FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari!
Kampuni kubwa ya teknolojia ya Kichina Huawei (Huawei Technologies Co., Ltd.) imezindua mradi wa ufugaji wa nguruwe kupitia teknolojia ya Akili Bandia (Artificial Intelligence) Jumatatu wakati kampuni hiyo ikigeukia katika maeneo mengine ya kibiashara wakati biashara yake ya simu janja (smartphone) ikikabiliwa na vikwazo vya kibiashara vya Marekani.
Kampuni hiyo kubwa ya simu nchini China ilizuiliwa kupata vifaa muhimu vinavyotumika katika uzalishaji wa bidhaa zake za simu janja baada ya serikali ya Trump kuitangaza kampuni hiyo kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa wa Marekani.
Mauzo ya simu janja za Huawei yaliporomoka kwa 42% katika robo ya mwisho ya mwaka 2020 kutokana na upatikanaji hafifu wa vifaa muhimu vinavyofahamika kama 'microchips' kulikotokana na vikwazo hivyo.
Kutokana na kudorora huko kwa mauzo ya simu janja, Huawei inatafuta vyanzo vingine vya mapato kwa teknolojia yake. Pamoja na teknolojia ya Akili Bandia kwa wafugaji wa nguruwe, Huawei pia inafanya kazi na sekta ya madini ya makaa ya mawe.
Kwa upande wa teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G, vikwazo pia vimeiathiri Huawei kupata baadhi ya vifaa muhimu vya usimikaji wa mtandao huo huku pia ikizuiliwa kuhusika katika usimikaji wa mtandao wa 5G katika nchi kadhaa kutokana na hofu juu ya usalama wa kitaifa.
Kwa taarifa zaidi kuhusiana na hili, waweza kuzipata kupitia vyanzo vifuatavyo:
1) BBC | Huawei turns to pig farming as smartphone sales fall
2) South China Morning Post | Huawei turns to AI pig farming as the Chinese tech giant explores new growth areas outside smartphones