Huduma za simu, ulaghai wa makampuni ya huduma hizo na hatma ya kulindwa kwa maslahi ya wateja

Huduma za simu, ulaghai wa makampuni ya huduma hizo na hatma ya kulindwa kwa maslahi ya wateja

Kobe_mzee

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2011
Posts
445
Reaction score
153
Ndugu zanguni Salaama?

Kwa muda sasa kupitia mwamvuli wa vigezo na masharti kumekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika bei za vifurushi vya mawasiliano kwa mitandao yote mikubwa, yaani: Vodacom, Airtel, na tiGo.

Kwa Mfano, kifushi cha Sh. 1000 kwa Airtel walianza kwa kutoa dk. 30, MB 250, na SMS kibao, baadae wakapunguza Mpaka Dk. 25, MB 100, SMS kadhaa, kwa Sasa ni Dk. 25 MB 8 na Sms kadhaa. Nilipowapigia Airtel na kuwahoji wakasema walikuwa kwenye promosheni!

Lakini hiyo imekuwa ni tabia (trend) kwa mitandao yote mitatu, na wimbo wao wa "MB 8 na dakika kiduchu"?. Je hii ni dhana ya soko huria au ni udhaifu wa MAMLAKA ZA UDHIBITI?? Au ndivyo vigezo na masharti katika sheria???

Suhisho:
Kama hatuna, nadhani sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha/kuimarisha JUMUIYA YA WATETEZI WA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA SIMU kisheria.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom