Kusema kweli mambo haya vijana wakati wa uchumba huwa wanazembea na kuyadharau. Siri hizi huwa muhimu sana kujua mtu ana mtazamo gani kuhusu mambo. Kwa mfano kutokana na familia yake ilivyo, mwingine anaona wanandoa kutembea nje si jambo baya kwa sababu amewaona wazazi wakifanya hivyo mara kwa mara.
Sasa ukimwambia mwenzio ni vizuri, ili kisaikolojia ajue kuwa ikiwa itatokea hali kama hii reaction ya mwenzie itakuwa nini.
Haya mambo ya kusema siri hata hivyo hapa bongo hata ukisema siri zote hakuna anayejali, au hatuzijali wakati ndo muhimu kweli.
Mi nilipooa mke wangu alikuwa mwaminifu sana, lakini akasema babake alikuwa na watoto kibao nje. Hivyo yeye anaamini kuwa wanaume wote hutoka nje. Kutokana na kufikiria hivyo, hata nifanye nini kumhakikishia sitoki nje bado hakubali. Hatimaye yeye katoka, kwa kuhisi tu kuwa mimi nimeshatoka. Baada ya kugundua anatoka, ninawaka, yeye anaona ni kosa dogo tuuu!!!
Ningejua ningeifanyia kazi hiyo siri, nisingeoa hapooooo.