CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kupata wakati mgumu baada ya mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, aliyedaiwa kuwa si raia wa Tanzania, Dk. Hamisi Andrea Kigwangala kuwekewa pingamizi la kutogombea kiti hicho na vyama vya upinzani.
Vyama vya upinzani viliwasilisha pingamizi hilo jana, baada ya kutambua kuwa mgombea huyo alitumia jina la Hamisi Andrea likiwa ni la mkazi mmoja wa jimboni hapa.
Habari zinasema Dk. Kigwangala alikuwa akitumia jina la Said Nasoro tangu akisoma Shule ya Msingi Kitongo.
Chama kilichoanza kupeleka pingamizi katika ofisi ya Tume ya Uchaguzi wilayani hapa ni pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), baada ya mgombea wake, Kizwalo Dominic Clement kuwasilisha barua yenye kumbukumbu namba: CUF /NZG/KM/UCH/17/30 ya Agosti 20, kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa mgombea wake, John Massanja Mezza.
Barua ya CHADEMA yenye kumbukumbu namba MJM/CH/I ilisema chanzo cha pingamizi hiyo ni pamoja na kufanya udanganyifu wa jina pamoja na shule aliyosomea.
Inadaiwa kuwa Kigwangala alikuwa akiitwa Said Nassoro katika Shule ya Msingi Kitongo iliyopo mjini Nzega mwaka 1984 akiwa darasa la kwanza hadi la saba mwaka 1990.
Barua hiyo inasema: Mgombea huyu ni wazi kabisa amesoma Shule ya Msingi Kitongo mjini Nzega, kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba 1984-1990 na hakubahatika kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari akiwa anatumia jina la Said Nasoro, hapa hapana ubishi juu ya hili, kwa sababu aliosoma nao wapo na walimu wake wapo, ni ushahidi tosha.
Barua hiyo inaeleza aliyesoma shule hiyo yupo kwa jina hilo hilo la Hamisi Andrea na alihitimu masomo yake ya msingi mwaka 1991 na kufaulu na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kigoma.
Kilichofanyika ni kumdhulumu mwana kijiji huyu, kwani alipofuata masharti ya kujiunga na Idara ya Elimu Nzega, jibu alilopewa ni akasubiri barua nyumbani atatumiwa na idara hiyo, hadi leo hajatumiwa barua hiyo.
Inadhihirisha kwamba kwa kutopata msaada kutoka shule aliyosomea na kwa kutoelewa kwake, inaonyesha wazi Idara ya Elimu Nzega na Shule ya Msingi Mwanzoli kuna mchezo mchafu ulifanyika. Mgombea wa CCM, Kizwalo Dominic Clement, aliiambia Tanzania Daima kuwa:
Hapa kuna ushahidi wa kutosha kabisa ambao unakana kutosomea Mwanzoli Shule ya Msingi Ndugu Hamisi Andrea Kigwangara, kwani Hamisi Andrea halisi yupo, wanafunzi aliosoma nao wapo na walimu wapo hapa, sasa basi kwa hiyo tunaomba atenguliwe, pia ashitakiwe kwa kughushi elimu na kumdhulumu mwanakijiji huyu, alisema Kizwalo.