Hububujikwa na machozi kila nikiona wanafunzi na wanavyuo wakilia na serikali kuhusu kero zao

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Pale ninapowaona kwenye kupitia luninga wakiilalamikia serikali kero mbali mbali wakati wakitafuta elimu – kero kama huduma duni vyuoni/mashuleni, ukosefu wa chakula cha kutosha, ukosefu wa walimu, vifaa vya kujisomea kama vile maabara na vitabu na kero zao nyingi nyingine. Na hasa pale tunaona wanasiasa na viongozi wa serikali hii ya CCM wakifuja pesa, wakiiba na kujitajirisha, wakipokea milungula na kuweka mabilioni huko Uswisi na kwingineko kutokana na mikataba mibovu nay a siri isiyokuwa na masilahi kwa taifa. Halafu hapo hapo wanajaribu kutafuta visababu vya kushindwa kuboresha elimu na mazingira yake. Ndiyo, huwa nabubujika machozi na kuilaani sana serikali ya CCM.
 

Mimi huwa nalia hasa -- haya magamba hayajali kabisa elimu, wanachojali ni matumbo yao! Siyapendi kabisa.
 
Kweli inatia machungu sana, hasa pale twaambiwa nchi tajiri lakini watoto wetu wanapata elimu kwa njia za tabu sana na kudhalilishwa.
 

Wapinzani kwenye halmashauri wanazoziongoza wamefanya nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…