A
Anonymous
Guest
Uhitaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ni mkubwa sana, lakini wananchi wanakumbana na changamoto nyingi, hasa kupitia idara ya uhamiaji. Kama iliyokawaida, Wananchi wanapaswa kufika katika ofisi ya uhamiaji iliyopo ndani ya Ofisi ya NIDA kwa ajili ya ukaguzi wa viambatanisho vyao wanapoomba kitambulisho.
Safari yangu ya kutaka kujiridhisha kuhusu huduma hii muhimu ilianza takribani wiki moja iliyopita baada ya kupata taarifa kuhusu uwepo wa changamoto za kiutendaji, lakini pia nilikuwa nimeshuhudia wimbi kubwa la watu wanaotafuta huduma hiyo katika ofisi za NIDA Ukonga.
Nilianza kwa kufika eneo la geti ambapo utaratibu wa kujiandikisha ulikuwa mzuri na niliridhika. Baada ya kujiandikisha, nilielekezwa kupitia uhamiaji kwa ajili ya ukaguzi wa maombi yangu. Nilipofika, niliwasilisha fomu zangu lakini nikaambiwa moja ya fomu haipo, na hivyo nikahitajika kuileta baadaye. Niliona huo ni utaratibu wa kawaida tu.
Leo, tarehe 08.11.2024, majira ya asubuhi nilifika na kujiandikisha tena getini. Baada ya hapo, nikaelekezwa tena kwenda uhamiaji, ambapo walikuwepo wahudumu watatu: mdada mmoja, kijana mmoja, na kijana anayekaribia uzee. Nilimkabidhi yule mdada fomu zangu zote na nikasubiri huku nikihitaji kushuhudia huduma inayotolewa.
Alianza kuzichambua fomu zangu na kugundua kuwa nakala iliyopo ni copy, akasema wanahitaji OG kutoka kwa mwanasheria. Nilitoka na kwenda kuichukua kutoka kwenye begi nililoacha kwa walinzi, kisha nikarudi nayo. Baada ya kurejea, yule mdada aliendelea kukagua na akagundua sikuweka sahihi, akaniambia niweke sahihi. Nilipomuomba fomu ili nisaini na kuweka tarehe, alichukua fomu hizo kisha akaanza kunifokea na kuniamuru nitoke nje kwa maneno machafu:
"Toka nje wewe, unajifanya mkaka kumbe mnuka kwapa!"
Kauli hiyo ilikuwa ngeni masikioni mwangu. Wahudumu wenzake walikuwa wakisikia na mmoja wao, yule kijana anayekaribia uzee, alinambia, "Umeshaambiwa Toka, Toka." Yule mdada aliendelea kwa kusema, "Ngoja nitakuonyesha, wewe si unajidai mwanaume, nitakuonyesha."
Nilijikuta natoka nje nikiwa sijiamini kwa yale niliyoyasikia. Niliweka sahihi kama alivyohitaji akiwa nje, kisha nikarudi kuomba huduma. Nilipofika, yule mdada alikataa kunihudumia na kusema, "Sitakuhudumia, nilikwambia nitakuonyesha." Nilijaribu kwenda kwa yule kijana aliyekaa pembeni ili nipate huduma, lakini naye alikataa na kusema, "Kama yule amekataa nami siwezi."
Nilitoka nikiwa nimekosa majibu, na kiukweli najua wananchi wengi wanakumbana na hali kama hii. NIDA na Uhamiaji mna wajibu wa kufuatilia madhila yanayowapata wananchi kupitia mkasa huu ili kuwasaidia. Wananchi wanahangaika sana na huduma mbovu inayotolewa na baadhi ya watoa huduma wasioelewa majukumu yao. Hali kama hii inaweza kusababisha wananchi kumchukia kiongozi wa nchi pasipo kuelewa chanzo halisi cha tatizo.
Nimesikitika sana na naamini kuwa mtachukua hatua stahiki kuboresha huduma hii muhimu kwa wananchi.
Pia soma:
~ NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao
~ Waziri Bashungwa aitaka Idara ya Uhamiaji kuondoa urasimu wa kuwazungusha Wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa (NIDA)