Nadhani hauna tabia ya kujitengenezea plan ya mwezi. Unapaswa kabla hujapokea huo mshahara bila kujali ni kiasi gani ujaribu kukaa chini, kama umeoa/olewa upange na mwenzio, ni gharama gani ambazo ni za lazima, mzitambue na mziandike mf. Bili za maji, umeme, rent kama mnapanga nyumba, bili za maziwa kama una watoto n.k
Ukisha fanya hivyo unaangalia kiasi kilichobaki na unaanza kuweka priorities, mf. Chakula (Ni lazima mle vile mlivyozoea au mnaweza kupata balanced diet kutoka kwenye cheaper sources?, fuel n.k. Kama una watoto wanaoenda shule, unapaswa kutenga japo kiasi kidogo sana uweke kenye bank acount zoa (Kama huna wafungulie), hii itasaidia sana ifikapo mwanzo wa term kutotumia fedha ya mshahara kulipia gharama za shule.
Hapo sasa unapaswa kutenga kiasi cha fedha za tahadhari ambazo zinapaswa zisitoke nyumbani (weka sehemu ambayo hugusi), then unaweza kujipongeza.
NB. Kila mwezi jaribu kupanga mambo ambayo utapenda kufanya mwezi unaofuata, hiyo itakufanya uweze kufikiri zaidi (Mimi binafsi kwa mfano, mwishoni mwa mwaka hukaa na mwenzangu na tunapanga mambo yote ambayo tunatamani kufanya ndani ya mwaka unaofuata, bila kujali vyanzo vya mapato, na tunapanga muda ambao tungependa tuwe tumefanikisha, kwa kweli inasaidia sana, na tumejikuta tunaepuka sana matumizi yasiyo ya lazima).
Nakutakia kila la heri. Hakuna kiasi cha fedha kinachotosha, tunahitaji mipango tu.