Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,641
Yaani Watoto wamekaa karibia Miezi Mitatu bila Masomo, huku wengi Wao wakiwa tayari wameshaathirika Kisaikolojia kulingana na Hofu iliyokuwepo na bila shaka wengine hata Topiki zao hawakumaliza anatokea Mtanzania Mmoja anasema watafanya Mtihani yao Wiki chache zijazo.
Hivi hawa Watoto walitakiwa wajengwe Kwanza Kisaikolojia kutokana na Janga lililopo huku wakipewa muda wa Kujiandaa angalau hata Mwezi Mmoja ua Miwili au Waharakishwe Kufanya Mitihani yao kwa Shinikizo tu la Siasa na Maandalizi yetu ya Uchaguzi Mkuu ujao?
Kwa haya Maamuzi yaliyofanywa hivi leo nayaona mambo mawili Makuu ambapo kuna uwezekano Wanafunzi hawa Wakafeli kuliko ilivyowahi kutokea katika Historia ya Elimu (Taaluma) nchini au Wakafaulishwa (Wakabebwa) ili mradi tu Kuwahi muda na Kumfurahisha Mheshimiwa Rais JPM.
Taratibu sasa naanza Kuwadharau Wasomi Wetu wenye Doctorates (PhD's) zao na wenye Dhamana Kisiasa Nchini Tanzania.