Huduma ya kubandika kucha, kope za macho na kutoa magaga imepamba moto

Huduma ya kubandika kucha, kope za macho na kutoa magaga imepamba moto

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Siku hizi hii huduma imepamba moto kila kona ya mji yaani unakuta mtu amekodi fremu au anaweka banda ameariji vijana kabisa kazi yao ni kusafisha wamama/ wadada miguu kuwatoa magaga kuseti kucha kupaka rangi kucha kupunguza hadi kupachika kucha za bandia na kope za bandia.

Hii huduma kwa sasa wamama/ wadada (baadhi sio wote) imewafanya hawanawi tena miguu majumbani mwao yaani anatoka anaenda bandani unamkuta kanyanyuliwa miguu juu anafanyiwa hadi masage za miguu na kwenye vidole vya miguuni na kupandisha hadi sehemu za magotini. Hii imewafanya hadi dada zetu/mama zetu kuwa wavivu kwenye swala la usafi wao binafsi.

Hii imenifanya hadi nikampa masharti shemeji yenu ziku namkuta/ namfuma akifanyiwa haya mambo hataamini kama ni mimi kile nitakachofanya.

Hivi wamama/ wadada mnaelekea wapi? Badilikeni ndio maana kwa sasa wengine hamuolewi/kuachika kwa sababu ya mambo /starehe mnazojizoelesha ambazo ni aibu kwenu na familia.

1625747383548.png


1625747042521.png
Zaidi soma:
  1. Mke wako huwa anaoshwa miguu na kijana wake wa kutengeneza kucha?
  2. Mwanaume unaweza kukubali mkeo aoshwe miguu na kusuguliwa kucha na vijana wengine?
 
Mimi nikiona hayo makucha tayari najua huyo anatembea na mauchafu mwilini, hapo maana yake akikojoa haoshi na akikata gogo pia haoshi.
 
me nikiona hayo makucha tayari najua huyo anatambea namauchafu mwilini...hapo maana yake akikojoa haoshi na akikata gogo pia haoshi....
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] nilikua na mpango ukaniomba hela ya kwenda kubandika kucha yaani niliuacha siku hiyo hiyo.
 
Bongo bwana sijui muda wanaupata wapi wa kukaa sehemu Masaa kadhaa bila kufanya chochote.
 
Siku hizi hii huduma imepamba moto kila kona ya mji yaani unakuta mtu amekodi fremu au anaweka banda ameariji vijana kabisa kazi yao ni kusafisha wamama/wadada miguu kuwatoa magaga kuseti kucha kupaka rangi kucha kupunguza hadi kupachika kucha za bandia na kope za bandia...
Hahahaaa, sio wanawake tu mkuu, hadi wanaume siku hizi utawakuta kwenye hizo sehemu wanaoshwa miguu na kukatwa kuchwa, wabadilike wote.
 
Na wanaume nao kuwa chawa imekuwa ndio kazi inamuweka mtu mjini
 
Hao wapaka rangi na waosha miguu husugua vizuri na kutekenya hadi wasinzia, pia ni wapongeze maana wamejiajiri na kupunguzu umasikini.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] nlikua na mpango ukaniomba hela ya kwenda kubandika kucha yani nliuacha siku hiyo hiyo.
SEMA huna Hela ya kumpa akapake jel maana ni elfu ishirini hivi
 
Acheni uchawi jamani, hiyo ni ajira kwa vijana.
 
Hao wapaka rangi na waosha miguu husugua vizuri na kutekenya Hadi wasinzia, pia ni wapongeze maana wamejiajiri na kupunguzu umaskini.
Hapo kwenye kutekenywa nafikiri wengi wanapenda hapo, nilikuwa na manzi hakubali umguse unyayo wake…. ila kwa Mr Kucha anaenda kuoshwa.

Ukimuuliza anasema, yule sina hisia naye sisikii chochote…. NYIEEE![emoji16]
 
Hao wapaka rangi na waosha miguu husugua vizuri na kutekenya Hadi wasinzia, pia ni wapongeze maana wamejiajiri na kupunguzu umaskini.
[emoji23][emoji23][emoji23] ila wee dea bhana.
 
Wanafanya hayo yote kwa sababu kuu mbili,
•kushindana.
•Kuvutia wanaume.
 
Wanawake sijawahi waelewa
Hata mimi huwa siwaelewi hawa wanawake wenzangu wanaokaa kitako saluni au mwengine kusuguliwa miguu na mabaharia, nahisi ni uvivu wa kusafisha miili yao unaowasumbua, ni heri mtu ukanunua vifaa vyako vya kutosha kila weekend unasafisha miguu yako na kutengeneza kucha zao nyumbani kwako, naona kama ni salama zaidi maana vifaa unatumia pekeyako.
 
Back
Top Bottom