganda kabisa, midomo inakua kama iliyotiwa zege, hawachangii kitu, ila tukienda mapumziko ya kunywa chai jamaa wanatiririka maneno maneno balaa kwa Kiswahili, unakuta jamaa anaeleza baadhi ya points ambazo zingesaidia sana kama angeyasema kwenye kikao.

Tanzania, kingereza kwa sasa kipo tu kwa watoto wa vigogo "elites" na wenye hela zao ndio wanapelekwa kusomea kwenye shule za gharama, ambazo walimu wengi humo ni Wakenya na Waganda. Lakini wengine wote wameachwa wahangaike wenyewe kwenye st. Kayumba za kawaida huku wakiaminishwa kukomaa na Kiswahili kama namna ya kuonyesha uzalendo, ila kwenye nafasi za ajira inatangazwa "Lazima mhojiwa au msailiwa awe na uwezo wa kuongea na kuandika kwa Kingereza na kwa ufasaha".

Na hii ndio kiini cha mabango kama hili hapa

 
[emoji1547][emoji1547][emoji1547][emoji1547]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…