HUDUMA YETU NI "KUKUAGIZIA GARI KUTOKA NJE "

Dunia inazidi kuwa well organised ktk businesses. Hao beforward na exporters wengine wengi duniani NAO wanahitaji sole agents kama sisi ili biashara iende. Kwaivo kadri tunavyokuwa wengi ktk kuagiza ilimradi terms and conditions zifuatwe ndivyo automobile sector inakua.
Ni option ya MTU kwa kadri ya ufahamu na accessibility yake kuwatumia agents au ofisi za exporters moja kwa moja. Mimi naagiza gari za wateja wangu kutoka kwa hao Beforward na makampuni mengine ya kuaminika duniani. Nikifanya hivyo haiongezi gharama kubwa kwa mteja kama angeamua kuagiza directly kwao...ila pia kumbuka sio kila mteja atakae kuagiza yuko karibu na hizo ofisi...akiridhika utaratibu wa ofisi yangu hakuna tofauti kubwa....let say gari imekuwa na tatizo...bado hata mimi naweza claim kwa exporter ili hatua stahiki zichukuliwe kwa ajili ya mteja. NA SIO KILA HITAJI LA MTEJA LINAPATIKANA KWENYE KAMPUNI MOJA...sometimes Agent kama mimi lazima nitafute gari ya mteja toka zaidi ya exporter mmoja ili mimi na mteja turidhie pamoja, ipi tuagize...considerations zetu zikiwa quality ya gari. Mfano mimi nimefanya na SBT TZ office, badae nikaamua kusajili ofisi yangu binafsi ili mambo yaende, kwaivo sbt ni main exporter wangu, ila nisipopata kwao natafuta kampuni zingine za kueleweka.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Beforward gharama zao za uwakala wa kuligomboa gari bandarini zikoje mkuu?

Yaani ndinga limeshatua bongo nikalipia mazagazaga yote ya kodi na ushuru wa bandari sijui na ship delivery fee n.k,wao wanacharge kiasi gani
 
Beforward gharama zao za uwakala wa kuligomboa gari bandarini zikoje mkuu?

Yaani ndinga limeshatua bongo nikalipia mazagazaga yote ya kodi na ushuru wa bandari sijui na ship delivery fee n.k,wao wanacharge kiasi gani
Fee yao ya Clearing & Forwarding ni laki 3. Wanalitoa gari bandarini na kuliweka yard yao. Zaidi ya hiyo, wataku charge elfu 15 ya dereva na mafuta. Wanalitoa gari bandarini siku 2 tu baada ya meli kuingia. Ninachowapendea wapo fasta ku ship gari na kila kitu kipo wazi wana ku update kupitia account ya mybeforward. Pia wanakupunguzia bei hadi dollar 200 ya bei ya mtandaoni ukiomba punguzo. Kiujumla BeForward wapo vizuri sana.
 
Sawasawa mkuu. Nashukuru kwa kuwa muwazi aka open kuhusu business yako. Inaonekana una uzoefu mkubwa ambao umekuwezesha kutafuta niche katika hii biashara.
 
Yes, ila gharama za kutoa na gharama za bandari ni tofauti..kuna mtu aliambiwa hivyo akadhani gari kanunua japan, kalipa ushuru na clearing 300,000 basi mchezo umeisha. Anyway BF ni moja ya wanaofanya vema kwakuwa wana ofisi zao hapa dar. Ila kuhusu punguzo almost exporters wote wanatoa discount even more than 200$. Ila pia wabongo tupende kuwatumia wajasiliamali ktk sekta hii hasa kama umejiridhisha uhalali wao.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi nahitaji engine na giabox yake ya 3L pamoja na dashboard ya hilux 2.8 double cubin unaweza kuniagizia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna noma. Pesa namlipa directly muuzaji wa nje au inakuwaje?
Toyota Tundra, 2012 /petrol/4600cv/AT/USA/Left hand drive
JUMLA SH 78.8M HADI MKONONI NAKUKABIDHI.
Kuhusu malipo zipo njia mbili..ila ya kwanza tunapenda kuitumia , sisi tunaomba invoice ya kulipia na exporter wetu anatutumia na tunakupa wewe unalipia moja kwa moja kwa exporter....popote ulipo Tz, na unatukabidhi TT receipt kwa kututumia hata kwa whasap, ....ktk hayo malipo kuna commision yetu ndani tunayokuwa tumekubaliana na exporter wetu..hiyo unatutumia sisi au bank deposit. Baada ya week 4 original docs za gari yako zikifika tutakupa lakini pia tutazipeleka TRA kufanya assessment kwa TIN yako...tutakupa assessment form ili ukalipie mwenyewe popote ulipo Tz. Malipo ya clearing agent na bandari charges unatutumia sisi, kisha unangoja tukuite uchukue gari yako. Payment option no 2 tunatumia mkataba wetu wa kiofisi ,pesa ya kila awamu inadadavuliwa humo.
KWA UCHACHE TU ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hiyo imekaa byee mkuu,nilikuwa,nawaogopa nilijua ni wapigaji nikawa natumia,agents wa kitaa
 

Hapoo kwenye mkataba hapooo....
 
cheki Subaru Legacy moonroof s/wagon touring ile ya zamani kama 2006 kama itapatikana quote me we make business
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…