YAH: UNYANYASAJI WA ABIRIA
Nimekuwa nikisafiri na mabasi yaendao mikoani na mara kwa mara nimekuwa nikishuhudia unyanyasaji wa abiria kwa namna moja au nyingine kutoka kwa wahudumu wa mabasi hayo, pamoja na lugha chafu; kwa sasa kumekuwa na tabia kwamba makondakta ndiyo wenye mamlaka juu ya basi husika kuliko dereva ambaye kwa mtazamo wangu naona kama ndio ana dhamana kubwa juu ya abiria.
Tarehe 06/08/2013, Mimi na mke wangu na mtoto wetu wa umri wa miaka mitatu (3) tulikuwa tunasafiri kutoka Dodoma kuelekea Mbeya Mjini kwa basi la Hood, ambapo tulipofika eneo la mbuyuni basi liliingia na kusimama katika mgahawa ujulikanao kwa jina la al-jazera na mhudumu wa basi alitaarifu abiria wote kwamba tuna muda wa dakika kumi (10) kwa ajili ya kupata chakula.
Abiria wengine walianza kushuka, nami pamoja na mtoto wangu tulivhukua uamuzi wa kushuka vile vile; lakini eneo la kupita abiria lilikuwa limejaa mizigo (vifurushi) hivyo kufanya zoezi la kushuka kwenye basi kuchukua muda mrefu, ukizingati mimi nilikuwa kwenye kiti namba 49 na 50.
Baada ya kushuka, nilielekea chooni na huko kulikuwa na foleni; tulirejea kwenye gari kwa kupitia sehemu iliyokuwa inauzwa vinywaji baridi (soda na juice), lakini cha kusikitisha nilipofika eneo ambalo basi lilikuwa limeegeshwa nilikuta basi limeondoka, nilipoangaza barabara kuu niliona basi likiondoka kwa umbali wa takribani mita 500; nilijaribu kutafuta usafiri wa pikipiki kwa lengo la kufuatilia basi hilo, nikitarajia wahudumu watapewa taarifa za kutokuwepo kwangu kutoka kwa mke wangu (ambaye nimwacha ndani ya basi) na abriria wengineo. Lakini hatukufanikiwa kulikuta basi hilo na kuamua kurejea pale katika hotel ya aljazera, nilielekezwa kumuona mtu mmoja (ambaye nafikiri ni mmoja kati ya wamiliki au watumishi wa hotel), nilimweleza kwamba nimeachwa na basi; hivyo nilitaka kufahamu uwezekano wa kupata usafiri mwingine; lakini mtu huyu alishangazwa na tabia hiyo ya basi la hood kuacha abiria katika hotel hiyo, kwani alidai ktk siku za karibuni takribani mara tatu wameacha abiria.
Nilifanikiwa kupata basi la Abood na kulipa nauli nyingine kuelekea mbeya. Nikiwa njiani nilifanikiwa kuwasiliana na mke wangu na kumshauri anisubiri katika ofisi la basi la hood kwani alikuwa mgeni kabisa ktk mji huo na hatukuwa na mwenyeji, kwani lengo la safari yetu ilikuwa kushiriki katika maonyesho ya Nanenane-Kanda ya kusini.
Nilifika Mbeya Mjini majira ya saa 3 usiku na kuelekea ofisi za Hood na kukutana na mke wangu ambaye alinitaarifu kwa kulikuwa na abiria takribani 6 ambao tuliachwa wakiwemo mama wenye watoto wachanga amba tulikaa nao jirani ndani ya basi hilo; pamoja na taarifa aliyotoa kwa wahudumu wa basi hilo juu ya kuacha abiria wengine, wahudumu hao hawakujali na walisema watapanda mabasi mengine. Kuna abiria mwingine ambaye alipanda basi jingine na walifanikiwa kulikuta basi la hood kabla ya kufika Iringa na walijaribu kulisimamisha basi hilo bila mafanikio, mpaka walipolikuta tena eneo la makambako; ambapo abiria huyu alikuwa na mtoto mchanga na aliacha kila kitu ndani ya basi la hood yakiwemo mahitaji ya muhimu kwa mtoto.
Mimi nilikuwa na mtoto wangu ambaye chakula chake kilikuwa ndani ya basi la hood, hivyo hakuweza kupata chakula na kulazimika kumpatia soda tu mpaka tulipofika Mbeya.
Nilipofika Mbeya nilikuta ofisi za basi la hood zimefungwa na kumkuta mke wangu nje ya ofisi hizo.
Tilkwenda kituo cha polis kwa ajili ya kutoa taarifa na tulielekezwa kwenda ofisi za trafic, ambapo tulipofika pale mapokezi baada ya kueleza kwa ufupi mkasa huo, walituomba kuonana na oSS - Ndimbo ili kumpatia maelezo hayo na ndipo OSS alipowapa maelekezo askari waliopo maelekezo kuchukua maelezo na kufungua jalada la unyanyasaji wa abiria.
Baada ya kuchukuliwa maelezo, tumeahidiwa kupigiwa simu kwa siku inayofuata (07.08.2013).
Ningependa kufahamu zaidi juu ya sheria husika na kama naweza kupata msaada wa kisheria zaidi; kulikuwa na chama cha kutetea haki za abiria, bali sifahamu wanatendaje kazi zao na wanapatikana wapi.
Wakati umefika wa kuchukua hatua badala ya kulalamika, nategemea michango ya mawazo yenu