Wakulu jana nimesoma kwenye gazeti kuwa Zantel wameanzisha huduma ya internate kwa wale wenye BB ila kama vile ni makusudi au kupitiwa hawajatoa kiasi unachotakiwa kukilipia ili upate hiyo huduma,pia hatujui kama ni limited au unlimited,kwa yule mwenye taarifa zaidi na atuhabarisha,sisi watumiaji sasa tunakuwa na uwanja mpana wa kuamua umtumie mtoa huduma gani kati ya watoa huduma
Mkuu,huduma zao ziko kwa package,package ya week moja sh 12,000 mwezi sh 40,000 miezi mitatu 90,000. kujiuonga una *77207# jamaa inaonekana gharama zao ziko juu kuliko Zain.
Hio huduma wanayo siku nyingi sema jamaa zao wa marketing nadhani wana mitindio ya akili kwani tangazo ambalo wameweka jana ni la kuitangaza Blackberry Curve 8900 na wala hawajagusia kama wana huduma ya BIS.
Mimi nimewahi jaribu service yao kwa wiki moja lakini nikaamua kurudi Zain maana naona bado wako juu sana kigharama na haileweki eleweki...ni kama wako kwenye 'Beta' stage kama tiGO!