KERO Huduma ya mabasi ya mwendokasi inazidi kuwa mbovu na mbaya kupitiliza siku hadi siku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Huduma ya mabasi ya mwendokasi inazidi kuwa mbovu, wahudumu na madereva wananyanyasa sana abiria, tunacheleweshwa vituoni zaidi ya saa mbili na inakuwa kero tunachelewa makazini.

Serikali imeshindwa kabisa kusimamia huduma hii, heri iwape wawekezaji katika sekta ya usafiri wao watajua uchungu wa biashara hii.

Magari ni mabovu na machache, vituo kama Stop Vver, Suka, Temboni , Kivukoni, Jiji Posta ya zamani, na vituo vya Kariakoo abiria wanasimama zaidi ya saa 2 iwe ni asubuhi, mchana ama usiku. Tunakwazika kupitiliza, hii sio mwendokasi hii ni polepolekasi na shurubakasi.

Vituoni wameng'oa mabenchi hakuna tena sehemu za kukaa na wahudumu wana kauli mbaya sana za Kiswahili na lugha mbovu na ubabe usio na sababu za msingi kama vile abiria wanapata hisani ya kusafirishwa bure na hawalipi nauli.

Hii huduma isipochukuliwa hatua inakufa, hakuna sababu ya kutengeneza barabaraba mpya ikiwa huduma iliyopo ni mbovu na haichukuliwi hatua stahiki.

Hili ni doa kubwa sana kwa Serikali maana inaonekana inacheka na kufurahia wananchi wake wakiteseka kwa kitu kinacholalamikiwa kila siku.
 
Kwanza phase 1 tu wameshindwa na bado wanaongeza mbagala na gongolamboto wataweza sio Tena mwendokasi Bali ni mwendokero kiukweli wametukosea sana heri warudishe magari ya kawaida
 
Furahia mradi kujengwa na mama, hayo ya mabasi ni katika mengineyo.
 
"Black people are not complete human beings because they don't have a good brain to govern the society as White people. They are still under the process of becoming the complete human beings."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
route ya kibaha wamefuta kabisa.
 
mama yuko vizuriiiii...makapuku mjipangee
 
Kwa kweli ktk hili ni big failure. Unasubiri basi zaidi ya nusu saa, kweli hii ndio Bus Rapid Transport?
 
Ikifika kituo Cha Muhimbili uwe na fedha taslimu Kila siku na saa hawana chenchi nasikia hawakosi elfu thelathini kila aliyeko kukata tiketi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…