HUDUMA MBOVU ZA BASI LA AIFOLA EXPRESS (Dar-kigoma)

Jimmy Haizer

New Member
Joined
Nov 22, 2014
Posts
1
Reaction score
1
Habari wanajamii, sijawahi kuona huduma mbovu za usafirishaji wa nchi kavu kama hizi za basi la AIFOLA EXPRESS linalofanya safari zake Dar-Kigoma, wahudumu wanakauli mbaya, hawajali wateja wao sio kwenye upande wa abiria wala mizigo, mara kadhaa limekua likichelewesha abiria kufika kwa wakati kwa kupigwa faini za kizembe kwenye mizani yakupimia uzito na ushuru wa kutoka stendi, kwenye upande wa mizigo ndio balaa zaidi, ukisafirsha mzigo kwenye hili basi uandae na muda wa kugombana na wahudumu maana usumbufu utakaoupata utajuta, AIFOLA EXPRESS MNATUKWAZA WATEJA WENU, JIREKEBESHENI
 
Peleka mzigo saratoga uone cha moto kuanzia ofisini kwao,

Utarudi Aifola mikono nyuma
 
Nasafirisha parcel na Aifola sijawahi kupata changamoto
Makampuni ya magari mengi yana changamoto,kama bado hujakutana nazo ni muda tu ndio utaamua. Hawana consistency ya huduma nzuri wala mbaya,wapo wapo tu.
 
Afiola ni moja ya basi standard kwa dar kigoma, bado hajapata upinzani ndo sababu wahudumu wanajisahau kwa customer care mbovu. Na maneno ya kuudhi
Ni swala la muda tu vumilieni, lami ikimalizika mtapata basi nyingi nzuri kwa route hiyo, hapo kampuni ya basi yenye udhaifu itaondoka kwenye biashara
Uliza watu wa kusini, begi la nguo lilikuwa na nauli yake , tofauti na nauli ya kawaida , leo hii buti la zungu anawasha ac dar mtwara ,mwanzo mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…