Huduma hospitali za umma zinatisha..and...the way forward..

Huduma hospitali za umma zinatisha..and...the way forward..

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
utafiti wangu wa muda mrefu kwenye hospitali za umma umebaini yafuatayo:-

1) Huduma ni mbaya sana na pia wagonjwa wengi hawapewi matibabu yanayokidhi khali zao.

2) Pamoja na baadhi ya madawa kutolewa kwa bei poa lakini hayawafikii wagonjwa bali kwa kutakiwa kuyalipia au kuelekezwa kwenye maduka ya madawa yanayomilikiwa na wahudumu wa hospitali za umma.

3) Wahudumu wengi wa hospitali za umma wanafanya biashara ambazo zinashindana na huduma za mwajiri wao na hivyo kuleta mgongano mkubwa wa kimasilahi na hivyo kuzorotesha huduma za mwajiri wao.

4) Madai ya khali bora yaliyosababisha mgomo wa madaktari yana msingi isipokuwa viwango vya malipo wakiyokuwa wakidai yako juu ya uwezo wa serikali.

5) Kutokana na mazingira mabaya ya kufanyakazi, tabia za wahudumu (Yaani madaktari na wauguzi na wasaidizi wao wote kwa ujumla) ni mbaya na wamekuwa wakitumia matusi, vipigo na hata kuwahujumu wagonjwa kinyume na maadili ya kazi zao.

6) Majengo mengi yamechoka na hata ukarabati hayafai ila kubomolewa na kujenga mapya na yenye ghorofa nyingi angalau zisipungue 8 ili kumudu mahitaji yaliyopo ya wagonjwa na uhaba wa ardhi.

7) Dawa nyingi ambazo zimepitwa na wakati kwenye famasia za wahudumu tajwa baadhi yao hurudishwa na kubadilishwa na zile ambazo ni nzima na zile dawa zisizofaa kupewa wagonjwa ambao wengi wao ni masikini na wala hawajui hata kusoma au kuandika. Na hata yule anayejua kusoma huwa hana mazoea ya ukaguzi tajwa.

8) Wahudumu wengi bila ya hata haya hudai rushwa kutoka kwa wagonjwa ili kufanyakazi ambayo wanalipwa mishahara kama mikataba yao ya ajira inavyosema.

9) Tatizo la maji ni kubwa kwenye hospitali hizo.

10) Mrundikano wa wagonjwa wanaolazwa kwenye chumba kimoja na wengine hata kulala kitanda kimoja unatishia usalama wa afya za wagonjwa wenyewe na hata watoa huduma.

11) Maabara hazifanyi kazi masaa 24 na wikiendi na sikukuu eti zimefungwa. Mgonjwa akilazwa siku hizo inamaanisha matibabu yake ni ya kubahatisha tu kwa gharama kubwa kwa mgonjwa na serikali kwa sababu ni tiba pata potea tu..........

The way forward:-

1) Serikali lazima itenge angalau bilioni mia tatu kwa mwaka katika mradi maalumu wa kuimarisha hospitali zetu za Umma. Visingizio kuwa hakuna pesa sasa vifikie ukomo tumechoka kuona wagonjwa masikini wanavyotaabika!

2) Waziri wa afya na Katibu Mkuu wake lazima wawe walikwisha kuwahi kuwa madaktari/wauguzi ambaye wanayoyafahamu matatizo ya hospitali za mikoani na wawe wametoa huduma kwenye hizi hospitali kwa miaka isiyopungua 15 hivi.

3) Kwenye katiba ya nchi iwekwe wazi kuwa hakuna hata sumni ambayo itagharimia watumishi wa umma katika hospitali ambazo siyo za umma. Mwanya wa viongozi kutibiwa nje ya nchi na hata kwenye hospitali za binafsi hapa nchini kunachangia sana katika kuzorota kwa huduma za umma. Viongozi ni wabunifu wa kuja na misamiati mingi ya kuonyesha wanajali huduma kwenye hizi hospitali lakini matunda yao kwenye hospitali husika ni ushahidi kuwa wafungwe kifungo cha milele kutumia fedha za umma kwenda ng'ambo au hata hospitali za hapa nchini. Haya yakifanyika utashangaa kuona huduma tajwa zitakavyopendeza.

