mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Nimekuwa nafuga kwa miaka mingi sasa , kiufupi nimerithi hii shughuli , kinachoshangaza ni kunishitua ni gharama za ufugaji zinapanda hadi sio vizuri hapa nazungumzia ufugaji wenye akili sio ule wa kisukuma na kimasai 1.bei ya mifugo mfano bei ya ndama dume wa kisasa mwenyew wiki Moja ni elfu 50000 to laki Moja , then bei zinaenda juu kutegemea na umri na hali yake kiafya 2. Bei ya ndama jike ni laki nne huyo ni mwenye miezi mitatu kwenda juu kutegemea na umri na hali yake kiafya,. 3 jichanganye kutafuta mitamba na ngombe wa maziwa bei zinakatisha tamaa, mfano mzungu pale iringa Philips anauza hadi Milion Tano. Hizo bei za mifugo then let's turn kwenye malisho , lipa mfanyakazi , nunua pumba , nunua mashudu, nunua madini, pelaka maji , na kibaya kuliko vyote serikali imeruhusu watu kutoka nje kununua hizo supplement mfano ukingia sasa mbeya, mbarali , tunduma wamejaa maa agents wanakusanya pumba wanapatia wakenya , na mbaya zaidi product za mifugo yetu zinapata ushindani toka nje yaani Tanzania wanagiza maziwa, nyama za kopo etc matokeo yake tunauza na kupata faida kidogo sana, yaani unaweka Milion hamsini unapata faida Milion mbili na kama ununuzi wa concentrate kama pumba, mashudu utaendelea hivi wengi tunaenda kimbia