Mimi mtanismehe na hichi kidhungu - nikiandika au kuzungumza kidogo kichwa kinaanza kuniuma - lol.
Kwanza nahisi hilo la "kuruhusu, ku"motisha" na kusadia au kuunga mkono", ni wajibu wa pande mbili. Kwa nini iwe ni jukumu la mwanamume tu, au ndio hiyo "man supremacy?". Ni pale tu mnapo ruhusiana, kumotishana na kusaidiana ndio maisha ya upendo yanafana.
Lakini pia kuna tatizo kama wengine walivyodokeza juu ya "mapenzi ya siku hizi", watu wanakosa kuaminiana.
Kwa kufanya hayo hapo juu kwa nia njema, wengine huutumia uhuru huo na kuwageuka wenzao. Kuna mifano mingi ya wanaoanza maisha chini kabisa, lakini mara tu baada ya kufanikiwa ki"material", mume anakimbilia kuoa mke/wake wengine au kuweka nyumba ndogo, au yote mawili, ikitegemea na dini. Au mwanamke anakuwa mfujaji, anahonga, anaanza dharau na mflulizo wa mikasa.
Ni nadra siku hizi kukuta mwanamke asiyewania kujenga nyumba yake au kujenga kwao bila ya kumshirikisha mume wake, pengine kwa hofu kuwa siku yoyote anaweza kutimuliwa. Au mume kuanza kuwajengea mahara wake kama kwamba hana watoto wa kuwatayarisshia maisha.
All in all, it's too complicated. How a man/women would know (110%) that he/she wouldn't be betrayed? (Lo hapa kidhungu kimekuja wenyewe bila kuumwa na kichwa).
Tufanye nini - wanawake na wanaume ili tupendane, turuhusiane, tuhamasishane, tusaidiane, na zaidi tuaminiane?