4) Majengo yote ya hospitali zilizopo yafanyiwe tathmini na mengi yao ni ya kuyabomoa na kujenga majengo ya kisasa yenye huduma zinazokwenda na wakati. Lisiwepo jengo jipya ambalo ni chini ya ghorofa nane kukidhi mahitaji ya kihuduma na hadhi ya ardhi kesho na kesho kutwa. Mfano tu wagonjwa kwenye chumba kimoja wasizidi wawili na wawe na choo na bafu lao. Kila hospitali iwe na kisima na jenereta lao mbali ya kutegemea huduma za taasisi nyingine.

5) Zipitishwe sheria za kuwakataza watumishi wa umma kuanzisha na kumiliki au hata kuajiriwa na makampuni ambayo yanafanyakazi ambazo zinashindana na kazi za mwajiri wao ili kuondoa migongano mikubwa ya kimasilahi.

6) Vifaa vya uchunguzi wa kiawali vinunuliwe na kuwekwa kwenye hospitali zote za mikoa. Baadhi ya huduma hizi ni pamoja na T-scan/ C-Scan n.k. Taarifa nyingi za madaktari ambazo huzifanyia kazi ni za kukisia tu na hivyo hazina msingi wa kitaalamu na hivyo huongeza gharama kubwa kwa wagonjwa na mzigo kwa serikali kwa kutibu vitu ambavyo havipo!

7) Masilahi ya watumishi wote wa umma kuanzia Raisi hadi mfagiaji iwe na uwiano ambao umepitishwa na sheria ya bunge yakiwemo mafao ya kustaafu na kuondoa matabaka makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa yameleta msononeko uliopo kwenye sekta zote za huduma kama ya afya, elimu, polisi n.k na kuchangia huduma kuwa mbaya sana na hivyo kuhatarisha utaifa wetu ambao wanasiasa ni magwiji kuukemea bila ya kubainisha vyanzo vya mmommonyoko wa utaifa ambao unachangiwa sana na tofauti za kimapato kwa kazi ambazo zinafanana.

8) Baadhi ya hospitali tajwa zinatoza gharama ya tshs 10,000/= kwa kitanda ambao ni wizi wa macho macho mbali ya ukweli huduma ya umma ni lazima iwe bure. Inawezekanaje kitanda ambacho watu wamerundikwa kama ghala la kutunzia nafaka mgonjwa alipie chochote? Gharama tajwa zifutwe mara moja na tuachane na huu wizi wa kimachomacho kabisa.....

9) Maabara zifanye kazi masaa 24 kama ni wafanyakazi waongezwe wafanye kazi kwa shift na vipimo vya kisasa viwekwe. Ni upumbavu kutumia pesa nyingi kununua madawa ya tiba huku hatuna vifaa vya kung'amua magonjwa ya wateja wa hospitali zetu.............

10)...............................ongezeni nanyi nisitafune kila kitu hata mkashindwa kumeza........

[h=2][/h]
Mkuu.@Rutashubanyuma waku laumiwa ni viongozi wa Wizara ya Afya pamoja na Waziri wa Afya hawafai kuongoza hiyo Wizara.

MziziMkavu hata JK ambaye amewapachika pale ni bomu. Yule Mwinyi sifa aliyonayo ni kuwa baba yake aliwahi kuwa Raisi.........bila ya kukemea hizi mbeleko za cronyism tunakoelekea ni machafuko.......................
 
Tanzania kwa sasa hatuna huduma za afya bali tuna usanii wa kiafya.
Kumpeleka hospitali za umma mgonjwa wako ni sawa na kumsindikiza kaburini.
 
Muhimbili+hospital.jpg
3940383859_73f48abf02.jpg
 
Wao na watoto wao hawatibiwi humo, watajuaje matatizo yote hayo?
Mtu kaumwa maleria tu kapelekwa sauz.
 
Unajua kitu ambacho hukitumiii ata kukitunza ni issue
Hawa viongozi tiba zao ni nje ya inchi sasa why wahangaike na hospitali zetu
Naona katiba mpya ianishe ili suala la tiba za viongozi maana wengine ata Check up anakwea pipa
 
Tena wodi za kinamama na za watoto hali inatisha zaidi maana kule ni kupakatana!
 
