Kwenu wanabodi,
Nimekuwa nimefanya utafiti katika kupata huduma ya macho ambayo yamenisumbua tokea darasa la 6,nilikataa kutumia miwani mpka nafika umri huu miaka 22 nimefika chuoni naona sasa kuna haja ya kutumia miwani.
Sasa nilikuwa naomba mnijuze kama kuna mtu anafahamu kituo kizuri chenye kutoa huduma ya macho kwa kutumia bima ya afya NHIF.
Mkikitoa CCBRT kwa sababu kwenye utafiti wangu nimebaini watu wengi wanakilalamikia siku hizi huduma zinazotolewa pale.