SoC01 Huduma kwa wateja Mkoani Mara

SoC01 Huduma kwa wateja Mkoani Mara

Stories of Change - 2021 Competition

Timber TZA

New Member
Joined
Jun 1, 2020
Posts
4
Reaction score
3
Mkoa wa Mara una watu wenye kabila tofauti na nyingi ingawa matamshi yao kwa asilimia kubwa hurandana kwani huwa katika hali ya ukali.

Endapo kama wewe siyo mwenyeji wa Mkoa huo unaweza kustaajabishwa jinsi wenyeji wanavyowasiliana.

Matharan kwenye biashara husadikiwa kuwa mteja ni mfalme, lakini mkoani Mara ni agharabu kukuta watoa huduma wakizingatia dhana hiyo.

Wengi wao hawana "Nyama ya ulimi" kwa wateja wao, hutumia lugha ya ukali mithiri ya wanaogombana lakini katika uhalisia hiyo ndiyo aina ya kawaida ya kuwasiliana kwao.

Haiwezi kuwa ajabu ukienda hotelini na kukutana na hali ya namna hii;

Mhudumu: We, unakula nini? (akitaka kujua mteja anahitaji kuhudumiwa chakula gani).

Mteja: Ugali, Nyama.

Mhudumu: Sema kingine (akimaanisha chakula kilichotajwa na mteja hakipo).

Mteja: Lete ugali dagaa upesi

Baada ya Mhudumu kumpelekea mteja chakula utasikia, "Nipe pesa..."
Mteja: Shilingi ngapi?

Mhudumu; Kwani unajua shilingi ngapi?

Mteja anaweza kutoa kwa kukadiria na hapo utasikia akiambiwa, ongeza kiasi fulani au akirejeshewa chenji ikiwa kiasi alichotoa ni zaidi ya gharama.

Tukio Nililoshuhudia

NIMO ndani ya basi la abiria
linalotokea Sirari, Wilaya ya Tarime kwenda jijini Mwanza ambapo baada ya muda mfupi tangu safari ianze, nikamsikia kondakta akimwambia abiria aliyekaa kiti cha pembeni yangu karibu yangu:

Konda: Nipe hizo hela!

Abiria: Sh ngapi?

Konda: Kwani hujui?

Baada ya majibishano kidogo abiria akatoa nauli na ikawa imekamilika lakini majibishano yakaendelea;

Abiria: Si ungenifahamisha nauli sahihi kwa ustaarabu?

Konda: Kwani wewe nani? Usiniletee mambo yenu ya Kikurya!

Wakati wao wakiamini wanazungumza kwa njia sahihi, katika jamii nyingine ndani ya Tanzania mtu anayezungumza kwa mtindo huo angetafsiriwa kuwa mgomvi, asiye mstaarabu wala mwenye heshima na kwingine kungetokea kukunjana na kupigana ngumi.

Lakini mkoani Mara, aina hiyo ya mawasiliano huchukuliwa kama njia ya kawaida ya mtu na mtu kuwasiliana.

USULI;
Biblia Kutoka 15:23
"Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara"

Ahsanteni naomba kura yenu
0675834288
timbertza@gmail.com
 
Upvote 2
Back
Top Bottom