[/QUOTE]
hongera sana mkuu Rutashubanyuma kwa kuleta mada hii!nami naomba nichangie kama ifuatavyo;
1.Nakubaliana na wewe kuwa utoaji wa huduma katika mahospitali yetu kwa ujumla wake(Private na umma) bado uko ICU.kwa hospitali za umma huduma mbaya zinachangiwa na ukosefu wa madawa na vifaa tiba,miundo mbinu mibovu,wafanyakazi kukosa motisha na ukosefu wa weledi(incompetency) kwa wafanyakazi hasa katika level ya zahanati na vituo vya afya.mfano usitegemee mgonjwa wa stroke katika hospitali ya wilaya au mkoa kupata matibabu 'sahihi' ikiwa hakuna kipimo cha CT scan ya umma katika mkoa huo.kwa upande wa hospitali binafsi ubovu wa huduma mara nyingi husababishwa na ukosefu wa wataalam wa kutoa huduma na pia utoaji wa matibabu hauzingatii miongozo ya MOHSW.
1) Huduma ni mbaya sana na pia wagonjwa wengi hawapewi matibabu yanayokidhi khali zao.
2.Hili ni tatizo kubwa na sababu zake ni zile zile,unawalipa kiwango kidogo cha mshahara watumishi wako,haupeleki madawa kwa wakati katika hospitali matokeo yake unajenga tabia ya watumishi kujibebea madawa kwenye mapochi na kuja kuwauzia wagonjwa hospitalini au kuwaelekeza kwenye maduka yao ya dawa.kimsingi ni lazima tuhakikishe dawa muhimu zinapatikana kwa kipindi chote cha mwaka ndipo tutakapoweza kudhibiti ufisadi huu.najua kuna ambao watakaosema kuwa dawa hizi huibiwa hapo hapo hospitali na kuuzwa kwenye maduka ya nje,sikatai lakini kuna lundo la dawa na vifaa tiba vya msingi ambavyo vinatakiwa kuwepo mahospitalini lakini havipo MSD na vinapatikana kwenye maduka binafsi au hospitali binafsi.
kimsingi serikali kupitia MSD itimize jukumu lake la kuweka dawa na vifaa tiba vya msingi ili iweze kupambana na rushwa hii na pia ni lazima kuongeza motisha kwa watumishi wa afya kwa kiwango kitakachomfanya muhudumu wa afya asifikirie kuwa mjasiliamali bali afikirie kuwa mtoa huduma.
2) Pamoja na baadhi ya madawa kutolewa kwa bei poa lakini hayawafikii wagonjwa bali kwa kutakiwa kuyalipia au kuelekezwa kwenye maduka ya madawa yanayomilikiwa na wahudumu wa hospitali za umma.

4.mkuu msingi wa madai ya maslahi ya madaktari na watumishi wa afya kwa ujumla ni utafiti uliofanywa na serikali yenyewe miaka kadhaa iliyopita.kimsingi madaktari hawakuibuka na madai ya kujikweza bali walitambua kuwa kuna utafiti ulifanyika na kuainisha viwango vya mishahara na motisha mbalimbali ambazo Tanzania kama nchi inayoendelea ingeweza kuafford.sisi wananchi tunasema na tunaona kuwa serikali ina uwezo mkubwa sana wa kulipa hao madaktari kiwango kilichosemwa ubaya walioko madarakani wamefikia ukomo wa fikra na pia ni watu waliolewa madaraka.
watu wanaomba kuongezewa fedha ya kuitwa kazini ili kuokoa maisha wewe unarespond kwa kuongeza fedha ya kuchunguza maiti........Hapa unahitaji uwezo gani kutambua kwamba serikali ni mbumbumbu.

4) Madai ya khali bora yaliyosababisha mgomo wa madaktari yana msingi isipokuwa viwango vya malipo wakiyokuwa wakidai yako juu ya uwezo wa serikali.

5.Naam ni kweli kabisa kuwa wahudumu wa afya wako katika msongo mkubwa wa mawazo.assume mtu anatoka nyumbani jioni kuelekea kazini huku kaacha mtoto wake mchanga nyumbani halafu anafika kazini hakuna vifaa vya kutolea huduma na bado analetewa kashfa na mwananchi(mara nyingi ni ndugu wa wagonjwa) ambaye aliichagua serikali hii mbovu,unadhani muhudumu huyu ataacha kuporomosha matusi au hata vibao?yeye sio yesu bana!
tabia hii ipo sana kwa wahudumu wa kada ya waganga na manesi wa vyeti na inawezekana ni kwa sababu ya kutofundishwa kwa undani juu a maadili ya kazi hii.

