Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Shirika linalofuatilia upatikanaji wa huduma ya intanet la NetBlocks limesema huduma ya intaneti kwa majukwaa ya Facebook, WhatsApp na Instagram imerudi nchini Ethiopia baada ya kukosekana mwishoni mwa juma.
Taasisi ya Huduma za Habari ya Ethiopia na Kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Mawasiliano ya Ethiopia la Ethio Telecom hazikutoa maelezo yoyote kukubali ama kukanusha taarifa hizo.
Majukwaa mengine ya Twitter, YouTune, Snapchat na LinkedIn yaliendelea kupatikana. Hata hivyo, watumiaji waliokuwa wakitumia huduma ya VPN waliweza kupata huduma katika majukwaa yaliyokuwa hayapatikani.
Kukosekana kwa huduma ya intanet nchini Ethiopia kunakuja wakati Tume ya Uchaguzi ikitangaza siku ya Jumamosi kuwa inaahirisha uchaguzi wa Wabunge uliokuwa ufanyike Juni 5, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuahirishwa kutoka tarehe ya awali ya Agosti mwaka jana kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Huduma ya intaneti imekuwa ikikosekana mara kwa mara nchini Ethiopia kutokana na machafuko ya kisiasa, hasa katika eneo la Kaskazini la Tigray baada ya vikosi vya jeshi kuingia katika mzozo na Serikali ya eneo hilo.
Shirika la NetBlocks, lenye Makao yake Makuu nchini Uingereza, limesema linaendelea kufuatilia mwenendo wa Uhuru wa Intaneti nchini Ethiopia.
Chanzo: Reuters