KERO Huduma ya maji wilayani Nachingwea ni changamoto; yakitoka ni machafu na kwa muda mfupi hukatika

KERO Huduma ya maji wilayani Nachingwea ni changamoto; yakitoka ni machafu na kwa muda mfupi hukatika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
4,495
Reaction score
5,025
Habari wanajukwaa wenzangu na Mamlaka zote zinazohusika.

Kumekuwa na sintofahamu sasa ya muda mrefu kuhusu nini hatima ya Wakazi wa Nachingwea katika upatikanaji wa Maji na Salama.

Tunaomba mamlaka zinazohusika ziingilie kati kwani mitaa mingi ya wilaya ya Nachingwea haina maji (kumaanisha kuwa hayatoki licha ya miundo mbinu hiyo kuwa imewafikia wananchi).

Utokaji maji mabombani umekuwa kero kubwa kiasi kwamba hatujui kama ni saa ngapi au lini tunayapata hayo maji na hata yakitoka ni machafu na kwa muda mfupi tu hukatika

Kwa leo niishie hapo ila naomba sana mamlaka husika ziingilie kati suala hili.
 
Back
Top Bottom