Howo Vs Scania

Kwa mahitaji ya used engine za howo na faw kutoka china tuwasiliane 0621691776

 

Attachments

  • IMG_0545.jpg
    182.3 KB · Views: 21
Hivi bei ya Scania horse mpya bei gani please
 
Juzi hapa nilikuwa nafuatulia mjadala wa China kuipiku Japan kwenye mauzo ya magari ya umeme yaani mchina ndio anaongoza kwa kuuza magari ya umeme Duniani , Jana tna nikakuta mjadala china kuzipiga chini Scania,Volvo,Man kwenye mauzo ya malori na mabasi makubwa hapa Tanzania

Ukweli usewe tu Tabia ya mchina kuja na utamaduni wa kutengeneza bidhaa kulingana na pesa ya mtu ataendelea kuwapiga chini Wazungu kila kona atakuwa Tishio.. We unasema Gari Za china ni kimeo na huna hata bajaji ila matajiri wa Tanzania wamehamia china mnadhani ni wajinga?

Bidhaa za Mzungu zipo vingunguti pale ukiambiwa utoe bilioni moja upewe full scania hapa kati ya watu 100 ni matajiri watatu tu wanaweza kuzimudu sio kwamba watu hawapendi viatu vizuri ila ni kipato chetu kidogo, ndio maana matajiri walikuwa wananunua mitumba ambayo ikifika hapa ni kama kubeti linaweza kudumu au kukusumbua

Ila Tajiri akinunua Howo au Faw mpya ana uhakika wa kulitumia miaka 6 bila usumbufu na pesa inarudi na garama ya manunuzi ni ndogo na ndio maana Mtajiri wamekimbilia china, Kwenye mabasi ndio hivyo hivyo mtu ananunua Yutong kwa bei cheap analitumia kwa miaka 5 na halisumbui pesa ikirudi anazuza , kila Tajiri anapenda Marcopolo ila miliomi 800 nani anazo?
 
Thanks man
 
Wajanja kwenye modern investment hawaangalii gari itadumu miaka mingapi, wanaangalia how flexible wanaweza kuwa endapo watakuwa na gari fulani mkononi, say DAF. Dunia ya sasa inabadilika kila uchwao. So investor mwenye akili hawezi kufikiri kununua gari kwa kufikiri itamsaidia up to 20 years to come kwa sababu dunia inabadilika haraka sana. Kutokana na hayo, mimi nimefanya utafiti mdogo tu (observatory) nimegindua kwa Tanzania matajiri wengi wameachana na magari yanayodumu muda mrefu kama scania wamekimbilia magari ya kichina especially HOWO. Angalia akina Dangote, Lake oil na wasafirishaji wengine wa mafuta wanatumia sana hizi gari kwa ajili ya flexibility (They are cheap). Yani chochote kikibadilika it becomes easy to switch to it.
 
Wee ni wakala wa HOWO NA ZHUNGTONG!
 
Hata Sina hobby nalo , la kizamani sana mkuu
 
Huyu jamaa anaelewa kuhusu magari
 
It all because of business approach, watu wanata return ya haraka in a low cost.
Quality and durability imewekwa pembeni, but hiyo tanzania, european coutries, south america hata hapo south africa wana approach gani? Tusije tumia merit za tz tukadhani wengine ndio wako hivyo hivyo
 
sijaelewa unavosema ya pili kwa nguvu...
nguvu inatokana na horse power bhana mfa
Sijajua kama umewahi fanya biashara zote mbili na ukalinganisha Faida, uchakavu, na thamani ya gari kulingana na muda uliolitumia, kati ya tipa na semi au hata kipisi. Hela ya tipa ni ya matumizi ya hapa na pale lkn kama unajenga kampuni biashara ya tipa hunishawishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…