SoC03 Huduma mitandao ya Serikali sio Timilivu

SoC03 Huduma mitandao ya Serikali sio Timilivu

Stories of Change - 2023 Competition

Maxing maxed

Member
Joined
May 6, 2021
Posts
6
Reaction score
12
Je, ulishawahi kutembelea tovuti gani ya taasisi ya kiserikali?Ni kweli kuna watu wako nyuma ya mifumo hiyo na wajibu wao ni kutufikishia huduma nzuri ya mtandaoni.
Inasikitisha wakati ambapo dunia inaendeshwa kwa njia za kisasa za mtandaoni lakini Platforms zilizo chini ya Serikali hazitoi huduma timilivu. Na ikitokea changamoto katika namna ya kuitumia hiyo huduma ya mtandao unakosa msaada na kupelekea mambo yako kukwama ama kuingia gharama na hasara kufuatia changamoto hiyo. Pia huduma zimekuwa hazijitoshelezi na hivyo kuwalazimu watumiaji kwenda ofisini kupanga foleni.

Chini ni mifano kadhaa.

1. Kipengele cha contact us kina njia ambazo haziwezi kusaidia kwa haraka. Platforms mbalimbali namba za simu sio rafiki kwa mtumiaji pia email ukituma haujibiwi milele.
Hivyo nashauri Serikali iache kuweka hicho kipengere ili kutimiza wajibu bali iweke ili kusaidia raia. Mfano mzuri ni NECTA


2. Maandiko kwenye baadhi ya platforms hayajitoshelezi na hayawezi kutoa muongozo kamili kwa mtumiaji. Mfano, ukitaka kufanya utalii (Utalii wa ndani) ukitembelea tovuti ya TANAPA kwenye huduma mtandao unakutana na huduma zinataka tu login hakuna signup. Koo inatakiwa utumie muda wa ziada kujaribu kujua uanzie wapi.

3. Huduma mtandao ya POSTA iko vizuri katika mwonekano .Na pia program yao ya "posta kiganjani" inambinu za kisasa kabisa za usafirishaji wa mizigo. Lakini watu hawaitumii badala yake wanatumia huduma binafsi za mabasi kwasababu ipo kama kutimiza wajibu wala sio kutimiza malengo na wala haioneshi ushindani. Huduma mtandao ya POSTA ilitakiwa iwe inatoa huduma mtandao kama za UPs vile. Na cha ajabu siku moja nimekuta tangazo la Happy birthday ya supervisor mmoja wapo 😂

Screenshot_20230615-171445.jpg


4. TMS CHECK haitoi huduma za ziada ila mhimu kama vile kutoa taarifa ya unyanyasaji ama rushwa kwa askari wa barabarani, ama huduma ya kutafuta mumiliki wa leseni iliyopotea.
Niiombe Serikali iweze kuendeleza ubunifu katika huduma mtandao ili siku moja tuwe na huduma nzuri na nyingi zinazoisgia mtandaoni tu badala ya kila anayekwama mtandaoni achome nauli kwenda ofisi husika. Huduma mtandao inaondoa usumbufu na kurahisisha kazi pamoja na kuondoa myanya ya RUSHWA. Hivyo ni mhimu kuzipa kipaumbele na kuhakikisha zinatoa huduma thabiti kwa Watanzania.
Natamani siku moja TANAPA wanipe mwongozo wa kueleweka pamoja na namna ya kulipia online na hiyo itahakikisha watu hawatumii wadau binafsi kama vile "Safaris" kwa huduma za utalii ikiwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya vibali na usafiri ndani ya hifadhi zetu.
Natamani siku moja TRA watoe mwongozo wa kuhamisha eneo la TIN namba online mfano mtu akianzia biashara Tabora kisha kuhamia Geita basi aweze kumaliza kila kitu mtandaoni.
Ama siku moja niingie TMS CHECK niweze kupata huduma kama za kuripoti rushwa ama unyanyasaji unaofanywa na traffic barabarani badala ya kuishia kuandika namba ya gari na kusoma deni peke yake.
Pia siku moja kuwe na maelekezo na namba za simu ya mkononi kwenye tovuti za serikali na email ambazo ziko active.
Na siku moja kuwe na GPS tracking feature kwenye kwenye tovuti za PCCB ili kuongeza ushahidi na uhalali wa tukio la rushwa.
Kwa ujumla serikali ikiwekeza kwenye mifumo ya TEHAMA kikamilifu inaweza kutatua changamoto nyingi sana.
 

Attachments

  • Screenshot_20230615-164724.jpg
    Screenshot_20230615-164724.jpg
    52.6 KB · Views: 8
  • Screenshot_20230615-172218.jpg
    Screenshot_20230615-172218.jpg
    31.6 KB · Views: 6
Upvote 8
Back
Top Bottom