Huduma ya Fiber ya TTCL

Joined
Aug 15, 2018
Posts
19
Reaction score
19
Leo nilienda kujaza fomu pale TTCL-Tegeta kwa ajili ya huduma ya fiber nyumbani

Kwanza picha linaanza naambiwa utaratibu ni kujaza fomu kwanza halafu baadae mtu wa survey atakuja kungalia ndio taratibu zingine zinafuata, lakini makadirio itachukua kama mwezi mmoja hivi.

Nimejaza ile fomu lakini bahati mbaya sikumkuta fundi yeyote zaidi ya customer care.

Mliowahi kufunga kuna njia zipi ili nikamilishe swala langu chap chap?

Msaada wakuu..[emoji120]
 
Hapo atakuja surveyor, atachukuwa vipimo na mchoro, baada ya hapo mchoro uke utaenda Kwa management ya Biashara na Support then muhasibu atakupigia simu au watakuletea invoice… ni mzunguko Kama siku 2 tuu kama manager anakuwa SI mswahili.

Na kama vifaa vipo na kazi ni chache siku 1 mbele unafungiwa na kuanza kupata huduma.
 
Asante sana mkuu, nina imani jambo litafanikiwa maana nina uhitaji sana[emoji120]
 
Ofisi za TTCL Tegeta ziko sehemu gani mkuu?
 
Watakuja January 2023
 
upo maeneo gani mkuu hapa tegeta
 
Hao customer care wanachosha sana.

Utadhani kufungiwa fiber ni kama kuingia ikulu.

Inaonekana kama ni favor.
 
Kiongozi tunaomba mrejesho kama walikufungia
 
Mrejesho mkuu
 

Mrejesho ?
 
Mkuu, vipi ulifungiwa huduma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…