Huduma za Vivuko Kigamboni janga linaloenda kusababisha maafa nchini

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Nimeona Bashungwa kajitokeza fasta kusafisha anga baada ya Mwananchi kuja na makala hii, kweli uongozi mtamu! Malamiko kibao juu ya vivuko hivi hayaoni au? Ripoti ya CAG nayo ilieleza jinsi kivuko cha Azam kinavyolipwa baada vivuko hivi kuwa vichomi, leo anakuja kutuambia ni chuki binafsi?
--
Hii makala ilioandaliwa na gazeti la mwananchi ikilize hali ya usalama ya vivuko vinavyotumiwa Kigamaboni kama visipoangaliwa kwa jicho la tatu basi vitaenda kuleta maafa makubwa nchini

=====

1716893859419.png

Usalama wa zaidi ya watu 60,000 wanaotumia huduma ya vivuko kati ya Kigamboni na Magogoni kila siku upo shakani.

Mashaka ya usalama wa watu hao yanatokana na ubovu wa vivuko hivyo, unaosababishwa na kutofanyiwa matengenezo makubwa kwa mujibu wa sheria, ratiba na matakwa ya kitaalamu.

Hali hiyo inazua hofu ya kuharibika vivuko hivyo vikiwa safarini, kama ilivyowahi kutokea mara kadhaa vyombo hivyo vilipozima vikiwa na abiria katikati ya maji.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainika ukiukwaji wa sheria ya Solas ya mwaka 1974, kwa kuwa baadhi ya vivuko vinavyotoa huduma Kigamboni vimefikisha miaka sita bila kufanyiwa matengenezo makubwa, huku vikiendelea kufanya kazi, Mv Kigamboni kikiwa miongoni mwa hivyo.

Kama umewahi kuhisi maumivu ya kutwishwa mzigo mzito zaidi ya nguvu zako, basi hali hiyo ndiyo inayoukabili Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), katika jukumu la uendeshaji wa vivuko nchini.

Temesa inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake ya mwaka 2005, inayotaka pamoja na majukumu mengine ya msingi, wakala huo uwajibike na uendeshaji wa uhakika na usalama wa vivuko nchini.

Jukumu hilo la kisheria badala ya kuwa fursa ya mapato kutokana na makusanyo ya vivuko, limegeuka shubiri na mzigo mzito kwa Temesa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi kwa takriban miezi mitatu umebaini hilo.

Uchunguzi umefanyika kutokana na malalamiko ya wananchi wanaotumia vivuko hivyo, ambao mara kadhaa wameeleza kutoridhishwa na huduma inayotolewa.

Hoja kubwa ya watumiaji wa vivuko waliozungumza na Mwananchi ni kuchelewa kwa huduma wanapofika eneo la kuvuka, kuharibika mara kwa mara kwa vivuko na hata uchache wake.

====

Pia soma:
 
Tumuazime Dr Makonda she kutatua hilo tatizo mara moja
 
Maisha ya watumiaji wa vivuko yanewekwa rehani kabisa, nao kwa bahati mbaya wamekubali iwe hivyo, hawana namna nyingine ya kufanya.

Hapo tunasubiri litokee janga lingine kama yale ya meli zilizowahi kuzama miaka ya karibuni, taifa liingie kwenye maombolezo ya siku tatu, wanasiasa waongee ongee kama kawaida yao, kisha baada ya hapo maisha yaendelee kama kawaida huku tukisubiri janga lingine..
 
Nimeona Bashungwa kajitokeza fasta kusafisha anga baada ya Mwananchi kuja na makala hii, kweli uongozi mtamu! Malamiko kibao juu ya vivuko hivi hayaoni au? Ripoti ya CAG nayo ilieleza jinsi kivuko cha Azam kinavyolipwa baada vivuko hivi kuwa vichomi, leo anakuja kutuambia ni chuki binafsi?
--
Hii makala ilioandaliwa na gazeti la mwananchi ikilize hali ya usalama ya vivuko vinavyotumiwa Kigamaboni kama visipoangaliwa kwa jicho la tatu basi vitaenda kuleta maafa makubwa nchini

=====

Usalama wa zaidi ya watu 60,000 wanaotumia huduma ya vivuko kati ya Kigamboni na Magogoni kila siku upo shakani.

Mashaka ya usalama wa watu hao yanatokana na ubovu wa vivuko hivyo, unaosababishwa na kutofanyiwa matengenezo makubwa kwa mujibu wa sheria, ratiba na matakwa ya kitaalamu.

Hali hiyo inazua hofu ya kuharibika vivuko hivyo vikiwa safarini, kama ilivyowahi kutokea mara kadhaa vyombo hivyo vilipozima vikiwa na abiria katikati ya maji.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainika ukiukwaji wa sheria ya Solas ya mwaka 1974, kwa kuwa baadhi ya vivuko vinavyotoa huduma Kigamboni vimefikisha miaka sita bila kufanyiwa matengenezo makubwa, huku vikiendelea kufanya kazi, Mv Kigamboni kikiwa miongoni mwa hivyo.

Kama umewahi kuhisi maumivu ya kutwishwa mzigo mzito zaidi ya nguvu zako, basi hali hiyo ndiyo inayoukabili Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), katika jukumu la uendeshaji wa vivuko nchini.

Temesa inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake ya mwaka 2005, inayotaka pamoja na majukumu mengine ya msingi, wakala huo uwajibike na uendeshaji wa uhakika na usalama wa vivuko nchini.

Jukumu hilo la kisheria badala ya kuwa fursa ya mapato kutokana na makusanyo ya vivuko, limegeuka shubiri na mzigo mzito kwa Temesa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi kwa takriban miezi mitatu umebaini hilo.

Uchunguzi umefanyika kutokana na malalamiko ya wananchi wanaotumia vivuko hivyo, ambao mara kadhaa wameeleza kutoridhishwa na huduma inayotolewa.

Hoja kubwa ya watumiaji wa vivuko waliozungumza na Mwananchi ni kuchelewa kwa huduma wanapofika eneo la kuvuka, kuharibika mara kwa mara kwa vivuko na hata uchache wake.

====

Pia soma:
Punguen na nyie wengine wazaliwa kungekuwa hamna kifo tungekaaje ..
 
Hivi sisi ninini tunaweza? Labda rushwa na majungu
 
Back
Top Bottom