5) Kutokana na mazingira mabaya ya kufanyakazi, tabia za wahudumu (Yaani madaktari na wauguzi na wasaidizi wao wote kwa ujumla) ni mbaya na wamekuwa wakitumia matusi, vipigo na hata kuwahujumu wagonjwa kinyume na maadili ya kazi zao.

6.Hapo kwenye majengo ni kama ilivyo kwa shule na maofisi ya serikali.kwa kweli bajeti ya ukarabati au uendelezaji wa majengo ni hakuna.kwa sasa tunajidai tunajenga dispensari kila kata huku tukiacha kuboresha hospitali.

6) Majengo mengi yamechoka na hata ukarabati hayafai ila kubomolewa na kujenga mapya na yenye ghorofa nyingi angalau zisipungue 8 ili kumudu mahitaji yaliyopo ya wagonjwa na uhaba wa ardhi.

9.Mkuu hapa umenikumbusha kitu cha kuchekesha sana kwani kuna mambo yapo ndani ya uwezo wa wananchi lakini wanaisubiri serikali au mfadhili.unaweza kukuta hospitali imezungukwa na vijiji vyenye maji lakini wananchi hawa hawataki kuipatia maji hospitali hiyo,ni jambo la kushangaza sana lakini yanatokea.

9) Tatizo la maji ni kubwa kwenye hospitali hizo.

hapa kwenye way foward kuna baadhi ya vitu nakubalia na nawe hasa hasa hivi hapo chini
The way forward:-

1) Serikali lazima itenge angalau bilioni mia tatu kwa mwaka katika mradi maalumu wa kuimarisha hospitali zetu za Umma. Visingizio kuwa hakuna pesa sasa vifikie ukomo tumechoka kuona wagonjwa masikini wanavyotaabika!

2) Waziri wa afya na Katibu Mkuu wake lazima wawe walikwisha kuwahi kuwa madaktari/wauguzi ambaye wanayoyafahamu matatizo ya hospitali za mikoani na wawe wametoa huduma kwenye hizi hospitali kwa miaka isiyopungua 15 hivi.

3) Kwenye katiba ya nchi iwekwe wazi kuwa hakuna hata sumni ambayo itagharimia watumishi wa umma katika hospitali ambazo siyo za umma. Mwanya wa viongozi kutibiwa nje ya nchi na hata kwenye hospitali za binafsi hapa nchini kunachangia sana katika kuzorota kwa huduma za umma. Viongozi ni wabunifu wa kuja na misamiati mingi ya kuonyesha wanajali huduma kwenye hizi hospitali lakini matunda yao kwenye hospitali husika ni ushahidi kuwa wafungwe kifungo cha milele kutumia fedha za umma kwenda ng'ambo au hata hospitali za hapa nchini. Haya yakifanyika utashangaa kuona huduma tajwa zitakavyopendeza

6) Vifaa vya uchunguzi wa kiawali vinunuliwe na kuwekwa kwenye hospitali zote za mikoa. Baadhi ya huduma hizi ni pamoja na T-scan/ C-Scan n.k. Taarifa nyingi za madaktari ambazo huzifanyia kazi ni za kukisia tu na hivyo hazina msingi wa kitaalamu na hivyo huongeza gharama kubwa kwa wagonjwa na mzigo kwa serikali kwa kutibu vitu ambavyo havipo!

7) Masilahi ya watumishi wote wa umma kuanzia Raisi hadi mfagiaji iwe na uwiano ambao umepitishwa na sheria ya bunge yakiwemo mafao ya kustaafu na kuondoa matabaka makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa yameleta msononeko uliopo kwenye sekta zote za huduma kama ya afya, elimu, polisi n.k na kuchangia huduma kuwa mbaya sana na hivyo kuhatarisha utaifa wetu ambao wanasiasa ni magwiji kuukemea bila ya kubainisha vyanzo vya mmommonyoko wa utaifa ambao unachangiwa sana na tofauti za kimapato kwa kazi ambazo zinafanana.

