Tetesi: Huenda chama kipya cha Lissu kikasheheni watu waadilifu kama Dkt. Slaa, Prof. Safari, Mnyika, Heche, Wenje na wale wote waliotoka CHADEMA kwa figisu

Synonyms MP

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2024
Posts
320
Reaction score
346
Wasalaam, JF.

Wakati Tundu AM Lissu akiamua kuasisi chama kipya cha siasa na kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya vyama 20 vya siasa akianzia kukisimika chama hicho kipya mkoani kwake Singida kabla ya kuanza harakati Tanzania nzima.

Tayari baadhi ya watu waadilifu kama Dkt. Slaa, Prof Safari, Boniface Mwambukusi, John Heche, John Pambalu, Godbless Lema, wanatajwa kuwa Viongozi wa awali wa Chama hicho ambacho bado jina lake halijajulikana.

Mkakati huu unakuja baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika kukataa kuendelea kukaa ofisi kwa madai kwamba kazi zote za Katibu Mkuu anafanya Mpwa wa Mbowe ndugu John Mrema akisaidiwa na Bw Reginard Mtumishi ambae ni mjomba wa Freeman Mbowe.

Mkakati uliopo leo CHADEMA ni Freeman Mbowe kugombea tena nafasi ya Uenyekiti wa chama kwa mara ya nne mfululizo ukiacha mara mbili alizokuwa mwenyekiti kupitia BAVICHA na kufanya jumla ya mihula yote hiyo inamfanya Freeman Mbowe kuwa na miaka 30 kwenye uongozi wa CHADEMA bila kupisha yoyote kwenye uongozi Chama hicho.

Tundu AM Lissu ndio nembo pekee iliyosalia ndani ya CHADEMA ambayo imekuwa ikiibeba CHADEMA kama chama tangu kabla wakati na baada ya kupigwa kwake risasi 16 akiwa katika shughuli za kibunge Jijini Dodoma.

Kama Tundu AM Lissu ataihama CHADEMA basi huenda CHADEMA ikasalia kuwa kama CUF, NCCR na hata TLP kwa tayari imeshapoteza agenda yake ya Msingi ambayo ni kupinga Uzembe, Wizi na Ufisadi.

Tetesi za Mbowe kulamba asali ili aendelee kuwako CHADEMA kama Mwenyekiti ili kumdhibiti Tundu AM Lissu zimemlemea Mbowe na kuamua kurejesha Majeshi yake matiifu kutoka katika orodha ya Wabunge 19 waliofukuzwa.

Mbunge mmoja toka miongoni mwao jina tunalihifadhi anasema namnukuu "Halima ametuambia tusiendee CCM ila tumpambanie Mbowe awe mwenyekiti na Heche makamu ili amtoe Mnyika na Lissu ili turudi CHADEMA" mwisho wa kunukuu.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali zinaunga mkono Lissu kuanzisha chama chake hicho kipya kwani CHADEMA tayari imechafuka na imekuwa ngumu kuitofautisha na Chama tawala cha CCM kimaadili na kimwenendo na hivyo kupoteza tafsiri ya neno "Upinzani"

Tundu AM Lissu anasifika kwa kukemea rushwa na ufisadi ndani na nje ya CHADEMA waziwazi na ndio turufu pekee inayomfanya azidi kuaminika na kipendwa zaidi na Watanzania hasa wa tabaka la chini.

Kitendo hicho kinampa wakati mgumu zaidi Mwenyekiti wa Sasa Freeman Mbowe ambae Uadilifu wake na nyendo zake hasa awamu hii ya sita zinamashaka mengi kutokana na tuhuma nyingi za ulambaji wa asali kwa maeneo na nyakati tofauti tofauti.

Mbowe anaamini mfumo sasa uko tayari kupeleka dola CHADEMA wakati Lissu anaamini mfumo ndio CCM na CCM ndio mfumo wenyewe.

Lissu anaamini katika kutwaa dola kupitia Wananchi wakati Mbowe anaamini katika kutwaa dola kupitia mfumo au dola yenyewe.

Kitendo cha Lemma kujitoa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Kanda ya Kask ni ishara inayoakisi ninachokiandika hapa kwani ni dhahiri ananga'tuka CHADEMA na kuelekea kwenye hicho chama jipya,

Tanzania inahitaji upinzani safi sio bora upinzani, ndio maana waliwakataa CUF, wakawakataa NCCR na hivyo hivyo wakafanya kwa TLP na leo hii ni zamu ya CHADEMA kukataliwa wazi wazi

CHADEMA ndio chama Cha upinzani kinachomiliki mwenyekiti mmoja kwa miaka 30 huku wakiranda randa kuomba katiba mpya kwa wananchi wakati katiba yao inamatundu kama chekecheo.
 
Kama kitaanzishwa chama kipya.
Dr slaa,
profesa Safari
Wakiwa ndani ya hicho chama basi CCM 2025 watakuwa na hali mbaya sana.
Tatizo la sasa CCM hatuwataki na CHADEMA hawaaminiki. Hapo ndipo ccm wanapookota point za bure.
Hakuna CCM nyepesi kuitoa madarakani kama huu ya Samia. Tena inatolewa kwa kutumia katiba hii hii.
Aulizwe mzee wa Msoga kilichomkuta 2010
 
Ila kwanini Mbowe asipishe kama kweli anakipenda chama chake?

Nakumbuka story ya Mfalme Suleiman na Wanawake wawili waliogombea mtoto.

Stori iko hivi,

Wakati Wanawake hao wawili wamelala wakiwa na watoto wao wachanga,

Mwanamke mmoja akamlalia na kumbana mtoto wake akafa.

Mwanamke huyo alipogundua mtoto wake amekufa akamchukua yule mzima wa rafiki yake na akamuwekea huyo wake aliyekufa.

Palipokucha wote wawiwili wakaanza kugombania mtoto huyo aliye hai.

Ikawabidi waende kwa mfalme ili kuamuliwa yule mtoto ni wa nani?

Walipofika mbele ya Mfalme,

Mfalme akasema nileteeni Upanga.

Akawaambia mleteni huyo mtoto,

Sasa ninamchana vipande viwili ili Kila mmoja apate kipande sawa.

Ghafla yule mama mwenye mtoto akasema mwache mwanangu usimuue mpatie huyu Mama aende nae.

Mfalme akampata mama mwenye mtoto kuwa ni huyu aliyesema usimuue mpe tu huyu ili aishi.

Ukitaka kujua Mbowe hana mapenzi na CHADEMA angalia anavyoiweka hatarini CHADEMA kwa masilahi yake kwa kisingizio Cha hawaamini wenzake wote.
 
Wao wangeungana na Act Wazalendo bado wangefanya vizuri
 
Aisee funzo kubwa sana hili
 
 
Kuna watu wazito sana umewataja na wenye maadili

Hawawezi kuongozwa na mtu mwenye mitusi, mropokaji na asiye na agenda zaidi ya uanaharakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…