How can i get clients from different countries fortourism business

MZEE SERENGETI

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
214
Reaction score
10
Hope all is good have started my company dealing with tourism,but the main chalLenge am facing is the way of getting customer. Please assist.
 
mkuu uko wapi wewe? I want to start samthing about tourism hop utaniongoza then tutajua cha kufanya tukiunganisha akili zetu.
 
Ninavofahamu ni lazima uwe na website ya kampuni yako kwa ajili ya kujitangaza, pia ukiweza uhudhurie Tourism Expo zinazofanyika Ulaya na America kwa ajili ya kuitangaza kampuni yako. Pia Tembelea ofisi za Bodi ya Utalii kwa ajili ya kupata info zaidi
 
Ungeandika kiswahili ingesaidi sana.

Utalii wa Ndani unalipa.Fanya Promo itakulipa.

Ili kuhudhuria Tourism Exhibitions ni lazima uwe na pesa si chini ya US$ 5,000 kwa uchache sana na inabidi upige kama miaka kadhaa ndio unaweza kupata Agents.na pia sio Guarantee kwamba utapata Agents maana wao wanaokwenda pia wanakwenda ili kuonana na Agents wenzao kwenye biashara.

Nakushauri anza na utalii wa ndani na hudhuria maonyesho ya East Africa yote ili ujijenge.
 
Hope all is good have started my company dealing with tourism,but the main chalLenge am facing is the way of getting customer. Please assist.

Ni biashara ya namna gani???????you need to be clear, is it Accommodation business(hotel,lodge,Inn,?) Travel agency/ Tour Operator? car rental company? and location of your business?????? kwanini nauliza hivi? Mfano kama uko Kigoma na Una Tour Company.....ni ngumu kidogo kupata wageni directly from tourist generating countries mfano Ulaya Arabuni na Marekani Uchina ( hapa siongelei domestic tourists ambao ni mimi na wewe) kwa sababu gani Kilichopo kigoma mtalii akila hawezi shiba meaning very limited tourist attractions,facilities accessibility na GARAMA (huu mfano una apply Kagera,katavi,nk)...kama uko huko Unaweza jenga urafiki na kampani kubwa zinaweza kukulink na wageni wachache wanaopenda tembelea maeneo tofanuti na Northern circuit na kama sio uwindaji Kusini huko

Ungefunguka zaidi ningeweza kukusaidia kwa mawazo.....how....jitahidi uwe na active webpage kwenye social Media kama facebook, blogs etc na uwe una update kila siku kwa kuweka picha na story fupi fupi ..zinazovutia lakini..........pili Temeblea website za makampuni makubwa/ size ya kati hapa TZ nenda kwa page ile ambayo clients wanatoa feedback wengine wanaweka mpaka address zao ukizipata WASILIANA

.....Tengeneza brochures nyingi uwezavyo zisambaze maeneo ambayo wageni wanatembelea mfano peleka TTB Information center, TANAPA,Ngorongoro, mawizara mbali mbali , Ofisi za watu binafsi,,,Air port,mahotelini...ukisikia kuna mkutano mkubwa hoteli fulani?au any conference center peleka vipeperushi..... USISAHAU WIZARA YA MAMBO YA NJE PIA NI MUHIMU TENA SAANA

.......na maeneo mengine namaanisha Visitors Entry Point kama Tunduma,,,,,Namanga ,,,Holili,,,,nk...peleka vipeperushi vyako Kwenye Balozi mbalimbali.......MKUU HUTATOKA PATUPU......

......jitahidi uhudurie maonyesho HUSUSANI Karibu Trade Fair-Arusha, Indaba South Africa Kama HUNA PESA TAFUTA MAKAMPUNI YANAYOTUMA WATU WAPE VIPEPERUSHI WAKUPELEKEE, NA HATA MAONYESHO YA ULAYA WAWEZA FNAYA HIVYO

JENGA URAFIKI NA MADEREVA wanaondesha watalii.....mara nyingi wanakuwaga na wageni.......wao lazima wanaweza kukunganisha...

........fuatilia ratiba za ndege ndege kubwa( Mashirika makubwa kutoka Ulaya na Arabuni hata Uchina kama yapo-waongea kichina lakini?) kuna wageni wanokuja wenyewe bila kuwa na AGENT ( Tour Operator) nenda Airport na Bango la kampuni yako if you are Luck huwezi toka kapa( ili ufanikiwe ktk hili jenga urafiki na madereva tax wanaopark airport)........

KUMBUKA hii ni biashara inayolipa saana KAMA ukitumia akili za zaidi ya kuzaliwa KWANI kuna makampuni machache yamehodhi/shikilia hii biashara...na mara nyingi wanawabania saana

Kufanikiwa zaidi ungeweza anza kwa kuanjiriwa kwenye kampuni inayofanya biahsara kama ya kwako hata kwa miezi 6 tu inatosha

Kumbuka BIASHARA ya utalii inahitaji UAMINIFU wa hali ya juu na uvumilivu kwani inachukua muda kidogo kuanza kuiona faida kama...huna mtaji mkubwa wa kuanzia

Kila la kheri by the way umesajili biashara yako???????????????
 
Duh,Jamaa hapo juu umemaliza kila kitu.Stay Blessed.

tatizo nahis litamkuta kwenye Usajuili,maana nasikia wana masharti magum sana.
Inatakaiwa kwanza uwe na gari si chini ya gari 5 za Safari,we jiulize gari moja si chini ya 45m.
Hapo pakoje hapo.
 
Duh,Jamaa hapo juu umemaliza kila kitu.Stay Blessed.

tatizo nahis litamkuta kwenye Usajuili,maana nasikia wana masharti magum sana.
Inatakaiwa kwanza uwe na gari si chini ya gari 5 za Safari,we jiulize gari moja si chini ya 45m.
Hapo pakoje hapo.

Mkuu habari ya Zenji
magari sio Issue hata kidogo mkuu...hayo ni matakwa ya sheria....na kama unajua kwa Tanganyika...kila jambo linawezakana..........Kampuni zipo nyingi ambazo hata gari moja hawana...na wanachapa biashara
cha msingi angetuambia biashara yake ni IPI HASA mie nimehisi tu kwani ndani ya utalii hata muza vinyago ni biashara ya Kitalii, Aseme ni aina gani ya BIASHARA
 
Duh,Jamaa hapo juu umemaliza kila kitu.Stay Blessed.

tatizo nahis litamkuta kwenye Usajuili,maana nasikia wana masharti magum sana.
Inatakaiwa uwe na gari 5 za Safari

Pia ziwe mpya, less than 5 years old.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…