Huduma ya Starlink yaanza kupatikana nchini Kenya

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Huduma ya mtandao ya Starlink imeanza kupatikana nchini kenya kwa taarifa iliyotolewa na Bilionea Elon Musk.

Tanzania Nape alisema Musk hajatimiza vigezo.
 
Starlink imezindua internet yake nchini Kenya. Salamu ziwafikie TCRA ili wawakaribishe Starlink waje Tanzania kwa sababu internet yao itapatikana hata nje ya Kenya kwa sababu ni satelite. Sasa hii inawesa kusababisha Watanzania wakawa wanaenda kununua vifaa vya Starlink Kenya kimagendo na kuja kuvitumia Tanzania kama ilivyo kwa ving'amuzi vya Canal Sports kwa sababu ya kufuata bei nafuu. "Kama hauwezi kupigana nao, basi ungana nao"

Habari kamili.

Bilionea, Elon Musk ametangaza katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Kampuni yake ya Starlink, imezindua huduma ya internet yenye kasi, inayotumia satellaiti nchini Kenya, na kwamba kwa uzinduzi huo, mteja ataweza kupata huduma za kampuni hiyo bila kujali mipaka ya nchi hiyo.

Kabla ya uzinduzi huo nchini Kenya, wakati Fulani Tanzania ilipokea maombi ya kampuni hiyo kuja kuwekeza nchini, huku wadau wakisema itachochea uchumi wa kidijitali na itakuwa nafuu na yenye kasi.

Taarifa hizo zinasema, huenda hadi kufika Machi 2023 teknolojia hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya SpaceX itakuwa imeingia nchini.

Kwenye tovuti yao rasmi, Starlink ilitangaza mpango wao wa kuleta huduma hizo nchini kati ya Januari na Machi 2023, kama wangeruhusiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Hata hivyo, akizungumza na katika mahojiano maalum na Mwananchi Digital Februari mwaka huu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye; alisema Tanzania ipo tayari kuipokea internet ya Elon Musk 'Starlink', na kwamba wanasubiri wawasilishe nyaraka tu.

Chanzo: Mwananchi

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ila hii ilibidi ianze TANZANIA kwanza kabla ys KENYA
sema kwa kenya ni watu amabao hawapitwi na FULSA wakaichangamkia wakati sisi tunazubaazubaa

Mambo ya msingi serikali inaweka VIZINGITI kibao
Mambo ya KIPUUZI (dpword) ndio inaratibu mpk semina
Dah !! Nchi ya HOVYO sana
Huyo NAPE ndio aliiwekea UGUMU hiyo kampuni kwa kuipa mashart magumumpk ikaona ikate KONA sijui alipokea mlungula kwa kina TIGO na VODA ili waendelee kutukamua

We fikilia unapata internet ya SPEED kali hata ukiwa ndani ndani huko SAVULACHOLE polini na una STREAM NETFLIX safi kabisa au unashusha MADUDE ya maana Torrent
bila hofu ya NDUGU MTEJA UMEFIKIA 75% YA KIFURUSHI CHAKO
 
Nape si Alisema kigezo ni wao kuwa na Ofisi hapa Tanzania? Sidhani kama ni kigezo kigumu, its just dharau za wazungu kwetu,

Inawezekana Nape ameongea kisiasa ila chukua situation hii.
1. Starlink imekuja Tanzania umelipa hio milioni na nusu umenunua Dish lao
2. Umelipia Gharama ya usafirishaji 50k mpaka 100k toka Kwao hadi hapa
3. Kifaa kimefika kibovu
4. Ukisafirishe tena kiende Us ama Nchi ya kwao huko, Ufanyiwe replacement kirudi tena etc.

Usumbufu wote huu wa nini? Walishindwa hata kutafuta Agent hapa kwetu na kufungua ofisi ndogo kwa ajili ya support?

Na kama Nilivyosema post zilizopita wengi wenu humu mnasifia jina tu na sababu ni Elon Musk, kama TTCL imekushinda 99% huwezi ku Afford Starlink.
 
Wabongo ni watu wa kupelekwa na upepo sana , they barely do research on issues , wao ni siasa mwanzo mwisho . Duniani tu huko starlink imeshindwa kutoboa ndo ije iwe mbadala wa ISP hapa Tanzania ? Kifupi serikali imejaribu kuwalinda hawa watumiaji wa mwisho lakini suprisingly serikali ndo inalaumiwa kisa tweet moja ya Elon Musk. Ni jambo la kushangaza sana hasa ukichukulia wanaolaumu wengi ni graduate 🥹
 
Hujui unachoongea
 
Starlink imezindua internet yake nchini Kenya. Salamu ziwafikie TCRA ili wawakaribishe Starlink waje Tanzania kwa sababu internet yao itapatikana hata nje ya Kenya kwa sababu ni satelite. Sasa hii inawesa kusababisha Watanzania wakawa wanaenda kununua vifaa vya Starlink Kenya kimagendo na kuja kuvitumia Tanzania kama ilivyo kwa ving'amuzi vya Canal Sports kwa sababu ya kufuata bei nafuu. "Kama hauwezi kupigana nao, basi ungana nao"

Habari kamili.

Bilionea, Elon Musk ametangaza katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Kampuni yake ya Starlink, imezindua huduma ya internet yenye kasi, inayotumia satellaiti nchini Kenya, na kwamba kwa uzinduzi huo, mteja ataweza kupata huduma za kampuni hiyo bila kujali mipaka ya nchi hiyo.

Kabla ya uzinduzi huo nchini Kenya, wakati Fulani Tanzania ilipokea maombi ya kampuni hiyo kuja kuwekeza nchini, huku wadau wakisema itachochea uchumi wa kidijitali na itakuwa nafuu na yenye kasi.

Taarifa hizo zinasema, huenda hadi kufika Machi 2023 teknolojia hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya SpaceX itakuwa imeingia nchini.

Kwenye tovuti yao rasmi, Starlink ilitangaza mpango wao wa kuleta huduma hizo nchini kati ya Januari na Machi 2023, kama wangeruhusiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Hata hivyo, akizungumza na katika mahojiano maalum na Mwananchi Digital Februari mwaka huu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye; alisema Tanzania ipo tayari kuipokea internet ya Elon Musk 'Starlink', na kwamba wanasubiri wawasilishe nyaraka tu.

Chanzo: Mwananchi

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Aisee kwa wafukunyuzi tupeni tu utaratibu wa kupata hiyo huduma kutokea Kenya tuifuate tushachoka na haya majambazi ya humu
 
Screenshot_20230918_094225.jpg

Kama bando la siku tu huwezi kulimudu hizi gharama mtaziweza kweli??? Bora ujiunge na TTCL fiber to home
 
Back
Top Bottom