Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo amesema akichaguliwa kuwa Rais, mara baada tu ya kuapishwa siku hiyo hiyo atatangaza huduma za afya nchini kuanza kutolewa bure kwa watu wote bila malipo wala kutumia bima.
"Nikimaliza kuapa tu, dakika hiyo hiyo afya inakuwa bure na bill (malipo) ya siku hiyo ambayo mimi nimemaliza kuapwa haitalipwa. Dakika hiyo hiyo nitatangaza huduma za afya ni bure"
Gombo amesema hayo kwenye kipindi Maalum cha "Kiongozi 2025" kinachorushwa na TBC1.