Huduma ya Magari ya Mwendokasi (BRT) Ianze Mbagala

Huduma ya Magari ya Mwendokasi (BRT) Ianze Mbagala

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

HUDUMA YA MAGARI YA MWENDOKASI (BRT) IANZE MBAGALA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mhe Lazaro Nyamoga imefanya ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundombinu na uendeshaji wa mabasi yaendayo haraka

Akiongea na wananchi wa eneo la Mbagala Kijichi Mhe.Nyamoga ameitaka serikali kuhakikisha wanapeleka huduma ya mabasi katika eneo la Mbagala Kijichi ili waweze kupata huduma bora za usafiri katika eneo hilo

"Wananchi wa Mbagala wanahitaji huduma ya mabasi yaendayo kwa haraka kutokana na uwingi wa wananchi pamoja na uhitaji wa huduma hiyo, hivyo maiomba serikali iweze kutoa huduma hiyo kwa haraka" amesisitiza Kamoga

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema tayari mradi umekamilika kwa asilimia 98 hivyo itaanza kutoa huduma ya usafiri katika eneo hilo

Mradi umekamilika kwa asilimia 98 hivyo tupo tayari kuanza kutoa huduma ya mabasi yaendayo kwa haraka katika eneo hili ila tunakamilisha asilimia zilizobaki" amesema Mhe. Zainab Katimba
 

Attachments

  • GMuYcysXYAAZWkt.jpg
    GMuYcysXYAAZWkt.jpg
    569.3 KB · Views: 9
  • GMuYcyxWYAA90GD.jpg
    GMuYcyxWYAA90GD.jpg
    559.8 KB · Views: 8
  • GMuYcytWUAAiugG.jpg
    GMuYcytWUAAiugG.jpg
    505.3 KB · Views: 12
  • GMuYcysWsAAncLo.jpg
    GMuYcysWsAAncLo.jpg
    265.9 KB · Views: 12
Bila uwepo wa kampuni ya UDART hata kule Kimara kusingekuwa na mabasi. Sasa ndio ninajiuliza DART kazi yake hasa ni nini? Tuna TARURA na TANROADS kwenye ujenzi wa miundombinu, hii DART ambayo haiwezi kuleta kampuni nyingine za mabasi si bora hii kazi aachiwe LATRA?
 
Back
Top Bottom