SoC03 Huduma bora ndani ya nchi yetu

SoC03 Huduma bora ndani ya nchi yetu

Stories of Change - 2023 Competition

Fortuworker

Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
10
Reaction score
21
Ndg. Wanajukwaa wenzangu, Naomba kulipanda Jukwaa hili la Utawala Bora na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Nashukuru kwa kupata Nafasi ya Kupaza sauti Na Nakusema. Natambua Mchango Mkubwa wa "HUDUMA BORA NDANI YA NCHI YETU". Inayotolewa na Utawala Bora Wa Serikali ya Awamu ya Sita, Chini ya Utawala wa Raisi Wetu, Mpendwa. Mama yetu, Mh, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ndg. Wanajukwaa Ni dhairi shairi, Uwajibikaji wa watumishi wa umma Hapa Nchini, umezidi kuzaa Matunda Chini ya Utawala Bora na kuleta Mabadiliko Chanya katika Ukuaji wa sekta mbalimbali hapa Nchini. Kama vile Afya, Elimu, Michezo, na Teknolojia.

Ndg. Wanajukwaa katika Kipindi Ambacho nimebahatika kushuhudia Mafanikio yaliyoletwa na Utawala bora na Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma, Ni Awamu Hii. Nimegundua na kujifunza. Utawala Bora: Ni matumizi ya mamlaka ambayo Yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, Tija, uadilifu, usawa, na Unafuata utawala wa sheria.

Ndg Wanajukwaa Naomba Nipende kuwa Muwazi Kabisa, katika Dhama za utawala zilizopita za nchi yetu hazikufikia Kiwango cha Utawala bora na uwajibikaji katika Utumishi wa umma kama ilivyo awamu hii. Sasa tunaweza kushuhudia sisi Wenyewe kwa Kuona Utawala Bora unazingatia, Matumizi Sahihi ya dola, Matumizi Mazuri ya Rasilimali kwa faida ya Wananchi, Matumizi Mazuri ya Madaraka ya Viongozi, kwa kujua na kutambua Madaraka waliyonayo na Matumizi yake. Na Ni Sahihi kwamba huko nyuma. Tuliona Baadhi ya Viongozi wakipandisha Mabega na Kuamua Kitu anachojisikia. Lakini ni dhairi, Kwa Sasa Madaraka Yanatumika Ipasavyo kulingana na Mipaka iliyowekwa na Katiba na sheria.

Ndg. Wanajukwaa Kama tunavyoweza kuona Awamu ya Sasa. Ni Matokeo ya Utawala Bora na Uwajibikaji wa Utumishi wa umma kutoa 'HUDUMA BORA NDANI YA NCHI YETU'. Kupitia Matumizi Mazuri ya rasilimali za nchi, kama vile Uwekezaji wa Bandari na Mashirika ya Umma. Na Kuleta Maendeleo Endelevu, kupungua kwa umasikini, ujinga na maradhi. Kutokomea kwa Rushwa Ikiwa Mtu kupata Huduma Bora Kwa Wepesi. Kuwepo kwa Huduma Bora za Jamii kama Vile Afya, Elimu, Maji, Barabara na Umeme. Kuwepo kwa Amani na Utulivu Ndani Na Nje ya Mipaka ya Nchi yetu. Kuheshimiwa kwa Haki za Binadamu. Kuwepo utatuzi wa migogoro kwa Mujibu wa sheria, Taratibu na Maridhiano ili kuleta Ustawi wa Wananchi.

Ndg. Wanajukwaa Moja kati ya Misingi ya Utawala bora ni Uwajibikaji. Uwajibikaji Ni nini? Uwajibikaji: Ni hali ya Kiongozi na Mtendaji kuwa Tayari kujibu, kubeba dhamana na kutoa maelezo kwa Wananchi juu ya maamuzi au matendo aliyoyafanya katika kutekeleza dhamana aliyopewa. Kwa Mujibu wa Ibara ya 8(i) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania, 1997 Serikali ( Watumishi wa Umma) Watawajibika kwa Wananchi.

Ndg. Wanajukwaa Ili nchi iwe na maendeleo ni muhimu kwa kila mwananchi kudhamiria kufikia kiwango cha juu cha uadilifu na Uaminifu. Hii inamaanisha kwamba tunahitaji kufanya kilicho Sahihi bila Itikadi ya Mtu. kama Mtumishi wa umma, ili kufanya kilicho sahihi hapana budi kutekeleza Majukumu kwa kuzingatia Taaluma, kuwa Mwaminifu, na Kuwajibika. Serikali inajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wake ili waweze kuzingatia Utaalamu wao na wawe waaminifu na Wawajibike ipasavyo.

Ndg. Wanajukwaa Lengo ni Kusaidia kuelewa kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma. Ni Sambamba na sera, sheria na kanuni za Nchi kwa kutumia maadili ya Msingi. Ambayo ni kuzingatua Utaalamu, Kuwa Mwaminifu na Kuwajibika bila ya kujali Jinsia, kabila, Rangi, Cheo, Dini, au Umri. Kama Mtumishi wa Umma Pia ni Mlezi wa Dhamana ya Umma. Watu Unaowahudumia wanakutegemea utekeleze Majukumu yako kwa uadilifu na kwa kiwango cha juu cha uwezo wako. Hivyo una wajibu wa kuonyeaha kuwa unastahili dhamna uliyopewa kwa kutekeleza kwa vitendo maadili ya utumishi wa umma.

Ndg. Wanajukwaa kwa kutumia maadili ya msingi kwa kuzingatua Utaalamu. Maana yake ni kutoa huduma kwa viwango vya juu kabisa kwa kutoa Huduma bora. Kutoa Huduma Bora Maana yake Ni nini?. Ni kufanya kazi ya kuwahudumia wateja kwa ubora na ufanisi.

Ndg. Wanajukwaa Maadili yana Misingi Pia ya kufanya Kazi kwa Bidii, Bila kuwa na Upendeleo wakati wa kutoa Huduma. Na Kutumia Taarifa rasmi za kazi ipasavyo.

Ndg. Wanajukwaa Naomba Kulishuka Jukwaa hili, kama Mmoja wa wanaowajibika kuheshimu na kutekeleza maadili ya utumishi wa umma, Mimi Binafsi nimeridhia kuonyesha mfano wa kutekeleza Majukumu yangu kwa kuzingatia Taaluma, Kuwa Mwaminifu, na Kuwa Mwajibikaji kutokana na Dhamana ya Umma Niliyopewa. Na shauri na Wewe Pia Hapo Ulipo Unatakiwa uwe Mfano wa Kuigwa.

F.N.Charles
 
Upvote 1
Back
Top Bottom