Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
HUDUMA ZA AFYA MUSOMA VIJIJINI: ZAHANATI MPYA 17 ZINAENDELEA KUJENGWA
Huduma za Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini, lenye Kata 21 zenye vijiji 68, zinaendelea kuboreshwa kwa ushirikiano mzuri kati ya Wananchi na Serikali yetu.
Vijiji 17 vya Jimboni mwetu vimeamua kujenga zahanati za vijiji vyao, na baadhi ya vijiji hivyo tayari vimeanza kupokea michango ya ujenzi wao kutoka Serikalini.
Huduma za Afya Jimboni mwetu:
(i) Hospitali mpya ya Halmashauri/Wilaya (1):
+Imejengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti, Kata ya Suguti
(ii) Idadi ya Vituo vya Afya (6):
+Vimejengwa kwenye Kata za Bugwema, Etaro (Kisiwa cha Rukuba), Kiriba, Makojo, Mugango na Murangi
(iii) Idadi ya Zahanati (28):
(a) 24 za Serikali
(b) 4 Binafsi
Zahanati za Serikali 24 ziko vijijini Bugoji, Bugunda, Bukima, Busungu, Bwai, Chitare, Etaro, Kiemba, Kigera Etuma, Kiriba, Kome, Kurugee, Kwikuba, Mkirira, Mmahare, Mwiringo, Nyakatende, Nyambono, Nyegina, Rusoli, Seka, Suguti, Tegeruka na Wanyere
Vijiji vinavyojenga zahanati mpya (16):
+Zinajengwa vijijini Bulinga, Burungu, Butata, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kwikerege, Kurukerege, Kurwaki, Mabuimerafuru, Maneke, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu
WITO: UCHANGIAJI
Wadau wa Maendeleo, wakiwemo Wazaliwa wa Musoma Vijijini, wanaombwa wachangie ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya vijijini mwetu, ukiwemo ujenzi wa zahanati mpya - karibuni tuchangie sote!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatano, 18.9.2024