Huduma za kibingwa za MOI kuanza kutolewa Hospitali ya rufaa Nkinga - Tabora

Huduma za kibingwa za MOI kuanza kutolewa Hospitali ya rufaa Nkinga - Tabora

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
41c5dd8a-298c-44ed-88f2-a135a1a5e2a0.jpg

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) iko mbioni kusogeza huduma zake za kibingwa kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na mikoa jirani katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga ili kuwaondolea wananchi usumbufu na gharama kubwa kufuata huduma hizo Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amesema imekuwa azma ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma za kibingwa zinasogezwa karibu na wananchi na kuwaondolea usumbufu wananchi wa kuzifuata huduma hizo umbali mrefu.

Amesema "Tulipokea wito wa wenzetu wa Hospitali ya Rufaa Nkinga kuja kutembelea hospitali yao, kuona miundombinu na vifaa vilivyopo ili tuone namna bora ya kusogeza huduma zetu kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na mikoa jirani, leo tumetembelea hospitali hii na tumeona mazingira yao kwakweli wanafanya kazi kubwa na nzuri na sisi tunawaahidi kusogeza huduma zetu hapa kama ambavyo Serikali inaelekeza."

e0d3ae3c-1a7c-4c2c-93ee-1c7e7d3e60a1.jpg

Aidha, Dkt. Boniface amesema kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya na sekta nyingine ipo kwenye mchakato wa Bima ya Afya kwa wote ambayo itawapa wananchi uhakika wa matibabu ya kibingwa wakati wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya rufaa ya Nkinga, Victor Ntundwe amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious Boniface kwa kuitikia wito na ombi la kufika katika Hospitali ya Nkinga ili kuona namna bora ya kuanzisha ushirikiano ili kusogeza huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wakazi wa Tabora na mikoa jirani.

“Leo imekua siku ya pekee kwetu kwani tumempokea Mkurugenzi Mtendaji wa MOI na timu yake ambao pamoja na mambo mengine wametembelea hospitali yetu ili kuona ni namna gani tunaweza kuanzisha huduma za MOI hapa, kwakweli tumefarijika sana na tunaamini matunda ya ziara hii yataonekana siku si nyingi," alisema Ntundwe.
f5d64822-08f9-4782-86a4-698c339fbfd1.jpg

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Nkinga, Dkt. Tito Chaula amesema ushirikiano kati ya MOI na Nkinga utaleta tija kwani kwa kipindi kirefu wananchi wamekuwa wakipata usumbufu wa kufuata huduma mbali na kwa gharama kubwa hivyo kuanza kwa huduma za MOI katika hospitali hiyo kutamaliza changamoto hiyo.
 
Back
Top Bottom