KERO Huduma mbovu za Benki ya ABC unapoomba mkopo

KERO Huduma mbovu za Benki ya ABC unapoomba mkopo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero

Tafadhari husika na kichwa tajwa hapo juu,

Mie ni mdau wa huduma za kifedha kutoka kwa makampuni mengi yanayotoa huduma hizo kila siku na ninafanya biashara.

Naomba kufikisha/ kusema/ kuwasilisha kero yangu kutoka mojawapo ya kampuni ya kifedha (African corporation Bank,ABC) inayotoa huduma za mikopo hapa nchini. Bank hii ina huduma /Sera mbovu Sana na sio shindani kulinganisha na Bank nyingine

Mfano: Mie nimefanya maombi ya mkopo tangu tarehe 22/05/2024 hapa Mbeya Mjini lakini mpaka sasa tarehe 17/06/2024 sijapata mkopo huo.

Nimejaribu kupiga simu na kwenda mara nyingi sana najibiwa nitalipwa nitalipwa lakini nikihoji kama kuna Changamoto kwenye nyaraka zangu za kuombea mkopo wanasema upande wangu hakuna shida

Na hii tabia upande wangu imetokea mara ya pili mkopo wa awali ulichukua wiki 4 kuupata tena baada ya kugombana nao

Naomba msaada wenu JF kutupazia sauti hizo tabia na Sera zao MBOVU waachane nazo maana hata nilivyoomba balance statement ili nihamie bank nyingine walinizungusha mpaka nikaghairi na biashar zangu zinaathirika

Nawasilisha
Ahsante
 
Hivi watanzania mmewekewa nini kwenye vichwa vyenu ni nani?

Yaani mkopo unalazimisha? Kwanini kama hawana huduma nzuri usitafute benki nyingine au taasisi nyingine zinazotoa mikopo?

Hivi ni lini watanzania wenzangu mtabadilika?
 
Hivi watanzania mmewekewa nini kwenye vichwa vyenu ni nani?

Yaani mkopo unalazimisha? Kwanini kama hawana huduma nzuri usitafute benki nyingine au taasisi nyingine zinazotoa mikopo? Hivi ni lini watanzania wenzangu mtabadirika?
mawazo yako na kichwa chako vimejaa matusi kama ulivyojidhihirisha hivyo unatakiwa kuwa menye busara na hekima unapojibu maana nilichoandika wenye akili wameelewa vizuri
 
Brother next time jiheshimu,wewe utaendaje kukopa benki ina ofisi kama kachumba ka duka la Mangi.
Umesoma kwa tabu sana,usijifanye rahisi.Umeshindwankwenda NMB,CRDB au hata Stanbinc ap.
 
Brother next time jiheshimu,wewe utaendaje kukopa benki ina ofisi kama kachumba ka duka la Mangi.
Umesoma kwa tabu sana,usijifanye rahisi.Umeshindwankwenda NMB,CRDB au hata Stanbinc ap.
Bank ni NMB, CRDB na NBC hizo zingine ni vijiwe vya wapiga dili
 
Back
Top Bottom