A
Anonymous
Guest
Huduma ya mabasi ya mwendokasi inazidi kuwa mbovu, wahudumu na madereva wananyanyasa sana abiria, tunacheleweshwa vituoni zaidi ya saa mbili na inakuwa kero tunachelewa makazini.
Serikali imeshindwa kabisa kusimamia huduma hii, heri iwape wawekezaji katika sekta ya usafiri wao watajua uchungu wa biashara hii.
Magari ni mabovu na machache, vituo kama Stop Vver, Suka, Temboni , Kivukoni, Jiji Posta ya zamani, na vituo vya Kariakoo abiria wanasimama zaidi ya saa 2 iwe ni asubuhi, mchana ama usiku. Tunakwazika kupitiliza, hii sio mwendokasi hii ni polepolekasi na shurubakasi.
Vituoni wameng'oa mabenchi hakuna tena sehemu za kukaa na wahudumu wana kauli mbaya sana za Kiswahili na lugha mbovu na ubabe usio na sababu za msingi kama vile abiria wanapata hisani ya kusafirishwa bure na hawalipi nauli.
Hii huduma isipochukuliwa hatua inakufa, hakuna sababu ya kutengeneza barabaraba mpya ikiwa huduma iliyopo ni mbovu na haichukuliwi hatua stahiki.
Hili ni doa kubwa sana kwa Serikali maana inaonekana inacheka na kufurahia wananchi wake wakiteseka kwa kitu kinacholalamikiwa kila siku.