ingawa ni jambo zuri lakini ni lazima serikali itekeleze suala zima la maslahi bora kwa mtumishi wa afya kwanza kabla ya kufanya hili hapa chini,na pia lisiwe kwa watumishi wa afya pekeee bali watumishi wote wa umma ikiwa ni pamoja na mawaziri.
5) Zipitishwe sheria za kuwakataza watumishi wa umma kuanzisha na kumiliki au hata kuajiriwa na makampuni ambayo yanafanyakazi ambazo zinashindana na kazi za mwajiri wao ili kuondoa migongano mikubwa ya kimasilahi.

mkuu hapa napingana na wewe ,kuanzia sasa ni lazima tuondokane na dhana ya kwamba huduma ya afya ni bure.lazima watu watambue wazungu ndio wanatulipia gharama za huduma hizi tunazoziita 'bure' nadhani ufike wakati tukubali kuwa huduma ya afya ni lazima ilipiwe,watu wahamasishwe kujiunga na mifuko ya bima za afya.ni aibu kuona mama mjamzito analetwa na RAV 4 na kikapu chenye vitenge vya wax halafu anajifungua bila kulipa chochote...huu ni utumwa wa kipuuzi.mmasai anamiliki ngo'mbe zaidi ya 80 halafu ashindwe kulipia elfu 10?ili serikali iweze kuboresha hayo uliyoyataja hapo juu ni lazima iweke mfumo wa uchangiaji ...nimeupenda huu mfumo wa CHF na Bima ya afya.
ni hawa hawa watanzania wanaoweza kutumia elfu 10 kwa siku mbili kwa ajili ya vocha ya kumsalimia shangazi wanashindwa kulipia kitanda kwa elfu kumi kwa wiki tatu wadini??nasisitiza watanzania sio masikini wa kushindwa kugharamia huduma hizi za msingi ni issue ya kuambiana ukweli tu.naamini watu wakianza kuilipia huduma hii wana uwezo wa kuidai iwe na ubora.
8) Baadhi ya hospitali tajwa zinatoza gharama ya tshs 10,000/= kwa kitanda ambao ni wizi wa macho macho mbali ya ukweli huduma ya umma ni lazima iwe bure. Inawezekanaje kitanda ambacho watu wamerundikwa kama ghala la kutunzia nafaka mgonjwa alipie chochote? Gharama tajwa zifutwe mara moja na tuachane na huu wizi wa kimachomacho kabisa.....

MKUU RUTASHUBANYUMA NAKUPONGEZA SANA KWA THREAD HII!!
 
Last edited by a moderator:
Huduma za afya ni janga la taifa, Elimu kadhalika. Sijui wapi kuna unafuu!
 
Ruta hembu nipe taarifa za wale wagonjwa mmoja aliyefanyiwa oparetion ya kichwa badala ya mguu pamoja na yule aliyefanyiwa oparetion ya mguu badala ya kichwa vipi wanaendeleaje?
 
Tatizo ni nani anajali? Viongozi hawana time na wananchi tunaishia kulalamika tu. Hata malalamiko yetu yasipofanyiwa kazi tunaanza kulalamika upya kuwa malalamiko yetu ya awali hayajashughulikiwa. Kodi tunalipa wenyewe kwa ajili ya kuboresha huduma kama hizo, tuna haki ya kudai, hata kwa nguvu, kuwa kodi zetu zifanye kile kinachotakiwa kufanya. Kama walio madarakani wanadhani kuwa hawawezi kukifanya hicho tunachotaka wakifanye, waondoke na wasipotaka kuondoka kwa hiari yao basi kuwa na utaratibu ambao utatupa haki wananchi kuwaondoa na kuwaweka wengine watutumikie
 
wakati mwingine huwa namwomba Mungu sana!!
 
Unatarajia nini kama hakuna mitaala ya elimu.

Hayo ni matokeo ya kucheka na CCM.
 
kuna hospital inaitwa Homso Songea yaani ukienda pale kutibiwa na ukazidiwa ujue safari yako imefika. sijui Madaktari wa pale wanatumia dawa za kienyeji. coz hata wakirefer kwenda Peramiho wakifika huwa hawachuki round they die. mimi niwashauri kwa sasa karibuni hospitali za Kanisa only wrking effectively
 
Back
Top Bottom