Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mjadala wa sasa ni kuhusu Feisal kuondoka Yanga, huku akihusishwa kutaka kuhamia Azam FC. Sio yeye Feisal wala Azam Fc waliosema kuhusu Feisal kuhamia Azam Fc bali ni tetesi za mitandaoni za mashabiki.
Kwa udadisi wangu nahisi huu ni mchezo tu ili kutupoteza maboya, lakini lengo halisi la Feisal ni kutimkia nje ya nchi hususani Afrika kusini, Afrika kaskazini au Uarabuni.
Haya yote yanatokea kwa sababu viongozi wa Yanga wameendelea kumng'ang'ania Feisal bila kuwa na mpango bora wa maisha yake ya kisoka na kimaisha.
Nyuma ya pazia Azam FC inahusishwa kama plan B tu, yaani akiwa dili la Feisal kwenda nje litakwama au kuchelewa basi atatua Azam kwa mpito.
Upande wa pili, wakala wa Feisal kufanikisha hili deal huenda anahusishwa na mmoja wa kiongozi wa Yanga au Azam Fc.
Kilichotokea kwa George Mpole akiwa na klabu ya Geita Gold Mining huenda kinakwenda kutokea kwa Feisal.
Muda utatoa majibu.