Data protection za nchi kibao zinafanana, ku-implement hapa Tanzania sidhani itakuwa shida... mimi naona kwenye vitu vingine kama hivi, hamna haja ya kuanzisha ma- endless consultations, ni bora tu ku-copy data protection acts kutoka nchi kama 5 hivi na kumodify ili ifanane na mazingira ya hapa Bongo, na kingine kuindeleza ili iendane na wakati.
Unajua nini, ni bora iwepo hivi sasa ili watu waanze kuzoea kidogo kidogo, hata kama haitakidhi mahitaji kwa 100%, kama walivyokwisha sema, ni bora nusu kibaba...
Na kwa uelewa wangu mdogo, hakutakuwa na data protection itakayo kidhi mambo ya wananchi wake kwa 100% anyway. So lets just roll it out, its high time!
Najua kama tunasubiria kutengemaa kwa ICT nyumbani ili ndiyo tuwe data protection act, tukifanya hivyo tutasubiri milele....
SteveD.